John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Wewe pamoja na wana-Chadema wenzako mnajidanganya bure. Kupigania upatikanaji wa Katiba Mpya ndio Jambo la msingi zaidi kwa sasa hivi hapa Tanzania, ndipo mambo mengine yafuatie.Kwa hiyo waache kujiandaa na uchaguzi ambao upo miezi mitatu ijayo (serikali za mitaa) na ule wa mwaka mmoja ujao badala yake watulie na kitu kimoja kuendelea kupigania katiba mpya tu kwa kuwa hawatatangazwa katika uchaguzi.?
Sijaelewa unafikiri kwa kukutumia nini wewe.
Ni lazima tupambane kwa mazingira haya haya. Hata nyakati zilezile kina Hayati Mwl. J. K. Nyerere wanapambania uhuru wa Tanganyika, mazingira yalikuwa magumu na giza kwa namna hii hii..
Lakini hawakusema "tutawaweza vipi hawa wakoloni wenye silaha na pesa huku sisi tukiwa hatuna chochote na wakati mwingone tukitembea kwa miguu kilometa nyingi ku - mobilize wananchi kuiunga mkono TANU na harakati zake za kudai uhuru".
Wangekuwa na mawazo kama yako, leo Tanganyika tungekuwa bado ni koloni la Mwingereza..!
Tuwaunge mkono CHADEMA kupambana ktk mazingira haya haya. Tukitaka mshindi lazima atangazwe, itakuwa hivyo. Na hii inawezekana iwapo kutakuwa na mass mobilization yaani - NGUVU YA UMMA..
Iliwezekana Kenya, Zambia, Ghana, South Africa na kwingineko. Sisi tunashindwa nini iwapo tuna watu aina ya Tundu Lissu wanaoweza kushawishi na ku-mobilize watu..
Yote yafanyike kwa wakati mmoja. Kushiriki chaguzi na kupigania katiba mpya..
Hauwezi kununua mabehewa na injini za kuvuta mabehewa Kabla ya kutengeneza na kutandika mataluma ya reli kwanza halafu utegemee kwamba mradi wa usafiri wa treni utakamilika na kutoa matunda mazuri. Never happen.
Ili mtoto azaliwe ni lazima ujauzito utungwe kwanza! Mwanamke asitarajie kupata mtoto wake wa kumzaa bila ya yeye kubeba ujauzito kwanza.
It's a pipedream!
Hiki wanachofanya CHADEMA kwa sasa hivi ni sawa na kusema kwamba "wanataka mtoto lakini hawataki kubeba ujauzito."
Hii inawezekana vipi ?