Hawa watu wa SGR waoga sana. Ila jamani Hawa viongozi wa juu inabidi wafanye ziara kwenye ngazi ya kijiji labda watagundua matatizo ya watanzania. Katika ngazi hizo hali si mbaya sana. Hakuna Maji, Zahanati na Vituo vya Afya, Shule za msingi mbovu, Sec hakuna, barabara mbovu mpaka inahuzunisha.
Hawa viongozi hasa RAIS, MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU wafanye angalau ziara kwenye wilaya 5 kila mmoja kwa KANDA tena wafike mpaka kwenye vitongoji vyake vyote wajionee maisha wanayoishi Wanyonge wa hii Nchi wakiwa na DIARY ili kuandika watakayoyaona naamini itawasaidia sana kusaidia hawa watu maana hawa wawakilishi hawajali hawa watu.
Hali bado ni mbaya sana kwa kweli wanahitaji msaada wa haraka sana.
Bila ziara kwenye hayo maeneo hakuna kitakacho fanyika asilani.