CHADEMA waache kujiita chama cha "Demokrasia na Maendeleo." Demokrasia na maendeleo huwa havikai pamoja

Sikubaliania na mambo mengi ambayo Serikali ya CCP inawafanyia raia wake wote.
China ni party dictatorship.
Mkuu una kubaliana na namna China anavyo watendea Uyghurs na Tibetians ?
 
Sikubaliania na mambo mengi ambayo Serikali ya CCP inawafanyia raia wake wote.
China ni party dictatorship.
Ina utofauti gani na Germany, France na Canada wakati wa ukuaji wake ?
 
Naona maana ya demokrasia kati yangu na yako iko tofauti
Na kuhusu Prussia na religion persecutions ili lipo wazi
Saxon Lutheran immigration of 1838–39 - Wikipedia.

Point yangu msingi na nairudia tena Demokrasia sio factor ya nchi kuendelea kiuchumi kama unavyojaribu kuonyesha bali mipango mizuri, consistency, utekelezaji ulio sahihi wa hio mipango.

Maana naona hii reply inatoka nje ya kile nilichokuwa nazungumzia Democracy & Economic Development
 
Kwanza unamaanisha nini unaposema ukuaji?
Economic growth, Economic development au state formation and development?

Swali lako litakuwa na mashiko endapo nitaelewa ni ukuaji upi unaouzungumzia.
Pamoja na hayo fahamu kwamba China imekuwa Empire kubwa na great civilization kwa karne nyingi wakati Ulaya wakiwa bado barbarians wanaopigana vita kutwa na kuchoma wachawi moto.
Ina utofauti gani na Germany, France na Canada wakati wa ukuaji wake ?
 
Je Udikteta ni factor ya nchi kuendelea kiuchumi?
 
Economic development.
 
Je Udikteta ni factor ya nchi kuendelea kiuchumi?
Hapana, na posti yangu #66 nimefafanua.
 
Tusichoshane mkuu. Maana hata hiyo Ghana unayoizungumzia haina democrasia kwa zaidi ya miaka 20. Hadi 2000 mwanzoni ipo chini ya madikteta. Na pia usifananishe economic depression kama hizo na yanayotokea Ghana au yaliyotokea juzi Sri Lanka. Na hizo nchi zenye resources kibao na watu wachache kama mkoa, kama iliyo Botswana si mfano mzuri. Udogo ninaosema ni udogo wa idadi ya watu ukifananisha na resources. Rwanda na Burundi zenye watu milioni kumi naa kila moja si nchi ndogo.

Pia wala hujajibu kwa nini nchi za Afrika kaskazini ambazo ndizo zimeendelea zaidi katika Afrika ni kama hakuna kabisa demokrasia kwa miaka yao yote zimekuwa huru, mpaka kidogo wakati wa arab spring. Unachagua tu points za kuadress. South Afrika ambayo imekuwa ya kidemokrasia zaidi inaenda shimoni.
 
Equatorial Guinea ina watu milioni 1.6, ni mojawapo ya mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Africa na bado ni Maskini, Togo ina watu milioni 8 ina rasilimali za kila aina ila bado ni Maskini, Mauritania ina watu milioni 5 ila, ni kubwa kama Tanzania, ina rasilimali za kila aina ila ni Maskini.

Ghana imechukua muelekeo wa Demokrasia tangu 1992, mafanikio makubwa iliyopata Ghana katika uchumi, maendeleo na stability ni wakati ilipoelekea katika mkondo wa demokrasia.

Mauritius na Seychelles ndio nchi zilizoendelea zaidi barani Africa, sio hizo nchi za Kaskazini. Pia Namibia na Botswana zinazizid hizo nchi za Africa Kaskazini kwa maendeleo na maendeleo jumuishi huku zikiwa na demokrasia pana kwa raia wake.
 
Hujui unachozungumzia, Karne ya 15 ndo kwanza Wafaransa na Waingereza walikuwa wanafika Amerika Kaskazini na wanapigana na Wahindi kwenye ardhi yao.
Hakukuwa na Taifa au hata koloni la Canada.
Karne ya 15
 
Hujui unachozungumzia, Karne ya 15 ndo kwanza Wafaransa na Waingereza walikuwa wanafika Amerika Kaskazini na wanapigana na Wahindi kwenye ardhi yao.
Hakukuwa na Taifa au hata koloni la Canada.
France imeanza ku control trade routes karne ipi ?
 
Hujui unachozungumzia, Karne ya 15 ndo kwanza Wafaransa na Waingereza walikuwa wanafika Amerika Kaskazini na wanapigana na Wahindi kwenye ardhi yao.
Hakukuwa na Taifa au hata koloni la Canada.
Ukiambiwa taifa la Canada una elewa nini ?
 
Hiyo Shelisheli unayoishabikia imeongozwa na madikteta walioingia kwa mapinduzi hadi mwaka 2016, toka miaka ya 1970s. Na nchi hizi ambazo zinaonekana na per capita kubwa kama Mauritius, Botswana, Namibia nk zina watu wachache ana. watu 8m wa Togo siyo wachache, Mauritania ni jangwa tupu. Hata equatorial Guinea inaonekana kufanya vizuri licha ya kuongozwa na kichaa. Idadi ya watu inamatter unapofanya vipimo hivi. Ndiyo maana hata HDI ya Zanzibar ni kubwa hapa EA.
Demokrasia si kigezo cha kupata maendeleo, tena imeonekana kuwa demokrasia inarudisha nyuma maendeleo. Maendeleo hayawezi kupatikana chini ya demokrasia. Udikteta si kigezo cha kupata maendeleo, lakini maendeleo yanaweza kupatikana na yameonekana yakipatikana chini ya udikteta, kama yalivyopatikana huko Shelisheli. Demokraia ni zao la maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…