CHADEMA yafungua rasmi pazia la mbio za Urais. Wanaotaka kuomba ridhaa hiyo waruhusiwa

CHADEMA yafungua rasmi pazia la mbio za Urais. Wanaotaka kuomba ridhaa hiyo waruhusiwa

Katibu Mkuu wa CHADEMA , John Mnyika atatoa tamko muhimu la Chama kwa umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari, leo Jumatano, Juni 3, 2020.

Je, Atamjibu Msajili wa vyama kuhusu vyama kupeleka ratiba za kampeni ilhali mikutano bado imezuiliwa na haijulikani lini itaruhusiwa.

Je, Ataijibu NEC Taifa kuja na kanuni zake mfukoni, mjawapo ikiwa mawakala kutopewa nakala ya matokeo.

STAY TUNED.

=====

"Bado kuna mwanya katika muda huu wa Bunge uliobakia, upelekwe muswada Bungeni ambao utafanya tupate Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kuhakikisha tunaitoa Ccm madarakani" Katibu Mkuu wa CHADEMA

"Tunatawaka watia nia wa CHADEMA kusoma miongozo vizuri, kuna muongozo mahsusi kabisa toka 2012, wazingatie muongozo katika hatua mbalimbali, wakikiuka Chama hakitasita kuwachukulia hatua,ili kuhakikisha tunapata viongozi walio bora katika Taifa" Katibu Mkuu Nyika.

"CHADEMA kimefungua milango 2 muhimu, kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mlango wa 1; ambao tunaufungua leo ni wa kuruhusu watia nia wa Urais kupitia Chadema na mlango wa 2; ni mlango wa majadiliano na vyama vyenye dhamira ya kweli ya kushirikiana kuitoa Ccm madarakani" Mnyika.

"Tulitaka Tume Huru ya Uchaguzi ili kuwe na uchaguzi huru na wa haki, bado tunasisitiza kwa watawala tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi, ila tumejiandaa kwa njia nyingine kuhakikisha Ccm wanatoka madarakani, katika wakati muafaka tutawaongoza wananchi kudai haki" Mnyika.

Miongoni mwa wanasiasa wachache kwenye akili kubwa ni JJ mnyika amenifanya niipende siasa
 
Kweli kabisa mnachukua nchi mwaka huu na kwa Sasa rais Magufuli anawajengea bonge la ikulu chamwino keshamwekea rais Mbowe wanyama, ndege tausi nk. Hongrezi chadema kwa kushinda urais 2020-2025.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafikiri ikulu ni ya Magufuli, hata anayoishi ilijengwa na Wajerumani.
 
That's that, lazima mjiandae kwa njia nyingine, sio kususa, siasa itakuwa imewashinda.
 
Ndo huo umoja uliwapa kura nyingi na wabunge wengi chadema,kwa kupata kura za CUF,NCCR,NLD na kura za wanachama wa CCM waliokua na mahaba na Edlow.

Kwa sasa never.hakuna tena mbeleko.

Kwa taarifa yako bila hata huo umoja bado cdm ingepata kura nyingi. Hata sasa tume ikifanya inachopaswa kufanya uje ulete mrejesho.
 
Tuna kusubiri kwa hamu mhe. J J mnyika katibu makini unayetokana na chama makini..kwa jinsi ccm wanavyo muota mnyika kuhamia ccm...cku akihamia watampa urais wa nchi kbs...[emoji1787][emoji1787]
hapana Ila anaweza akawa waziri wa nchi tawala za mikoa na serikal za mitaa TAMISEMI.

Kati ya majembe yaliyobaki kule chadomo abayo ccm inayatamani ni mnyika tu basi.
 
Sawa!!! Kama Kuna wakati Mgumu Tena kwa CDM ni Sasa,Kama karata mlivyo zichanga wakati wa uchuguzi wa viongozi wa chama pale Mlimano City ndivyo mnahitajika kicheza kwa mfumo ule ule,mkumbuke one mistake one goal

Mlango wapili ni sawa Umoja ni Nguvu lakini umoja nanani??hapa ndipo. Umakini inahitajika UKAWA ile ya 2015 Sasa haipo Tena,Utafungamana na ACT?? Huku tayari kisharamba ahadi ya Zanzibar???mbali na Happ tayari kuna BM anapewa kipaumbele jawabu ni ngumu kuhandle hii game.

Utaungana na NCCR-Mageuzi huyu Kisha pata ndoto ya Majimbo,unadhani atafungamana na ukweli??? Haya Unahitaji kufungamana na CUF ya Lipumba huku inafahamika Nguvu ya awali Sasa haipo Tena CUF maana assert ya Zanzibar ni Maalimu seif Sasa Yuko ACT,haya mlango wa pili una ufungua kwa Nani???

Siyo mbaya Tanzania tunazaidi ya vyama 20 vya siasa,Ukiondoa Chadema yenyewe nichama gani Tena chenye nguvu tofauti nanilivyo vitaja Happ juu??? Ikumbukwe dhana ya Umoja ni kuongeza Nguvu na Ushawishi kwa watu.Je Chauma,UDP,na NLD kwa mzee wangu Lungwe vinao Ushawishi kwa Sasa???

Mwisho nafikiri kila mtu ashinde mechi zake,Mlango wa pili muutizame vyema
 
Kwa taarifa yako bila hata huo umoja bado cdm ingepata kura nyingi. Hata sasa tume ikifanya inachopaswa kufanya uje ulete mrejesho.
Thubutu,ni upepo wa Edlow,Maalim,Juma Duni,Mzee kingunge,Mbatia na Sumaye.Kwa sasa hao wote wamesepa kabaki mpiga hela mbowe na shoga zake waropokaji akina Mdee
 
Thubutu,ni upepo wa Edlow,Maalim,Juma Duni,Mzee kingunge,Mbatia na Sumaye.Kwa sasa hao wote wamesepa kabaki mpiga hela mbowe na shoga zake waropokaji akina Mdee

Kama hao ndio walileta hizo kura wakiwa na miezi miwili ndani ya cdm, je walileta kura na kufungua matawi mangapi ya cdm zaidi ya miaka miwili waliyokaa? Hivi mnadhani hatujui kura za cdm zilitokana na juhudi gani?
 
Kuna wanachama na wafuasi wa chama.
Kuna mtu anakibeba chama,yani wafuasi wanamfata mtu na sio chama.
kura za lowasa(sio za Chadema)ni milioni 6.wakati wanachama wa chadema hawafiki hata laki 3,mpo wachache sana nyinyi nyumbu.

Hata Mbowe wakati anatoa hotuba ya(kubadili gia angani) kumkaribisha Edlow alizungumzia mtaji wa wafuasi watakao mfuata Edlow CDM.
 
Ili ujue ww ni bendera fuata upepo na huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, Lowassa mwenyewe alisema atakuja na wabunge hamsini wa ccm, taja majina ya hao wabunge 50 aliokwenda nao cdm. Narudia tena, kama Lowassa alikuja na kura 6m akiwa na miezi miwili ndani ya cdm, alileta kura au kufungua matawi mangapi, zaidi ya miaka miwili aliyokaa cdm? Mbona chaguzi za marudio zilikuwa zinaporwa wazi wazi, na yeye akiwa cdm asiagize hao watu milioni 6 wafanye jitihada zozote?
 
CDM inatakiwa iwe makini sana ktk zoezi la kumtafuta mpeperusha bendera. Iwachunguze kwa kina watia nia wake wote, kwa kuwa itakuwa ni fedheha aibu kubwa ya mwaka endapo itatokea atawasalti na hatimaye akaunga mkono juhudi waelekeapo kwenye siku za kampeni za uchaguzi.
 
Ili ujue ww ni bendera fuata upepo na huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, Lowassa mwenyewe alisema atakuja na wabunge hamsini wa ccm, taja majina ya hao wabunge 50 aliokwenda nao cdm. Narudia tena, kama Lowassa alikuja na kura 6m akiwa na miezi miwili ndani ya cdm, alileta kura au kufungua matawi mangapi, zaidi ya miaka miwili aliyokaa cdm? Mbona chaguzi za marudio zilikuwa zinaporwa wazi wazi, na yeye akiwa cdm asiagize hao watu milioni 6 wafanye jitihada zozote?
Lowasa hakuja kufungua matawi wala kujenga chama.
Lowasa alifata urais.Aliahidi alipokiwa CCM asipopitia mlangoni basi atapitia dirishani lakini lazima aingie ikulu.
Mwaka huu mkipata kura hata milioni moja naacha kuwatafuna.
 
Ni kweli hata hizo kura milioni moja mbona ni nyingi sana. Kwa huo uchaguzi wa kutaka kumfurahisha Magufuli, hata kura 20 zitakuwa ni maajabu.
 
Back
Top Bottom