CHADEMA wasitafute mchawi 2025 watakapopata kura moja

CHADEMA wasitafute mchawi 2025 watakapopata kura moja

Jambo moja unatakiwa kulijua ni kuwa,

Mbowe anapokaa kimya Huwa ni hatari ktk kupanga mikakati kuliko hata anapokuwa jukwaani.

Uchaguzi Leo hii ukifanyika Kwa HAKI, CDM wanapaita 70% ya wabunge wote.
Duuh!!! me najua ameelemewa na buyu la asali..
Hao wabunge anaweza kuwapata lakini sio kwa juhudi zake ila uzembe wa awamu iliyopo
 
Vyama hukosea pia,

Hata CCM wapo wanaoamini yule wa msoga hakufaa kupewa kiti ukilinganisha na Dr Salim Ahmad Salim.
Minajua walilamba asali, mtu jana alikuwa na kadi ya ccm kesho mnampitisha kuwa mgombea
wakati huo mlikuwa mnamuita fisadi hiyo sio mistake ni decision
 
Hiyo lugha ya "kulamba asali" ni ya maudhi sana. Ukiulizwa utueleze hiyo asali inalambwaje unaweza kueleza? Wewe mwenyewe uko nyuma ya keyboard huku ukitumia fake ID, halafu uko frontline kubeza watu wanaojitolea muda, rasilimali na uhai wao kurekebisha mambo. Afadhali wao wamefikia hapo, wewe mchango wako ni upi? Si ujitokeze unyooshe yaliyoshindikana ili tukuone kidume?
Katika akili yako timamu unahisi Mbowe kajitolea kwa ajili yako na sio maslahi yake? 🤣

Hesabu za CCM ni kuwajaza noti wapinzani na kuacha wafanye biashara zao kwa uhuru ili ikifika wakati wa uchaguzi mzugwe zugwe waanze kulia unafiki kuwa wameibiwa kura wapelekane korokoroni kimchongo baada ya muda maisha yanaendelea.
 
Minajua walilamba asali, mtu jana alikuwa na kadi ya ccm kesho mnampitisha kuwa mgombea
wakati huo mlikuwa mnamuita fisadi hiyo sio mistake ni decision
Nimekwambia Mbowe Hana Bei,

Wangekuwa wamenunuliwa wangemkabidhi uenyekiti wa chama.

Ile ilikuwa POLITICAL miscalculation
 
Nimekwambia Mbowe Hana Bei,

Wangekuwa wamenunuliwa wangemkabidhi uenyekiti wa chama.

Ile ilikuwa POLITICAL miscalculation
Kweli hana bei ila historia inatuambia tofauti pale alipomkabidhi ugombea uraisi mtu
aliyemuimba ni fisadi kwa miaka zaidi ya kumi
 
Leo naona wanashangilia kama mazuzu, hawana tofauti na mtoto aliyechapwa akaanza kulia akapewa pipi akanyamaza akiulizwa nani amekuchapa anamnyooshea kidole mtu aliyekuwa anambembeleza kipindi analia kabla ya kupewa pipi.

DJ hana chakupoteza keshalamba asali toka siku ya kwanza anatoka Lupango hana tena stori za katiba mpya, anasubiri tena maridhiano 2028.

Usiidharau CHADEMA. Wamefanikiwa kwenye ajenda zao. Misimamo yao ndio imekuwa chachu ya mabadiliko ya leo.
 
Nimekwambia Mbowe Hana Bei,

Wangekuwa wamenunuliwa wangemkabidhi uenyekiti wa chama.

Ile ilikuwa POLITICAL miscalculation
Kwa mujibu wako hayo unayosema. Unafikiri ni rahisi kumnyamazisha mtu mzima uliyempa kesi ya ugaidi kwa fitina tu.
 
Hapana mimi sio sadist ila siwezi kutema big G kwa karanga za kuonjeshwa

Hukutegemea CHADEMA kufanikiwa kupata point tatu muhimu. Mikutano na Mchakato wa Katiba mpya. Halafu happy Bado wapo kwenye mazungumzo Bado hayajaisha. So tutulie kwanza.
 
Kwa mujibu wako hayo unayosema. Unafikiri ni rahisi kumnyamazisha mtu mzima uliyempa kesi ya ugaidi kwa fitina tu.
Hellow STUKA bas!!

Mbowe alitaka kesi iendelee,

Alikuwa radhi hata kufia gerezani,

Sirikali kupitia DPP ndo waliingia mitini.

Walipomshindwa, hapakuwa na namna zaidi ya kutii matakwa yake😠😠
 
CCM waliporuhusu vyama vingi 1992 wakati ambao 80% ya wananchi walikuwa wamevikataa,

Unaamini pia NYERERE na CCM walikuwa wamehongwa?
waliokataa ni wana ccm wenyewe na waliokubali ni wao wale wale hakuna mwananchi alipiga kura ya maoni.
pressure ya mabeberu kupewa misaada
 
Katika akili yako timamu unahisi Mbowe kajitolea kwa ajili yako na sio maslahi yake? 🤣

Hesabu za CCM ni kuwajaza noti wapinzani na kuacha wafanye biashara zao kwa uhuru ili ikifika wakati wa uchaguzi mzugwe zugwe waanze kulia unafiki kuwa wameibiwa kura wapelekane korokoroni kimchongo baada ya muda maisha yanaendelea.
Childish argument.
 
Hellow STUKA bas!!

Mbowe alitaka kesi iendelee,

Alikuwa radhi hata kufia gerezani,

Sirikali kupitia DPP ndo waliingia mitini.

Walipomshindwa, hapakuwa na namna zaidi ya kutii matakwa yake😠😠
Mbowe alikutwa na kesi ya kujibu Dj akaona anunue uhuru wake huku akilamba na asali
 
Punguza unafiki, mnaona aibu CHADEMA kupata pointing tatu muhimu, Mikutano, katiba na marekebisho ya sheria. Mmebaki na hearsay za mfa maji.
Continue to fall for mind games🤣
 
Back
Top Bottom