CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Kama polisi wameziondoa ni kwa sababu Chadema hawakutii amri waliyopewa ya kuziondoa (kama sikosei walipewa masaa 2) na bill itapelekwa kwenye chama chao wasilie tu wakati watakapotakiwa kulipa bill ya Polisi pamoja na faini.

BTW CCM walikuwa na mkutano wao kule Mwanza, leteni picha za bendera zao ili kuwa fair.

Zilipambwa kwenye Barbara nyingi tu
 
HATUMFURAHISHI RAIS BALI TUNAMWARIBIA

Na Thadei Ole Mushi

Hebu Fikiria, Mahali ambapo Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa nchi amekaa na kamati kuu ya CCM Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri anaweza kutoa agizo la Bendera za Chama ziondolewe? Definitely hilo haliwezekani lakini kwa Chadema mahali ambapo Chama kikuu cha Upinzani kinakutana na kamati yake kuu na baraza kuu kwa ajili ya mkutano wake mkuu anatokea mtu tu anaamuru zitolewe.

Yeye anafikiri amekisaidia sana Chama Chetu CCM, anafikiri kwa kufanya Hivyo kamfurahisha sana Rais wetu. Hili ni kosa la kimkakati kabisa.

Katika kipindi kama hiki ambacho Chadema inafuatiliwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa katika uchaguzi wake tunawapa political mileage, tunawapa agenda, tunawapa justification ya wao kuonewa je hivi ndivyo tunavyoijenga CCM?

Katika kipindi kama hiki taifa linapotaka maridhiano ya Kisiasa vijana wa ngazi za chini bila kutumwa na mtu yeyote anaamua kupanda mbigiri Mpya kwa taifa letu. Anaamua kuleta mitafaruku isiyokuwa ya Lazima kwa taifa letu.

Wakati binti Akwilina akipigwa Risasi kabla yalitoka maamuzi ya kipuuzi na yasiyo na weledi kama Haya kuwa chelewesheni Barua za mawakala. Zile barua zingewahi Chadema wasingeandamana na CCM bado ingelishinda. Tumekaa mahali na familia zetu tunajiandaa kwa Xmass wakati Binti asiyekuwa na Kosa akiwa Kaburini anaendelea Kuoza. Tunajifariji kila upande kuwa Hatujui aliyerusha ile Risasi lakini tunajidanganya kwa kuwa Mungu anajua kila kitu.

Wakati Spring Revolution inaanzia Kule Tunisia na kusambaa maeneo Mengine ya North Afrika Tunisia ilikuwa kimya na Tulivu kabisa. Ben Ali alikuwa zake Ikulu na mambo yalikuwa yakienda kama kawaida Kosa la Askari wawili tu kumpiga vibao kijana Bouaziz kilitosha kuleta machafuko Makubwa na kusambaa hadi nchi nyingine. Hawa Askari hawakutumwa na Ben Ali walijiamulia tu kwa kufikiri wanamfurahisha Rais.

Umoja, Mshikamano hauletwi na Maamuzi ya aina hii.

Niwaambieni tu CCM kuwa Upinzani na hatari kubwa ya Chama chetu haupo njee ya CCM Bali upo ndani ya CCM. Chama changu hakijafikia kuogopa hadi Bendera.
Screenshot_20191218-075856.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAB hajawahi kuwa na fikra pevu. Kuna ka msemo kuwa "ukizoea kunywa utumbo, u sitegemee kuongea point" mkurugenzi tunamwonea bure. Tangu lini mkurugenzi akatoa amri kwa Polisi? Wahusika wapo, yeye kakurupushwa tu.
 
Basi hawa watu wanazidi kumharibia mh rais na wanazidi kulichafua jina zuri la nchi yetu, alafu waseme kuna watu siyo wazalendo wanaichafua nchi yetu kwa mabeberu
DAB hajawahi kuwa na fikra pevu. Kuna ka msemo kuwa "ukizoea kunywa utumbo, u sitegemee kuongea point" mkurugenzi tunamwonea bure. Tangu lini mkurugenzi akatoa amri kwa Polisi? Wahusika wapo, yeye kakurupushwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama polisi wameziondoa ni kwa sababu Chadema hawakutii amri waliyopewa ya kuziondoa (kama sikosei walipewa masaa 2) na bill itapelekwa kwenye chama chao wasilie tu wakati watakapotakiwa kulipa bill ya Polisi pamoja na faini.

BTW CCM walikuwa na mkutano wao kule Mwanza, leteni picha za bendera zao ili kuwa fair.
Ina maana bendera za chama siku hizi haruhusiwi kupeperushwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vyovyote huyu DED ana baraka zote za wakubwa wake, CDM kamwe msijibu ujinga huu wa kipambuvu kwa upumbavu bali busara ziendelee kuwatawalakama kawaida yenu. No hate no fear
 
Nanyie ndo mjifunze sasa hao watu wa ivo ndo mnaenda kutafuta malidhiano nao
 
Hivi inaweZekana anasoma haya huyo mwanamke na sura ngumu!
Mkuu acha kunishangaza, uliwahi kuona mwanamama mwana ccm asiye na sura ngumu?
Ukiona au kubahatika kumpata wa hivyo ujue ameingia humu sio kiutendaji bali kimkakati ili wazee waendelee "kukitumikia chama bila uchovu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni MD kwa maana ya Municipal Director na sio DED kwa maana ya District Executive Director..Sio kila Mkurugenzi anatumia hivyo vifupisho vya DED.
 
Kama polisi wameziondoa ni kwa sababu Chadema hawakutii amri waliyopewa ya kuziondoa (kama sikosei walipewa masaa 2) na bill itapelekwa kwenye chama chao wasilie tu wakati watakapotakiwa kulipa bill ya Polisi pamoja na faini.

BTW CCM walikuwa na mkutano wao kule Mwanza, leteni picha za bendera zao ili kuwa fair.

Wakipeleka hiyo unayoiita "bill" wasisahau kuambatanisha na kifungu cha sheria kilichovunjwa kwa uwepo wa bendera hizo kwa tukio halali kabisa la kichama hata mwisho wa siku wawe na guts za kuomba kulipwa fedha!!

Hao polisi wako (kama kweli wamefanya hii kazi), wamejituma wao wenyewe kufanya kazi isiyowahusu kisheria na iliyo kinyume na taratibu. DED wa Kinondoni alipe "bill" hiyo na shughuli inaendelea......
 
Back
Top Bottom