CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Hapa ndio utawapenda wabongo. Wote wanajua agizo limetoka wapi lakini wanazuga zuga weee
 
Chadema walifikili mlimani city ni ufipa watajuta sana

State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kama CCM mnapendwa sana na wananchi Kwa sababu ya kazi zenu nzuri za kuleta maendeleo, na mmepata ushindi wa kishindo juzi, kinachiwasumbua ni kitugani? Mnaziogopaje bendera za Chadema ambayo hata kitu kimoja cha Serikali za mitaa hawakupata?
Mbona mnashangaza sana??!!

Masajili wa vyama, anayejigamba kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa na hana chama, amesemaje? Atalikalia hili kimya? Hawezi kuona kuwa chama kinaonewa? Au yeye ni mlezi wa CCM?

Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa upande wa CCM.
Toeni mazingira sawa ya siasa muone moto wa Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia zaidi ya 90, ya wateule wa baba Jesca wameshajua baba J anataka nini.. Kwa tamko la Mkurugenzi awamu hii tayari amejijengea mazingira ya kupandishwa cheo. Na msishangae soon akapandishwa cheo. Kwani mtu tulie nae ni wa ajabu sana.
Uzi tayari....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mystery, kanuni ya vyama vya siasa inasemaje kuhusu kuchezea mali za vyama vya siasa mfano kushusha bendera, au hata hili mpaka msajili apewe taarifa au kwa kuwa ni CHADEMA business as usual!!!?
 
Kwa vyovyote huyu DED ana baraka zote za wakubwa wake, CDM kamwe msijibu ujinga huu wa kipambuvu kwa upumbavu bali busara ziendelee kuwatawalakama kawaida yenu. No hate no fear
Ndiyo maana alivyohutubia Jiwe kwenye ziara zake kule kanda ya Ziwa,alisema kuwa yeye anawateua kwenye nafasi zake za uteuzi "vichaa" wenzie!

Nadhani sasa mnaelewa kuwa mnaongozwa na mtu wa aina gani!
 
Asilimia zaidi ya 90, ya wateule wa baba Jesca wameshajua baba J anataka nini.. Kwa tamko la Mkurugenzi awamu hii tayari amejijengea mazingira ya kupandishwa cheo. Na msishangae soon akapandishwa cheo. Kwani mtu tulie nae ni wa ajabu sana.
Uzi tayari....

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Kama kapewa maagizo toka Juu ulitegemea asitekeleze? Mfano akaagizwa na mkuu wa Mkoa unatarajia nini? Kuna wakubwa wanawatumia wadogo kuumiza raia na Kwa mujibu wa mfumo wa nchi unapaswa uitie ndio mkuuu ndio mkuu akikata Simu unanyanyua Simu yako unaaanza kukusanya watekelezaji ndiko tuliko fika Kwa sasa
Nchi imekabidhiwa..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HATUMFURAHISHI RAIS BALI TUNAMWARIBIA

Na Thadei Ole Mushi

Hebu Fikiria, Mahali ambapo Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa nchi amekaa na kamati kuu ya CCM Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri anaweza kutoa agizo la Bendera za Chama ziondolewe? Definitely hilo haliwezekani lakini kwa Chadema mahali ambapo Chama kikuu cha Upinzani kinakutana na kamati yake kuu na baraza kuu kwa ajili ya mkutano wake mkuu anatokea mtu tu anaamuru zitolewe.

Yeye anafikiri amekisaidia sana Chama Chetu CCM, anafikiri kwa kufanya Hivyo kamfurahisha sana Rais wetu. Hili ni kosa la kimkakati kabisa.

Katika kipindi kama hiki ambacho Chadema inafuatiliwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa katika uchaguzi wake tunawapa political mileage, tunawapa agenda, tunawapa justification ya wao kuonewa je hivi ndivyo tunavyoijenga CCM?

Katika kipindi kama hiki taifa linapotaka maridhiano ya Kisiasa vijana wa ngazi za chini bila kutumwa na mtu yeyote anaamua kupanda mbigiri Mpya kwa taifa letu. Anaamua kuleta mitafaruku isiyokuwa ya Lazima kwa taifa letu.

Wakati binti Akwilina akipigwa Risasi kabla yalitoka maamuzi ya kipuuzi na yasiyo na weledi kama Haya kuwa chelewesheni Barua za mawakala. Zile barua zingewahi Chadema wasingeandamana na CCM bado ingelishinda. Tumekaa mahali na familia zetu tunajiandaa kwa Xmass wakati Binti asiyekuwa na Kosa akiwa Kaburini anaendelea Kuoza. Tunajifariji kila upande kuwa Hatujui aliyerusha ile Risasi lakini tunajidanganya kwa kuwa Mungu anajua kila kitu.

Wakati Spring Revolution inaanzia Kule Tunisia na kusambaa maeneo Mengine ya North Afrika Tunisia ilikuwa kimya na Tulivu kabisa. Ben Ali alikuwa zake Ikulu na mambo yalikuwa yakienda kama kawaida Kosa la Askari wawili tu kumpiga vibao kijana Bouaziz kilitosha kuleta machafuko Makubwa na kusambaa hadi nchi nyingine. Hawa Askari hawakutumwa na Ben Ali walijiamulia tu kwa kufikiri wanamfurahisha Rais.

Umoja, Mshikamano hauletwi na Maamuzi ya aina hii.

Niwaambieni tu CCM kuwa Upinzani na hatari kubwa ya Chama chetu haupo njee ya CCM Bali upo ndani ya CCM. Chama changu hakijafikia kuogopa hadi Bendera.

Anyway Ngoja nirudi jalalani....

Ole Mushi.
0712702602

FB_IMG_1576649421058.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mystery,
Mkuu kitendo chochote ambacho hakiwezi kufanywa kwa tawala ukikifanya kwa upinzani ni point za kukuweka salama katika kiti ulichonacho. Mifano ipi mingi tu!! Fungua macho uyaone!! Wala usingepata tabu kumpangia cha kufanya! Hapangiwiiii iiiiii
 
Mnapenda kusema amevunja katiba huku mkiambiwa mtaje hivyo vipengele alivyovunja hata hamvijui.
 
Hapo msajili atakuwa kiiimya kabisa
Matangazo yote yanatakiwa kulipiwa Manispaa yawe ya Chama au la. Ubungo meya ni CHADEMA kazi yake mmojawapo Ni kuhakikisha Manispaa inapata mapato yake.

Mabendera Ni matangazo ya biashara isipokuwa yakiwa kwenye Ofisi za Chama au matawi.

Hawezi fukuzwa kazi anatimiza wajibu wake wa kazi CHADEMA walipe Tena siku zote walizopeperusha na faini juiu
 
Mkuu kitendo chochote ambacho hakiwezi kufanywa kwa tawala ukikifanya kwa upinzani ni point za kukuweka salama katika kiti ulichonacho. Mifano ipi mingi tu!! Fungua macho uyaone!! Wala usingepata tabu kumpangia cha kufanya! Hapangiwiiii iiiiii
Hivi wapinzani wakiidai kuwa nchi hii inaendeshwa kidikteta, watakuwa wanakosea kweli?
 
Kitendo cha kung'oa bendera za chama kilichoandikishwa kihalali nchini ni kosa la jinai, ambalo mhusika anaweza hata akafungwa jela
Bendera zinatakiwa ziwe mahali kisheria.hixo hazikuwrpo kisheria kwani hawakulipia gharama za matangazo Manispaa Kama Sheria za jjiji lao ambalo liko chini ya chadema zinavyosema.Kuwa kila tangazo litalipiwa jiji
 
Back
Top Bottom