Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tunamuunga mkono Maalim Seif kwa Urais Zanzibar. Lissu hataendelea na kampeni, atapangiwa majukumu mengine

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tunamuunga mkono Maalim Seif kwa Urais Zanzibar. Lissu hataendelea na kampeni, atapangiwa majukumu mengine

Ccm chama mfu , tumeccm , policcm ,tissccm msaada kila upande .Kumbukumbu hizi zimetunzwx kwa matumizi ya baadaye huko the Hague .
IMG_20201004_081002.jpg
IMG_20201004_080635.jpg
 
Lissu na CHADEMA sio wapuuzi kama ccm na vijana wake wa Lumumba ndio maana wameweza kuwa chama kikuu cha upinzani kilicho tishio na chenye nguvu sana
Kumbe Chadema ni cham cha upinzani na sio chama tawala. Chama Cha upinzani ni dhaifu haswaa
 
Kakati kuu wamekosea sana, sijajua samewaza nini kutoa uamuzi kama huo. Huu uamuzi utarudisha nyuma sana ari iliyopo
 
Watanzania wanajua na pia dunia inajua kuwa CCM ni chama ambacho kinalazimisha kubakia madarakani kwa hila. Viongozi wake hawana tena mvuto wala ushawishi mbele ya wananchi, kama kuna mgombea ambaye angalipaswa kuitwa na kamati ya maadili na hata kuadhibiwa, tena mapema sana ni mgombea wa CCM.

Wote tu mashuhuda ya kwamba, ijapokuwa yupo ktk kinyang'anyiro cha nafasi ya uraisi na wagombea wengine wa nafasi hiyo nyeti, yeye bado anatembea kwa kuvuli cha uraisi na siyo kama mgombea kama wengine. Anakiuka maadili kwa kutoa rushwa hadharani. Anatoa amri za kiimla na kulazimisha fedha zitolewe ktk kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ktk maeneo anayopita.

CDM ni lazima wawe wavumilivu na watulivu kwa siku hizi saba. Wanapaswa waendelee na kampeni za nguvu ktk maeneo yote ya kimkakati kupitia kwa mgombea mwenza na viongozi wengine maarufu wa kitaifa. Tundu Lissu bado ni tishio kubwa sana kwa CCM, kwa hiyo pale atakaporudi jukwaani ataleta hamasa kubwa sana ktk kipindi hiki cha lala salama.

Ni lazima watumie busara na hekima ktk hili ili kuepuka na hata chama kuweza kuadhibiwa kwa hila kama hiyo ya awali iliyotumika kwa Tundu Lissu. "Stitch in time saves nine". Umma wa Watanzania upo bado na Tundu Lissu, hadi kieleweke na Nduli apate kuondolewa ikulu.
Good thinking 'hiyo kwa kinyakyusa tunaita strategy formulation'
 
Na
Sasa mkuu kama unachokisema hapa ni kweli,jaribuni kutafuta namna ya kupata haki yenu kwa vyombo husika/mamlaka za juu,


Ujinga huo unafanywa na baadhi ya watendaji kwa tamaa zao binafsi na si kwamba wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria,


Fuatilieni bila kuchoka mtapata tu haki yenu na hao jamaa watachukuliwa hatua
Asante sana kk lakini hatuna chakufanya ilihali kunawatendaji wa vijiji hadi kàta kazi piakunabwanasamaki wote hawa wameshuhudia ambaokesho ndiomashahidi wangu hawakutoa msaada kwahalihiyo unawezanyanyua mguu kweli?
 
Amani kwako.

Ikumbukwe kuwa mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa na late Mwl. Nyerere ilikuwa na lengo la kukubali na kuonyesha dunia kuwa Tanzania ina demokrasia.

View attachment 1589660
Pichani: late Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.

Siasa ina mchezo wa giza na nuru, vile vinavyofanywa gizani huwezi kuviona isipokuwa vya nuruni hapo ndipo mada imesimama.

Tukumbuke mwasisi wa uanzishwaji vyama vingi ni CCM, kupitia viongozi wake akiwepo fundi wa siasa late JKN, mzee baada ya kuambiwa na wahisani wape wananchi uhuru wa kuchagua, wakaona isiwe tabu, wakadesign na kuchambua matokeo yake ni vyama vingi ila vyama vyenyewe ni mali ya ccm.

Kuna late Kambona huyu jamaa angeweza kuwa mpinzani mahiri tatizo lake alikuwa na uroho wa madaraka mpaka alipotoka kwenye chama na kutaka kuingia msituni, tunajua kilichofuata baadaye.

View attachment 1589659
Pichani: late Oscah Kambona

CCM imekuwa ikiwekeza kimkakati kuonyesha wahisani kuna demokrasia ya ushindani na ndiyo maana kuna vyama vipo vipo tu havina hata mjumbe wa nyumba kumi na kila uchaguzi lazima waingize mtu kugombea urais wakijua hawapati kitu ila wanachukua fomu, mwenye uelewa unapata jibu hapo.

Wagombea urais wote waliopita dr. Wilbroud Slaa mpaka Lowassa walikuwa ni purely uccm na walikuwa kimaslahi, hivyo mfumo wa ccm uliweza kuwabeba, muite, mtulize mpe chake aondoke. Tundu Antipas Lissu siyo zao la ccm japo kakua akiongozwa na mfumo huo, ule mfumo wa muite, mtulize, mpe chake aondoke umeharibika baada ya kumchapa risasi na kushindwa kumuua, hapo ndipo shida kubwa imekuwa.


View attachment 1589661
Picha: Tundu Antipas Lissu.

Siasa ya vyama vingi hapa Tanzania haipo ila inakuja kuwa kweli kupitia watu kama Lissu mtu ambaye hawezi kununurika kupitia ile njia ya MMMa, sababu mojawapo inayogoma ni pale walipojaribu kumuua, upande wa wananchi wanafunguka na kufanya kweli, ila viongozi wa vyama hawana kauli thabiti pale kura zao zinapoibiwa au kubadilishwa.

Lissu ameamua kufanya mageuzi ya kweli katika mfumo usio sahihi na inaweza kuwa kweli mfumo huo ukambeba kupitia wananchi, kwa nini Mbowe as chairman nk wapo kimya au wanatoa maamuzi kimya kimya kwa mfumo wa ki_CIA hatujui!, ila jawabu mojawapo ni ile dhana ya MMMa, ambayo wapinzani wengi wamekuwa wanufaika na mpango huo wa mafao ya chukua kaa pembeni.

Njaa nayo mbaya, au ni ile dhana niliyoandika hapo juu ambayo muanzilishi wa vyama ccm anacheza unfair na tunaona wakongwe wengi wakishafanya yao, baadaye wanarejea nyumbani na kupewa kiinua mgongo kama nyadhifa kubwa kubwa wengine mabalozi, mawaziri nk, hapo ndipo unapata picha kuwa hii siasa ya vyma vingi hapa nchini ni changa la macho na Lissu anaweza kuwa asiwe yule wasiyemtegemea.


NB. Kumbukaa October ndiyo hii bado siku 24 ufanye mabadiliko na uingize historia nyingine.
The beautiful ones are now born. Let's us support them to grow. Grow Lissu grow.
 
Back
Top Bottom