thesym
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 3,843
- 4,796
Maendeleo ya Japan Yana Sura mbili.👍
Maendeleo yanaletwa na factors nyingi. Hapa tunajadili component ya demokrasia.
Ujue kuwa maendeleo hayana kikomo. Sijasema Japan ilikuwa nyuma km Tz. Bali daada ya WW2 imepata maendeleo makubwa, na pia ikiwa na demokrasia ya hali ya juu.
Sehemu ya Kwanza yalianza kipindi mfalme Meiji ambaye alichukua udhibiti na kuupa ufalme nguvu zaidi kwani kabla shogunate walikuwa na nguvu kuliko mfalme. Baada ya hapo mfalme akafanya mageuzi Japan ikawa nchi ya Kwanza nje ya nchi za maghatibi kuwa na industrial Revolution.
Sehemu ya pili ni kipindi cha miaka 1930s maendeleo unayoyaoana ni matokeo ya sera ya kipindi hicho kwani ni matokeo ya Sera za kipindi ambazo ambapo mawaziri wakuu walikuwa ni authoritarians. Wakati USA walipoikalia Japan baada WWII walianza kufirisi kampuni zilizokuwa karibu na serikali na kubadilisha mfumo WA uendeshaji uchumi unaoendana na nchi za maghatibi na mambo mengine ya kidemokrasia.
Baada ya occupation kuisha serikali ya Japan ikarudia Sera zake za kabla ya Vita huku biashara zikiwa zinapata maelekezo ya MITI (Ministry of International Trade and Industry), kwenye dunia ya kidemokrasia mfanya biashara hapangiwi cha kutengeneza wala kiasi cha kutengeneza kifupi MITI ilikuwa inawatisha wafanyabiashara wanaoenda kinyume na guidance Yao.
Japan Kwa muda mrefu imeongozwa na chama kimoja cha Liberal Democratic Party ambapo viongizi walikuwa ni viongizi kabla ya Vita vyama vyenye mlengo kiujamaa vilishughulikiwa kikamilifu na vingine vikafa na vingine having nguvu tena, hii ni demokrasia?
Kiuhalisia Demokrasia sio factor ya maendeleo Bali ni kitu kinachoambatana baada ya kupata maendeleo.
Haijalishi nchi IPO kwenye muundo upi kama hakuna mipango mizuri na utekelezaji sahihi nchi kamwe haitokuja kuendelea iwe Demokrasia au udikteta