Mkuu bado kidogo utaokota makopo sasa. Umefikia stage ya kuokoteza ''uchafu'' kama huu ili tu kuonyesha Lissu hafai? Anyway, hili mbona tulilitegemea sana! Au sahihi niseme bado kuna vita kubwa inaandaliwa na timu ya Mbowe ili kuonyesha tu kuwa ilikuwa ni makosa kumchagua Lissu na Chadema inakufa. Kwa kushirikiana na vyombo vya dola, Mbowe atahakikisha Chadema inayumba au hata kufa ili yeye aonekane ni shujaa. Hata ikitokea Mbowe akafaniwa, lakini sisi wananchi tumepata ushindi mkubwa wa kujua ukweli ulikuwa umefichwa nyuma ya pazia i.e. tungepoteza muda na mali yetu kusubiri mabadiliko kutoka kwa uongozi wa Mbowe. Mimi hata Chadema chini ya Lissu ikifa leo sitasikitika sana kwani najua kabisa ndiyo utakuwa mwanzo wa mabadiliko ya kweli kwa sababu kokoro la CCM haliwezi kumbeba kila mtu.