Pre GE2025 CHADEMA ni Wakati wa Kwenda na Lissu. Msisite, nina sababu…

Pre GE2025 CHADEMA ni Wakati wa Kwenda na Lissu. Msisite, nina sababu…

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sema mpambano utakuwa mkali sana. Waibaji wasipokuwa makini wanamuongezea TAL badala ya atakaye simama hapo Lumumba
 
Kuna wanaosema Mbowe ndo awe mgombea Kwakuwa Lissu aligombea wakati uliopita Ila wakumbuke
Mbowe aligombea 2005. Hata hivyo Tundu Lissu bado relevance yake ipo na anao mvuto ambao ni wa kipekee kwa sasa. Ni mzuri sana kwenye kuvuta attention ya watu kumsikiliza anapokuwa anaongea na hugusa maeneo ambayo hugusa hisia za walio wengi! Lakini Chama chao kitaona nani anwafaa!

Ulikuwa ushauri wangu tu 2025 Lissu anafaa na ataleta changamoto kubwa kwa CCM,

Britanicca
Ni ushauri mzuri kabisa.

Mbowe. Hapana. Hiyo itakuwa ni mbinu ya kumsaidia tu Samia kubaki madarakani; hata pengine kwa mategemeo/ahadi kwa CHADEMA kukaribishwa/kujumuishwa serikalini kwa mtindo ule ule unao tumika Kenya.
 
Nafikiri Bw. Tundu Lissu, CHADEMA, pamoja na wanachama wengine wa vyama vya Siasa hususani wapinzani kwa sasa hivi wajikite zaidi Kupigania upatikanaji wa Katiba Mpya itakayokuwa nzuri. Waachane na haya mambo ya kutaka kugombea vyeo, wafikirie suala la kubadilishwa kwa Katiba ya nchi kwanza ndipo masuala mengine yafuatie.

Tundu Lissu anataka kugombea Urais kwa kupitia kwenye Katiba ipi ambayo anafikiri kwamba atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi endapo kama atapata kura nyingi zaidi? Kwa sababu Katiba iliyopo hivi sasa hairuhusu jambo hili kufanyika. TAL Atakuwa anajisumbua nafsi yake bure na kupoteza wakati wake na rasilimali zake bure kabisa. Kwa Katiba hii iliyopo hapa Tanzania hata kama atapata Kura kwa Asilimia 99 ya Kura zote kabisa za Wagombea wa Kiti Cha Urais, KAMWE hataweza kutangazwa kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi kwa kiti Cha Urais. Badala yake Mgombea wa CCM ndiye atakayetangazwa kuwa ni Mshindi.
Kwa hiyo waache kujiandaa na uchaguzi ambao upo miezi mitatu ijayo (serikali za mitaa) na ule wa mwaka mmoja ujao badala yake watulie na kitu kimoja kuendelea kupigania katiba mpya tu kwa kuwa hawatatangazwa katika uchaguzi.?

Sijaelewa unafikiri kwa kukutumia nini wewe.

Ni lazima tupambane kwa mazingira haya haya. Hata nyakati zilezile kina Hayati Mwl. J. K. Nyerere wanapambania uhuru wa Tanganyika, mazingira yalikuwa magumu na giza kwa namna hii hii..

Lakini hawakusema "tutawaweza vipi hawa wakoloni wenye silaha na pesa huku sisi tukiwa hatuna chochote na wakati mwingone tukitembea kwa miguu kilometa nyingi ku - mobilize wananchi kuiunga mkono TANU na harakati zake za kudai uhuru".

Wangekuwa na mawazo kama yako, leo Tanganyika tungekuwa bado ni koloni la Mwingereza..!

Tuwaunge mkono CHADEMA kupambana ktk mazingira haya haya. Tukitaka mshindi lazima atangazwe, itakuwa hivyo. Na hii inawezekana iwapo kutakuwa na mass mobilization yaani - NGUVU YA UMMA..

Iliwezekana Kenya, Zambia, Ghana, South Africa na kwingineko. Sisi tunashindwa nini iwapo tuna watu aina ya Tundu Lissu wanaoweza kushawishi na ku-mobilize watu..

Yote yafanyike kwa wakati mmoja. Kushiriki chaguzi na kupigania katiba mpya..
 
Tundu Lissu anataka kugombea Urais kwa kupitia kwenye Katiba ipi ambayo anafikiri kwamba atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi endapo kama atapata kura nyingi zaidi? Kwa sababu Katiba iliyopo hivi sasa hairuhusu jambo hili kufanyika.
Hiyo katiba inayo madaraka kuzidi madaraka ya wananchi?
Hata sielewi unazungumzia kitu gani hapa!
 
Sheria za uchaguzi ndio kikwazo cha upinzani kuingia ikulu, jina la mgombea wa upinzani halijawahi kuwa tatizo.
Na hii ndiyo ingekuwa ni ajenda kuu ya CHADEMA kuanzia sasa hadi uchaguzi kuisha.

Bila kujali hizo sheria za uchaguzi, CHADEMA wajikite katika HAKI za wananchi kupiga kura; na usalama wa kura hizo.
Kama hizo kura zinaharibiwa kwa sababu ya "sheria za uchaguzi", hizo si sheria bali ni maelekezo ya uhalifu, ambao ni HAKI ya wananchi kuukataa na kuuzuia.

Ni hivi: Mimi nawasihi CHADEMA wawahimize waTanzania wengi sana kwenda kupiga kura kuchagua viongozi wao wanao wataka wao.
Wananchi hao hao wahimizwe kuhakikisha kuwa kura zilizo pigwa zina hesabika na mshindi kutangazwa bila ya hila!

Ni wananchi wenye uelewa pekee wanao weza kuifanya kazi hii, na hizo "sheria za uchaguzi" hazina zuio lolote wakiazimia kulinda haki zao zisivurugwe.
Mimi naamini inawezekana sana; hasa katika huu uchaguzi unaofuata.
 
Hata hili pia sio Tatizo. Shida inajulikana illipo
 
Kisu he is not presidential material
 
Kuna wanaosema Mbowe ndo awe mgombea Kwakuwa Lissu aligombea wakati uliopita Ila wakumbuke
Mbowe aligombea 2005. Hata hivyo Tundu Lissu bado relevance yake ipo na anao mvuto ambao ni wa kipekee kwa sasa. Ni mzuri sana kwenye kuvuta attention ya watu kumsikiliza anapokuwa anaongea na hugusa maeneo ambayo hugusa hisia za walio wengi! Lakini Chama chao kitaona nani anwafaa!

Ulikuwa ushauri wangu tu 2025 Lissu anafaa na ataleta changamoto kubwa kwa CCM,

Britanicca
Labda watakusikia...Nchi inamuhitaji yule kijana/mzee- Lissu aje atunyooshee mustakabali na njia ya maendelo yetu...Maliasili zetu zinakwisha na hatuoni mtanzania mmoja mmoja ananufaikaje na utitili wa maliasili zetu kama wenzetu wa kule Norway wanavyogawiwa na serikali yao matunda ya rasilimali zao...

Labda Lissu ataweza... CCM wameshindwa kutugawiya mapato ya huo uwekezaji...wao ni kupugia tu wenyewe kwa wenyewe. Hata yule professor Palamagamba Kabudi aliyeileta ile sheria ya kulinda maliasili akakaa kimya wakati bandari zetu, Mbuga zetu, madini yetu, yote yamepigwa mnada... sijui tunaelekea wapi ikiwa hata wale tulio dhani watatusaida nao ni domo zege...

Huyu Lissu anafaa kwa sasa au ndugu yake Mwabukusi kama Lissu hawamtaki...
 
Hiyo katiba inayo madaraka kuzidi madaraka ya wananchi?
Kwa Tanzania, jibu ni ndiyo, Katiba ya nchi hii ina madaraka makubwa zaidi kuzidi madaraka ya Wananchi.

Hata sielewi unazungumzia kitu gani hapa!
Wewe ndio hauelewi na wala haueleweki unazungumzia kitu gani. Inavyoonekana hata haujui nguvu iliyonayo Katiba ya nchi hii kuhusiana na suala hili la Chaguzi za Siasa.
Na hii ndiyo ingekuwa ni ajenda kuu ya CHADEMA kuanzia sasa hadi uchaguzi kuisha.

Bila kujali hizo sheria za uchaguzi, CHADEMA wajikite katika HAKI za wananchi kupiga kura; na usalama wa kura hizo.
Kama hizo kura zinaharibiwa kwa sababu ya "sheria za uchaguzi", hizo si sheria bali ni maelekezo ya uhalifu, ambao ni HAKI ya wananchi kuukataa na kuuzuia.

Ni hivi: Mimi nawasihi CHADEMA wawahimize waTanzania wengi sana kwenda kupiga kura kuchagua viongozi wao wanao wataka wao.
Wananchi hao hao wahimizwe kuhakikisha kuwa kura zilizo pigwa zina hesabika na mshindi kutangazwa bila ya hila!

Ni wananchi wenye uelewa pekee wanao weza kuifanya kazi hii, na hizo "sheria za uchaguzi" hazina zuio lolote wakiazimia kulinda haki zao zisivurugwe.
Mimi naamini inawezekana sana; hasa katika huu uchaguzi unaofuata.
You are completely Wrong and out of point.

CCM kuendelea kubaki madarakani au kushinda kwenye suala la Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania wala haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi iliyopo hivi sasa, Hata kama Tundu Lissu atapigiwa Kura na kupata ushindi wa asilimia 100 ya Kura zote kabisa kwa kiti Cha Wagombea Urais na CCM ikapata asilimia sifuri, bado na KAMWE Tundu Lissu hataweza kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa Uchaguzi kwa kiti Cha Urais. Badala yake Mgombea wa CCM ndiye atakayetangazwa kuwa ni mshindi, na Tundu Lissu pamoja na Wapiga Kura wake hawataweza kufanya kitu chochote kile.
Hivi nikuulize swali; Je, Maalim Seif kwenye Uchaguzi wa Siasa wa Mwaka 2015 kule Zanzibar hakupata Kura nyingi kumzidi mgombea wa Urais kutoka CCM? Je, Maalim Seif alitangazwa kuwa ndiye mshindi wa Uchaguzi huo??? Kwa nini? Kwani Maalim Seif alifanya Nini baada ya Jecha kuchukua Uamuzi aliochukua kuhusiana na Uchaguzi huo??

Nakukumbusha: "No research no right to speak"
Mao Zedong
 
Back
Top Bottom