CHADEMA ya LISSU na HECHE ijizuie Mikutano yake kuwa mikutano ya kutangaza Injili

Mmemaliza kusema CDM ni ya Wachagga sasa Mbowe ameondoka sasa mnataka muanze CDM ni ya Wakristo.
 
CDM hawafanyi bidii zozote za kujisafisha dhidi ya tuhuma za udini. Wazembe sana.
 
Una hoja nzuri sana. Hata mimi huwa sipendi sana viongozi wa dini kuonekana majukwaani hata tu kufanya wanachodai ni ''kuombea mkutano''. Hili suala ni CCM wanalitumia kama njia ya kuwaghilibu raia hivyo Chadema wajiepushe. Sikatai viongozi wa dini kukemea maovu lakini wafanye hivyo sehemu neutral. Vinginevyo, kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo basi washirikishe pia waislam au wakifika sehemu zenye waislam wengi basi wapandishe viongozi wa kiislam.
 
CDM hawafanyi bidii zozote za kujisafisha dhidi ya tuhuma za udini. Wazembe sana.
Wafanye juhudi gani wakati siyo wadini? I mean wewe ukituhumiwa ni mwizi, utafanya juhudi kujisafisha wakati wewe siyo mwizi? Chadema ilituhumiwa kuwa ni chama cha wachaga na wakawa wanawaita Chagadema, sasa hivi wamekosa cha kusema na wameingia kwenye udini. Japo hata mimi sikubali hili jambo la kusimamisha viongozi wa dini kwenye mikutano lakini kuna mambo mengine inabidi upuuze tu.
 
Mimi naamini kabisa CDM na viongozi wake hawana wala hawafikirii swala la udini, lakini sura ya chama chao inasema tofauti kabisa. Hivyo wanapaswa kufanya bidii kufuta hiyo sura. Hawajawahi simamisha Mgombea Urais Muislamu, wala kuwa na kiongozi mkubwa Muislamu, ni chama kikubwa lakini ni dhaifu maeneo yenye waislamu wengi nk nk. Bidii inahitajika kukipa sura ya watu wa dini zote.
 
Point
 
Unajua kuwa Chadema imewahi kuwa na mwenyekiti muislam na ni marehemu sasa? Ushamsikia Bob Makani? BTW n´mimi hili la kuhesabu viongozi kwa kuangalia dini huwa linanikwaza sana. Mimi ni mkristo lakini nipo tayari kuongozwa na rais, makamu na baraza la mawaziri, wote waislam ili mradi wawe viongozi bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…