CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Yale matambara ya kijani mpaka leo bado yananing'inia hapa Mza kwenye roundabout ya Nyerere road.
 
Wakati huu mngekuwa mnajenga hoja kwa ushahidi kama huu ulio wazi kukataa kabisa hawa watu wasimamie uchaguzi.
Hiyo mahakama imekwisha wapiga chini, mnazo mbinu gani zaidi ya hapo?
Ushahidi kama huu ulitolewa mahakamani majaji wa rufaa wakaukataa, hivyo hata ukauweka leo, kesho sidhani kama unasaidia. Lakini ni vema kuuweka. Tatizo kubwa ni mahakama zetu (judiciary) na majaji wa UPE akina.... and Co. Ltd!
 
Tunajua kuwa nchi hii inaendeshwa kwa kufuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977 na katika Katiba hiyo ya nchi, ibara ya 3(1) inasema hivi nikinukuu "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.

Nimeshangazwa sana na kitendo cha DED wa Ubungo, Beatrice Dominic, kwa kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kuzishusha bendera za chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, zilizotundikwa kwenye eneo linalotarajiwa kufanyika mkutano mkuu wa chama hicho la Mlimani City.

Nimuulize huyo DED hivi angeweza kutoa agizo la aina hiyo iwapo katika ukumbi huo ungekuwa unafanyika mkutano wowote wa CCM?

Ni dhahiri kuwa kitendo akichokifanya DED huyo ni uvunjaji wa waziwazi wa Katiba ya nchi yetu, ambayo inaeleza waziwazi kuwa nchi yetu itaendeshwa kwa kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi.

Tunafahamu pia kuwa chama cha Chadema ndio chama kikuu cha upinzani nchini

Hapa ndipo najiuliza ni kwanini Rais Magufuli anaendelea kumweka kazini DED huyo na hamfukuzi kazi, ambaye amevunja Katiba ya nchi waziwazi kabisa?

Kama kitendo alichofanya DED huyo hakina baraka za Mheshimiwa Rais, basi tutarajie kuwa atamfuta kazi kwa kuvunja Katiba ya nchi waziwazi kabisa

Iwapo Rais hatamfuta kazi DED huyo basi wananchi tutaelewa kuwa DED huyo aliyatenda hayo kwa "maagizo" yake.
 
Lengo kuu la kutaka kumfahamu ni kuweka kumbukumbu sawa kwa ajili ya vizazi vijavyo
Yaani wewe mtu akikuudhi tu unaomba kujua cv yake
Kiboko yako ni karujugumli alikutoa machozi
Sheria za mazingira serikali za mitaa inakataza kupeperusha hovyo mibendera bila kibali cha mkurugenzi,muulize mayor wako savimbi analijua hilo
 
Ni mchagga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…