Pre GE2025 Chadema yapigilia msumari masharti ya kushiriki kwao, wakisisitiza 'No reform, no election'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Marekani states 50 zimeungana. Wabunge hutegemea wingi wa watu. Ndio maana kuna states zina wabunge 50 na zingine wawili.

Uingereza zimeungana nchi nne. England, Scotland, Northern Ireland and Wales. Wabunge wao kutokana na idadi ya watu. Ndio maana Nirthern Ireland ina wabunge wachache
 
Mwambieni Huyu Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri. Asome Muungano wa states za Marekani ukoje kuhusu wabunge?
Asome wa Waingereza ukoje kuhusu Wabunge?

Sisi ni kama hao tu na wabunge wamefuata uwingi wa watu.
 
Wewe sio mhariri.
Mkuu Mwami, Mwami Ntale , je unamjua mhariri ni nani na mwandishi wa habari ni nani, hadi useme mimi sio mhariri?. Unajua mimi nafanyia kazi media gani?. Je unaijua PPR Media?, unamjua mhariri mkuu wa PPR Media?.
Wewe ni mwandishi wa habari za ccm.
Mimi sio mwandishi wa habari wa CCM, mimi ni mwandishi wa habari wa PPR.
Kila kitu unakiangalia kwa kutumia jicho la ccm .
Sii kweli!.
Ulishakiri humu kuwa unaamini ccm itatawala milele.
Ni kweli CCM itatawala milele!.
Kwahiyo huwezi kujizuia unaposhika kalamu yako,bali muda wote huwa unaipendelea ccm.Hufai .
Sii kweli!.
Angalia baadhi ya hizi mada zangu, kama kweli zinapendelea CCM.

P
 
Kuhusi Kinachoongelewa Hapa. Ni Dhahiri Tundu Lissu ni Hazina ya Taifa.
Unrealistic mahaba, let us wait and see atazuiaje uchaguzi na nguvu ya Umma...labda akodishe GEN Z kutoka Kenya. Tanzania bado sana kujitambua, bado sana nguvu ya Umma!

All in all I wish him the best of the maandalizi from now to attain that!
 
"Hapa hatutazungumza sera zingine tutazungumza habari ya uchaguzi kwasababu tunatekeleza maamuzi ya chama chetu (CHADEMA), tunataka (Wahariri) mtuelewe, tunataka mkituelewa kama mnakubaliana na sisi na nyinyi muwe sehemu ya mapambano haya,"
Lissu kwa hakika ni mtu makini sana. Hili jibu hapa na dokezo lake huku chini ni jibu sahihi kabisa kuhusu mkutano huo.
Natumaini watakuwa wamemwelewa vyema.
 
Ikitokea huo "Umma" ukakataa au ukishindwa kuzuia huo uchaguzi, CHADEMA Bado itashiriki?
 
TAHADHALI:
Mfa maji haachi kutapatapa. CCM watatumia kila njia; hata ya kutapatapa wakidhani hawatazama.
Sitaki kuzitaja hizo njia chafu hapa, lakini ndiyo 'option' pekee wanayotegemea CCM kuzuia adhma ya "No Reform, No Election'. Usifikiri CCM watakaa wakisubiri uchaguzi uzuiwe..., watazuia juhudi hizo kwa njia mbalimbali.

Kwa hiyo CHADEMA ni lazima wajizatiti na kuwa tayari kwa lolote. Hii CHADEMA isiwe ni ya kutegemea viongozi wa juu pekee. Kampeni toka mwanzo ni lazima iwe ya wananchi/wanachama/wapenzi wa chama na waTanzania wote wenye mapenzi na nchi hii
Kampeni hii isizuiwe kwa kuwaondoa viongozi wa juu wa chama. Kampani ni lazima iwe 'movement' ya watu toka mwanzo.

Kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha katika miezi hii michache CHADEMA itawezaje kuifikisha kwa umma wa waTanzania kwa ufanisi mkubwa. Ni lazima kampeni ienee kwenye matawi mitaani, vijijini; kwenye kata/tarafa kila wilaya na mikoa yote kwa haraka zaidi.
Viongozi wa chama kwenye ngazi hizo ni lazima kuchukua majukumu hata bila kuwepo viongozi wakuu wa chama kuwepo.
Haya ni mapambano ya kufa na kupona, kwa maslahi ya Tanzania.
 
Unrealistic mahaba, let us wait and see atazuiaje uchaguzi na nguvu ya Umma...labda akodishe GEN Z kutoka Kenya. Tanzania bado sana kujitambua, bado sana nguvu ya Umma!

All in all I wish him the best of the maandalizi from now to attain that!
Mkuu 'Retired' nilikuwa sijakusoma baada ya zile kampeni na uchaguzi kufanyika.

Pole sana!
Kwa hiyo sasa unasubiri Tundu Lissu na timu yake, na chama kwa ujumla waangukie pua, uje utueleze kuwa ulitutahadharisha?
Tuwaombe tu msiwe washiriki wa kuzuia mabadiliko haya yanayo tegemewa kwa hamu kubwa.
 
Handeni Vijijini Wapiga kura
Asante kwa taarifa, wahariri tupo na hatuna hofu.
P
Pascal Mayalla nakuona wakati huu ukizungumza.

Asante sana nimekuona tena Live......umerudia tena mambo yako ya Utopia😀😀
 
Ikitokea huo "Umma" ukakataa au ukishindwa kuzuia huo uchaguzi, CHADEMA Bado itashiriki?
Ulisikia wapi wananchi wooote ndani ya nchi walishiriki kuleta mabadiliko. Sehemu kubwa ya wananchi katika nchi yoyote hufuata tu matokeo ya mapambano kati ya pande zinazopingana.
Kuzuia uchaguzi huhitaji kuwa na waTanzania milioni 60 na zaidi kufanya hivyo.

Ni lini wewe ulisikia CCM ilikubaliwa na watu wote kuwa madarakani?
Swali zuri sana hili
Siyo swali zuri kama unavyo fikiri wewe.
 
Balile aliwahi kuwa mtu wa maana kipindi fulani lakini tangu alipolambishwa asali hasa ya DIIPIIWELDI ile akili na weledi wake kaukabidhi kwa yule mzee raia wa pori la GOMBE
 
Huyu balile analeta mambo ya kishamba, afadhali Ndugu Pascal Mayalla umempa za uso kwamba hamuwezi lissu na wakati mwingine awe makini anapo deal na watu wagumu aina hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…