Watanzania wanajua na pia dunia inajua kuwa CCM ni chama ambacho kinalazimisha kubakia madarakani kwa hila. Viongozi wake hawana tena mvuto wala ushawishi mbele ya wananchi, kama kuna mgombea ambaye angalipaswa kuitwa na kamati ya maadili na hata kuadhibiwa, tena mapema sana ni mgombea wa CCM.
Wote tu mashuhuda ya kwamba, ijapokuwa yupo ktk kinyang'anyiro cha nafasi ya uraisi na wagombea wengine wa nafasi hiyo nyeti, yeye bado anatembea kwa kuvuli cha uraisi na siyo kama mgombea kama wengine. Anakiuka maadili kwa kutoa rushwa hadharani. Anatoa amri za kiimla na kulazimisha fedha zitolewe ktk kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ktk maeneo anayopita.
CDM ni lazima wawe wavumilivu na watulivu kwa siku hizi saba. Wanapaswa waendelee na kampeni za nguvu ktk maeneo yote ya kimkakati kupitia kwa mgombea mwenza na viongozi wengine maarufu wa kitaifa. Tundu Lissu bado ni tishio kubwa sana kwa CCM, kwa hiyo pale atakaporudi jukwaani ataleta hamasa kubwa sana ktk kipindi hiki cha lala salama.
Ni lazima watumie busara na hekima ktk hili ili kuepuka na hata chama kuweza kuadhibiwa kwa hila kama hiyo ya awali iliyotumika kwa Tundu Lissu. "Stitch in time saves nine". Umma wa Watanzania upo bado na Tundu Lissu, hadi kieleweke na Nduli apate kuondolewa ikulu.