CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

"Nina taarifa kuna chama kimejitoa, ni imani yangu chama hicho kinaweza kuwa na mipango ya kuvuruga amani ya nchi hii, nitoe onyo hakutakuwa na nafasi ya chama cha siasa kuratibu kuvuruga amani, Serikali tumejipanga kutumia nguvu hakuna amani inavurugwa"- Waziri Kangi Lugola
Hapahitajiki vurugu kuleta mageuzi Tanzania.
Wananchi watakapokataa kuwa 'mifugo' wataleta mageuzi bila ya vurugu yoyote.
 
"Nina taarifa kuna chama kimejitoa, ni imani yangu chama hicho kinaweza kuwa na mipango ya kuvuruga amani ya nchi hii, nitoe onyo hakutakuwa na nafasi ya chama cha siasa kuratibu kuvuruga amani, Serikali tumejipanga kutumia nguvu hakuna amani inavurugwa"- Waziri Kangi Lugola
Stupid kangi, ikianza civil war utaweka pua zako mbele? Utasakizia watoto wa wenzako wafe wa kwako unakimbizia nje au kijijini kwako!
 
Haya maamuzi sahihi ila yamechelewa sana,sijui hata mlipopanga kushiriki mlikuwa mnafikiria nini.

Huwezi kufanya siasa na mtu asiyetayari kushindwa.
We jamaa umenena point sana
 
Cuf walisusia uchaguzi mkuu Zanzibar na maisha yanamesonga wazee
Huo ni mfano ambao CHADEMA na vyama vingine wanapaswa kuutumia na kuepuka kufanya makosa kama hayo.

Watu hawawezi kuacha kutafuta njia zingine za kuondokana na ukandamizaji kwa sababu tu CUF walishindwa.
 
Hizi post za kitaifa ilitakiwa ku " Like " tuu wala sio kucoment. Unakoment nini sasa ujumbe Murua kama huu.
 
Kuna jamaa emeniambia waache kulalamika Misitu si ipo?Sijamuelewa.
Misitu tena? Sio jambo la afya watanzania kufikia mawazo hayo. Hali itendeke Taifa lisipasuke kwa ajili ya madaraka wakati tukifa unarudi ulikotoka mtupu,mengine unayaacha yooote duniani.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.

“Nimesikia kuwa Chama kimojawapo kimejitoa kwenye Uchaguzi, ninachoweza kusema ni kuwa hawajawatendea haki Wananchi wa chini kwa sababu baadhi yao walishateuliwa na wengine wameshawasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Rufaa na tayari baadhi ya Kamati za Rufaa zimeshaanza kutoa maamuzi juu ya rufaa hizo.

Mtazamo wangu maamuzi hayo yatawanyima haki na kuwadhulumu wananchi wa chini haki yao ya kugombea na kuongoza Serikali za Mitaa ambao baadhi yao wameshateuliwa na wengine wanasubrii rufaa zao”

Mhe. Seleman S. Jafo
Waziiri wa Nchi OR-TAMISEMI
07/11/2019



Pia soma
Kujitoa kwao ni kuonyesha uhdaifu wa kushindwa
 
jibu ni wale wote waliotaka kukitumia chama kama jahazi la kuwavusha 2020 na kutwaa ubingwa ambao kiukweli sio wao. kila siku tunasema Chadema ina wenyewe, na wenyewe wameshasoma alama za nyakati kama kuna watu wanataka kukiondoa chama nje ya dhumuni lake la kuanzisha na kukimbia nacho kusikojulikana.

Tunacho kiona sasa, ni chama kujiweka kwenye "sleeping mode", kujirudisha nyuma na kujikosesha nguvu kwa makusudi ili kisiwe kivutio kwa wale wanotala kukitumia kwa manufaa yao. Wimbi la bahari likishapita, basi ni rahisi kujiamsha na kuanza kuendeleza ajenda ya awali au hata ikiwezekana mpya na yenye mvuto zaidi.
 
2020 pia hawagombei bali wanachukua nchi![emoji30][emoji30][emoji30]
Na nini matokeo ya mwisho huku mitaani au ndio tutakuwa na wenyeviti miungu watu wenye viburi visivyomithilika? au ndio wananchi hawatashirikiana na wenyeviti wao ama kinyume chake? Je mashirikiano kijamii yatakuwa kama awali pasi kujali uvyama? Je chuki hizi za kisiasa zitatupeleka wapi?
Naona giza...
Naona tunatumbukizwa shimoni...
 
[emoji30][emoji30][emoji30]
Screenshot_20191016-224559-picsay.jpeg
 
wangeshiriki unadhani nani angenufaika??
Wapo watu waliojiweka mkao wa kula 2020, kumbuka hata Mzee Lowassa alidandia jahazi na kumpiga kikumbo Dr. Slaa lakini mwisho wa siku haikuwa vile alitaka iwe.
 
Back
Top Bottom