CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Sasa ulitaka wafanye nini wakati wagombea wao wameenguliwa kwa hila ?

Achana na huyo jamaa, anataka cdm washiriki ili nchi na dunia iamini bado kuna demokrasia. Kimsingi anataka cdm washiriki ili kuficha huu upuuzi unaoendelea. Hiyo cdm anayotaka ishiriki itasongaje mbele bila kushinda uchaguzi? Bado cdm ina mtaji wa watu, wasihofie lolote hata kama hawatapata viongozi sasa kwa njia ya hila, lakini wananchi sasa wana ufahamu wa kutosha na hizi siasa za kishenzi wanaziona.
 
Kuna Waziri mmoja anaitwa "JAFO", bila aibu wala kupepesa macho leo anasema eti kususia uchaguzi ni kuwanyima raia haki yao.

Hivi inaingia akilini kweli "CCM" wamejipitisha nchi nzima bila kupingwa, wamewakata wagombea wa upinzani wote, na kama mgombea akipitishwa bila kupingwa maana yake hakutakua na uchaguzi wowote wa mitaa.

Swali kwa Jafo,

Hao wapinzani wanawanyima haki gani raia??? Au ni serikali kwa mabavu ndio wamewanyima haki raia ya kuchagua wagombea wanaowafaa na kuwachagulia viongozi kwa nguvu???

Wasifanye watanzania wapumbavu. Ama kweli tanzania hatuna mawaziri wala serikali. Aibu hii dunia nzima.

#CCM subirini wananchi wenye hasira kali #2020.
 
OK good-luck kama unadhani ni jambo ambalo impact zake ni chanya.

Nikuhakikishie pamoja na kelele zote mabeberu nyuma ya pazia pia ni 80% supporters wa Magu mengi anayofanya ndio yale wanayotaka (ukitoa ukandamizaji wa demokrasia, JK alikuwa anachezea financial sanctions kushinda Magufuli; hiyo ni message tosha kama una akili timamu) na 20% iliyobaki ndio kama sehemu ya pressure tu.

Mtabaki hapo hapo kama sio kurudi kwa stahili ya “hewala sio utumwa”

Hata nikikuuliza mafanikio ya kisiasa CDM itakayopata kwa uamuzi huu na tunayapimaje huko mbele I doubt kama unaweza kujibu.
Hiyo 80% umeipataje?
 
Sasa ulitaka wafanye nini wakati wagombea wao wameenguliwa kwa hila ?
Ingia mahakamani, pambana kutoa elimu kwenye jamii ya nini kinaendelea; etc with building your political mileage.

An A’level political book covers methods of political pressure and ways of mobilising support; let alone political books which are best sellers.

You don’t exert pressure in politics if you can’t win public support first, kwa jamii ya watanzania ambayo wengi ni wasiojali sana na si wapiga kura kususa is not an effective strategist, changamoto walizo nazo ni kukaa chini na kujua wanakuja kivipi.

It’s complicated requiring winning psychological battle, good lawyers, social pressure tactic, designed media messages etc with fitna za politics. CDM wana political strategist ndio wenye hilo jukumu la ku formulate how best to take the battle ahead.

Hila kususa na kutegemea mabeberu chini ya Tanzania ya Magu it won’t work
 
Waswahili husema kufa kufaana baada ya chama kikuu cha upinzani nchini kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimetoa fursa kwa chama cha ACT wazalendo kuimarika zaidi.

Maana yake ni kwamba kwa sasa Chadema itakosa uwakilishi katika serikali za mitaa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wake.

Nina imani Zitto na maalimu Seif hawatasusia uchaguzi ila watapanga mbinu muafaka za kumkabili mwenzao waziri Jafo kwenye uwanja wa uchaguzi kwani waswahili wanasema.......Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.

Poleni sana Chadema

Maendeleo hayana vyama!
Ningependa nikukumbushe kwa kukuuliza. Unafahamu kuna chama kinaitwa ADC (Allience for Democratic Change)? Je, unakumbuka kuwa chama hicho kilishirikinuchaguzi wa SMZ 2015 ambao ulisusiwa na CUF? Je chama hicho kimeimarika kupitia kushiriki uchaguzi huo?
 
Anajifanya hakijui hiko chama kilichojitoa...............Jinga kabisa.
 
Na iwe hivyo,viva kamanda mbowe.
Natarajia na vyam makini vote vya upinzani vitafuata nyayo zako.
Kabwe wa Act na Mbatia wa NCCR hayaaaaaa fuata mkondo.
 
Hicho anachokiongea Jafo kinatoka moyoni au machozi ya mamba?

Anahadaa umma ili ionekane wana nia njema, ukweli ni kuwa Jafo anajua kila kinachoendelea na lengo lake ni kuhadaa dunia kuwa kuna demokrasia. Lengo hasa ni ccm watangazwe washindi kwa 90%, ila hiyo 90% itapatikana kwa figisu, sasa cdm wakijitoa uchaguzi mzima unatoa taswira mbaya kwa dunia. Hivyo Jafo hawataki cdm kwa ajili ya ushindani, bali kwa ajili ya hadaa kwa nchi na dunia. Kuna vyama kibao wanaweza kushiriki huo upuuzi wa kuwasindikiza ccm kuhalalisha ushindi wao wa dhuluma.
 
Huyu Jaf ni mzima? Yale wanayofanya watendaji ndiyo yanawapa wananchi haki? Hopeless kabisa. There is a day coming when they will be held accountable.
 
Huyu Jafo soon ntaanza kumdharau
Ina maana mpaka sasa hujamdharau tu? Wengine tulikwishamwona wa hovyo pale aliporuhusu hayo mambo ya kipumbavu yanayofanywa na watendaji kuendelea.

Ni wendawazimu kuacha uhuni uendelee halafu unasema unasubiria rufaa.
 
Back
Top Bottom