Tetesi: CHADEMA ‘Nusu Mkate’ wote wanahamia CCM February 5 akiwemo Wenje, Sugu na Boni Yai

Punguza mihemko.Kama vip Hebu kua wewe sehemu ya hayo mabadiliko badala yakushutumu watu bila uthibitisbo kwasababu tu ya mihemko yako.
 
Lusungo ana maumivi kibao na sasa hivi adui yake ni Chadema. Kwake bora CCM kuliko Chadema. Hao hao kina Lusungo sasa wanasema ni chama cha wakristo.
Kwakweli nimemshangaa sana namna alivyoweza kubadirika ghafla na kuwa adui wa Lissu

Yeye shida yake ni Lissu, amekuwa akimnanga humu na kumfungulia nyuzi Kila Siku yeye na mwenzie wakuitwa Malaria 2

Kwakweli ningependa Mungu awape maisha marefu waje waione Chadema mpya ya kitaasisi itakayokuwa sehemu kubwa ya maamuzi ya Nchi kuelekea 2030
 
Siwezi kumpa ushirikiano jitu tapeli na laghai…. Tutahakikisha anashindwa.
Unaweza kutushawishi na sisi wengine Kwa kutuonesha huo ulaghai wake na Utapeli ili nasi tukuunge Mkono?
 
Unataka kuniambia Nasari na Boni Yai nani aliifaidi Chadema?

Yupo wap Nassari mkuu?
Mimi aliniacha hoi Machali tu. Alivyokua anaitukana CCM na viongozi wake na viongozi wa Serikali sikutegemea.
Ila baadae sana nikagundua kumbe ni afisa kipenyo alikua kule kwa kazi maalum.
TISS Bongo SHKAMOOO.
Sitashangaa hata kidogo nikija kusikia Lissu nae ni Afisa Kipenyo.
 
Reactions: Tui
Nashukuru kuweka kumbuka sawa, lakini hoja ya Uchaga ilikita mizizi Chadema labda kwakuwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake alikaa miaka mingi madarakani
huya wa sasa ni mnyaturu, sijui watamnasibisha na nini zaidi ya ubeberu wanaomtwisha nao maana wanyaturu hawana time na chadema kama ilivyokuwa wachaga na chadema. Propaganda ni nyingi wahuni hawakosi kumtwanga nazo
 
Nyuzi za hovyohovyo kama hizi zimekithiri JF
 
huya wa sasa ni mnyaturu, sijui watamnasibisha na nini zaidi ya ubeberu wanaomtwisha nao maana wanyaturu hawana time na chadema kama ilivyokuwa wachaga na chadema. Propaganda ni nyingi wahuni hawakosi kumtwanga nazo
Sasahivi wanamtwisha mzigo wa ubeberu mara ushoga

Hata humu JF nimewasikia wakisema

Kwa hali ya Nchi ilipofikia, tunahitaji Kiongozi msafi anayeweza kukataa na kupinga rushwa waziwazi kama ilivyo Kwa Lissu
 
Itakua jambo jema Sana cdm ikianza upya! Watu wa Mbowe wote waende CCM. Maana mpango wao kuuza cdm kwa CCM umefeli.
 
ni kweli wapo watakaohama, ni haki yao.

mafuta na maji kujitenga ni jambo zuri
 
wapeleke uhuni wao huko na njaa zao kali, povu sitaki
 
Kila mtu anahaki ya kuhamia popote. Hata wakitaka waende chaima wabakie hawana chama waache siasa.

Hakuna atakaye wahukumu, watakuwa wametimiza haki zao kama ambavyo wametiza wajibu zao walipokuwapo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…