HATUMFURAHISHI RAIS BALI TUNAMWARIBIA
Na Thadei Ole Mushi
Hebu Fikiria, Mahali ambapo Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa nchi amekaa na kamati kuu ya CCM Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri anaweza kutoa agizo la Bendera za Chama ziondolewe? Definitely hilo haliwezekani lakini kwa Chadema mahali ambapo Chama kikuu cha Upinzani kinakutana na kamati yake kuu na baraza kuu kwa ajili ya mkutano wake mkuu anatokea mtu tu anaamuru zitolewe.
Yeye anafikiri amekisaidia sana Chama Chetu CCM, anafikiri kwa kufanya Hivyo kamfurahisha sana Rais wetu. Hili ni kosa la kimkakati kabisa.
Katika kipindi kama hiki ambacho Chadema inafuatiliwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa katika uchaguzi wake tunawapa political mileage, tunawapa agenda, tunawapa justification ya wao kuonewa je hivi ndivyo tunavyoijenga CCM?
Katika kipindi kama hiki taifa linapotaka maridhiano ya Kisiasa vijana wa ngazi za chini bila kutumwa na mtu yeyote anaamua kupanda mbigiri Mpya kwa taifa letu. Anaamua kuleta mitafaruku isiyokuwa ya Lazima kwa taifa letu.
Wakati binti Akwilina akipigwa Risasi kabla yalitoka maamuzi ya kipuuzi na yasiyo na weledi kama Haya kuwa chelewesheni Barua za mawakala. Zile barua zingewahi Chadema wasingeandamana na CCM bado ingelishinda. Tumekaa mahali na familia zetu tunajiandaa kwa Xmass wakati Binti asiyekuwa na Kosa akiwa Kaburini anaendelea Kuoza. Tunajifariji kila upande kuwa Hatujui aliyerusha ile Risasi lakini tunajidanganya kwa kuwa Mungu anajua kila kitu.
Wakati Spring Revolution inaanzia Kule Tunisia na kusambaa maeneo Mengine ya North Afrika Tunisia ilikuwa kimya na Tulivu kabisa. Ben Ali alikuwa zake Ikulu na mambo yalikuwa yakienda kama kawaida Kosa la Askari wawili tu kumpiga vibao kijana Bouaziz kilitosha kuleta machafuko Makubwa na kusambaa hadi nchi nyingine. Hawa Askari hawakutumwa na Ben Ali walijiamulia tu kwa kufikiri wanamfurahisha Rais.
Umoja, Mshikamano hauletwi na Maamuzi ya aina hii.
Niwaambieni tu CCM kuwa Upinzani na hatari kubwa ya Chama chetu haupo njee ya CCM Bali upo ndani ya CCM. Chama changu hakijafikia kuogopa hadi Bendera.
Sent using
Jamii Forums mobile app