CHADEMA waache kujiita chama cha "Demokrasia na Maendeleo." Demokrasia na maendeleo huwa havikai pamoja

Kwnn ccm ni chama cha siasa ???
Hapana sio chama Cha siasa Ni chama Dola na kimejichimbia kwenye vyombo vyote vya Dola na taasisi zote za umma huko kina mizizi mpaka kwenye trade unions na taasisi za kidini zenye nguvu!
Kwa maana hiyo kinapoteza sifa zote za kuwa chama Cha siasa! Hicho Ni chama Dola(Vanguard Party)!
 
South Korea
South Korea imeanza kupata maendeleo maendeleo ya kiuchumi kipindi cha Raisi Park Chung Hee, ambaye aliingia madarakani baada ya kumpindua raisi aliyechagulia kidemokrasia.

Park alibadilisha katiba na kumfanya yeye kuwa raisi WA Maisha.

Park alikuwa anakamata wafanyabiashara na kuwaweka ndani kisha kuwalazimisha kukubali na matakwa ya serikali kwenye nini cha kufanya.

Mwanzilishi WA Samsung alikimbia nchi Ila baadae alirudi na kukubaliana kile serikali itakochokuwa inaamrisha.

Park alikuwa anawaangamiza wapinzani wake, moja ya mpinzani wake ambaye alitaka kumuua ni raisi WA Korea 1998 Kim Dae Jung, ambaye alimpa upinzani mkubwa kwenye uchaguzi 1971.


Kim alikimbilia Japan na Park akatuma majasusi kumkamata wakati wanakiribia kumuua Kwa kumdumbukiza kwenye maji wanajeshi WA Japan walitokea.

Raisi alipiga marufuku uwepo WA vyama vya wafanyakazi na maandamano.

Korea kusini kipindi hiko ilipiga marufuku wanaume kuwa na nywele ndefu na wanawake kuvaa mini skirt, ulikuwa ukikutwa na "secret polices" basi unanyolewa mbele ya umma.

Hapa wakorea kusini waliokamatwa na polisi wakikatwa nywele na polisi mtaani

Mwisho WA siku park Chung Hee aliuwawa Kwa kupigwa risasi na mlinzi wake WA karibu,

Pamoja na udekteta huo, hiki ni kipinde ambacho Korea kusini ilikuwa inashuhudia mapinfuzi ya viwanda Chini ya maelezo ya serikali kupitia, ndio kipindi ambacho Korea kusini inaipita Korea kaskazini huku makampuni makubwa kama Hyundai, Samsung, LG, POSCO, KIA nk yakaibuka.

Kiuhalisia ni kuwa Korea kusini iliongozwa na madiktekta tangu 1961 mpaka miaka 1994 ambapo uchaguzi WA Kwanza kimeokrasia zaidi ulifanyika, dikteta aliefuata mwingine akaua watu karibu 600 kwenye maandamano yanayojulikana kama Gwangju Democratization Struggle

Lakini pia kipindi hiko Korea ilikuwa bado inachanja mbuga kiuchumi

kifupi Korea kusini huwezi kuiweka kama nchi iliyoendelea Kwa Demokrasia kabisa,

 
South Korea
SK imetawaliwa na majenerali wa kijeshi kuanzia mwaka 1961 hai 1987. Huo ndiyo wakati maendeleo makubwa ya nchi hiyo yalipatikana. Pitiapitia haya mambo ndiyo uje tujadiliane, walau tunapojadiliana uwe unajua mawili matatu.
 
Maendeleo hayana budi yaendane na uhuru ,heshima na utu. Demokrasia inahusika blood!
 
Mbona sehemu kubwa ya Africa hakuna demokrasia tangu nchi zao kupata uhuru na bado ni hakuna maendeleo??
 
Mbona Africa hakuna demokrasia na hakuna maendeleo kwa nusu karne sasa??
 
"Kiuhalisia Demokrasia sio factor ya maendeleo Bali ni kitu kinachoambatana baada ya kupata maendeleo."
 
Mbona kwa muda mrefu nchi za Africa zimekuwa chini ya tawala za kidikteta na hazijaweza kuendelea??
Japana ilikuwa mbali sana kabla hata ya WWII. Na ndiyo maana iliweza kupigana vita ile na mataifa makubwa. Hapo ilikuwa chini ya maliki na si ya kidemokrasia.
 
Sudan ilitawaliwa Jenerali Omar Al Bashir kwa miaka 30.

Uganda imetawaliwa na Jenerali Museveni kwa miaka 30, kwa pamoja na Iddi Amini ni miaka 50 ya utawala wa majenerali.

Nigeria ilitawaliwa na majenerali kwa zaidi ya miaka 40.

DRC imetawaliwa na wanajeshi kwa zaidi ya miaka 50.

Burkinafaso imetawaliwa na mwanajeshi kwa miaka 40.

Zipo Rwanda, Burundi, Mali, Guinea, CAR na nyingine nyingi.

HIZI ZOTE HAZINA MAENDELEO.
SK imetawaliwa na majenerali wa kijeshi kuanzia mwaka 1961 hai 1987. Huo ndiyo wakati maendeleo makubwa ya nchi hiyo yalipatikana. Pitiapitia haya mambo ndiyo uje tujadiliane, walau tunapojadiliana uwe unajua mawili matatu.
 
Sasa ikiwa demokrasia inachelewesha maendeleo mbona Japan haikuchelewa kuendelea licha ya kufuata mfumo wa kidemokrasia,

Lakini pia hujaeleza ni Kwa jinsi Gani hiyo demokrasia inachelewesha hayo maendeleo,

Mfano nchi yetu wakati wa utawala wa chama kimoja zaidi ya Miaka 30 na baada ya kurejea kwenye mfumo wa vyama vingi zaidi ya Miaka 30 sasa, ni kipindi kipi kati ya hivyo viwili ambapo walau tumepigwa hatua kimaendeleo?
 
[emoji106][emoji119]
 
Mbona Africa imekuwa na madikteta wengi sana waliodumu madarakani kwa muda mrefu ila bado imedumaa kimaendeleo?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…