CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Pia tujiulize CCM ile ya Mwl Nerere na Wenyeviti waliofuata baada yake, ilistahili kuwa na Mwenyekiti tuliyenae sasa?
 
Iko hivi. Hawa jamaa baada ya kuona kasi ya JPM kwenye maendeleo ya nchi na watu wake haikamatiki basi wao wakaja na mkakati wa values za kiliberali ambazo hakika kwa nchi yetu sio kipaumbele kama kuboresha na kuendeleza hali ya kiuchumi na kijamii ya watu.

Wanajidai wanapigania uhuru wa kutoa maoni na kujieleza wakati ni kisingizio waweze kufanya uchochezi dhidi ya serikali wanapinga wazi sera za ujenzi wa nchi za kupambana na unyonyaji wa ndani na nje kwa kufadhiliwa na hao mabeberu. Bahati nzuri wananchi wameliona hilo wanaunga mkono kwa asilimia kubwa na CHADEMA ila kufanya usanii jinsi ia mitini bila kuabika kwenye uchaguzi
Mwehu
 
Daah Lumumba mnafeli wapi?
Mimi sio CHADEMA wala ACT.. ila ningependa haki na uhuru wa uchaguzi ili kujipima kama kweli tunakubalika au tunalazimisha. kama mtu hakupendi hata ukilazimisha kupendwa bado hupendwi!! kupendwa ni ushawishi na sio nguvu. ushawishi uko kwenye kampeni.......................
 
Pamoja na figusu lakini CDM walikosa maandalizi ya huu uchaguzi mdogo...

Kama kususa Ni vizuri Ni heri wakafute usajiri wa chama kuliko kupoteza muda na siasa chafu...

Wananchi watajitetea wenyewe pasipo vyama vya siasa..
 
Mimi sio CHADEMA wala ACT.. ila ningependa haki na uhuru wa uchaguzi ili kujipima kama kweli tunakubalika au tunalazimisha. kama mtu hakupendi hata ukilazimisha kupendwa bado hupendwi!! kupendwa ni ushawishi na sio nguvu. ushawishi uko kwenye kampeni.......................
 
Nashauri Chadema baada ya tamko hili idara ya mawasiliano na habari waandae clip ya video ikiwabna vielelezo kuweka records sawa. Ili hawa wenye dhamana wawajibishwe siku moja.
 
Wewe ni kifafa
Mbowe wewe ni kiongozi wa chama cha siasa.
Lengo kuu la chama chochote ni kushika dola.

Unatakiwa kutambua kususia uchaguzi maana yake ni kuwadhulumu wananchi.
Sio kila mtaa majina yamekatwa, sasa madudu mliyofanya huko kwenu Hai unataka tuumie na tusiousika.

Hiki chama sio cha viongozi, maana ya maamuzi yenu ni kuua chama, serikali inaanzia mtaani, kama mnaona hamtendewi haki mbona ubunge mnaendelea?

Mbowe ni jipu litumbuliwe.
 
Namna pekee ya ccm kushinda ni ya kufanya uharamia kama huu
 
Viongozi wenu wanasema wawasusie viongozi watakaochaguliwa. Mi nakubali. Lakini viongozi hao walifikiria kabla ya kutoa tamko?
Hawaaminiki Hawa. Walisema hawamtambui Magufuli, hatuoni muendelezo. Bungeni ndio kila siku wanatoka nje Ila hatuoni matokeo chanya.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.

“Nimesikia kuwa Chama kimojawapo kimejitoa kwenye Uchaguzi, ninachoweza kusema ni kuwa hawajawatendea haki Wananchi wa chini kwa sababu baadhi yao walishateuliwa na wengine wameshawasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Rufaa na tayari baadhi ya Kamati za Rufaa zimeshaanza kutoa maamuzi juu ya rufaa hizo.

Mtazamo wangu maamuzi hayo yatawanyima haki na kuwadhulumu wananchi wa chini haki yao ya kugombea na kuongoza Serikali za Mitaa ambao baadhi yao wameshateuliwa na wengine wanasubrii rufaa zao”

Mhe. Seleman S. Jafo
Waziiri wa Nchi OR-TAMISEMI
07/11/2019



Pia soma
A right and just decision. It's only fools can support what is going on.We are being led by a bunch of crooks camouflaging in "politicians" costume!
 
J.Haule,on twitter.
74307216_2640425889349396_9170381318767247360_o.jpg
74605525_2410768639162850_3340225624064131072_n.jpg
 
Wapinzani wa nchi wananichekesha Sana baada ya kuona watashindwa uchaguzi wakaona Bora waokoe gharama. Sasa hivi mmekuwa vyama vya hovyo hamna vision wala mwelekeo hamna msimamo kabisa. Njia pekee ya kushindana na Magufuli ni kwenye kuleta maendeleo kuliko kuleta propaganda kwa bahati mbaya most of them mmeshindwa kufanya vizuri kwenye majimbo yenu.
 
Mzunguko mrefu akili kubwa ya mbowe imefanikiwa tatizo ni pesa chama hakina pesa jamani kikitangaza hakuna pesa kitazua ya kuzua na kuanzisha tafrani ni bora hii akili iliyotumiwa..

Najua hili unalijua ila umeamua tu kukifurahisha.
Waliopanda na mbunge mmoja, madiwani wachache hela walikuwa nayo?. Kiwango walichofikia walikopa kwako?.
Siku za mwizi ni 40. Tumieni mbinu zote ipo siku 40 yenu itafika.
Mnahitaji ushindi wa kishindo, mmeachiwa mpate wa Tsunami bado mnaleta maneno mhofumbofu. Shangilieni ushindi wenu.
 
Wapinzani wa nchi wananichekesha Sana baada ya kuona watashindwa uchaguzi wakaona Bora waokoe gharama. Sasa hivi mmekuwa vyama vya hovyo hamna vision wala mwelekeo hamna msimamo kabisa. Njia pekee ya kushindana na Magufuli ni kwenye kuleta maendeleo kuliko kuleta propaganda kwa bahati mbaya most of them mmeshindwa kufanya vizuri kwenye majimbo yenu.

Ndugu yangu democracy its more than political parties.
Ni hatari sana kwa serikali kufanya michezo hiyo wanayoifanya.

Ni vema sana mambo yahusuyo taifa hasa democracy yakaachwa watu wayaenjoy.
Ila wanachokipanda ni hatari mno kuliko hata faida ya ndege na miundombinu inayoendelea.
Time will tell mkuu
 
Hao walishaambiwa wanawashwa washwa wameamua kujikalia pembeni tu.

Hawapaswi kunyamaza
Waende beyond hata kuwa na vikao vya kumpika

Ukifika zimbabwe miundombinu ni mizuri sana lakini mwisho wake mmeuona wote.

Tukubali kwamba still tunatawaliwa as africa bado hatujawa tangible kujitawala kwa mambo mengi
Sasa tusifike huko tukarudishwa nyuma
 
Back
Top Bottom