Pre GE2025 Chadema yapigilia msumari masharti ya kushiriki kwao, wakisisitiza 'No reform, no election'

Pre GE2025 Chadema yapigilia msumari masharti ya kushiriki kwao, wakisisitiza 'No reform, no election'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ametoa maoni yake kuhusu hali ya ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akisisitiza kuwa chama hicho kilikumbwa na majeraha makubwa wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita na sasa kinahitaji kujenga umoja na mwelekeo mpya wa kisera.

"Siku moja nilisema wakati mnafanya kampeni zenu za uchaguzi CHADEMA, mlijeruhiana sana na sisi tunajua kazi yetu ni kama fundi nyundo, ukiwa unaezeka bati huangalii kwamba ni saa sita mchana huwezi kupanda juu kugonga msumari. Kufikisha ujumbe ndilo jukumu letu la msingi," amesema Balile.

"Mpaka ikafika hatua nikasema ama Tundu Lissu ama Mbowe atakayeshinda baada ya uchaguzi huu ninaamini ataanza kuzungumza kama Mwenyekiti. Wakati ule mlikuwa hamzungumzi kama Mwenyekiti bali kama wagombea."

"Nimeona CHADEMA ya Wenyeviti wote waliotangulia na sasa Tundu Lissu, mlikuwa na sera yenu ya majimbo, lakini haizungumzwi sana siku hizi," amesema Balile, akitaka kufahamu ikiwa sera hiyo bado ni nguzo muhimu kwa chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu akizungumza wakati wa mkutano kati ya CHADEMA na Jukwaa la Wahariri (TEF)

"Hapa hatutazungumza sera zingine tutazungumza habari ya uchaguzi kwasababu tunatekeleza maamuzi ya chama chetu (CHADEMA), tunataka (Wahariri) mtuelewe, tunataka mkituelewa kama mnakubaliana na sisi na nyinyi muwe sehemu ya mapambano haya,"

"Vyombo vya habari ni sehemu muhimu sana ya mapambano haya na ni sehemu muhimu vilevile ya ukandamizaji, kwasababu wanaokandamiza si tu wanakandamiza vyombo vya habari lakini vilevile wanataka kuweka vyombo vya habari viwasaidie katika ukandamizaji wao. Vyombo vya habari vinaweza kutumika kama daraja la ukombozi na vinaweza kutumika na vimetumika katika historia kama vyombo vya ukandamizaji. Tunataka vyombo vya habari vya Tanzania vichague upande wa kuwa vyombo vya ukombozi, vyombo vya kuleta demokrasia katika nchi ya Tanzania."

"Sasa shida iko wapi? Kwanini kila tume inayoteuliwa (Ikiwamo Tume ya Jaji Warioba) inasema tufanye mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi? Huu mfumo wa uchaguzi una shida gani hasa? Na hii shida hii ndiyo inayoelezea sababu ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi."

"Hiyo shida ndiyo tunayosema isipotatuliwa hakutakuwa na uchaguzi. Mheshimiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, lugha yangu ilikuwa bayana kabisa, tumesema siyo hatutasusia uchaguzi, tutazuia uchaguzi, lugha siyo kususia uchaguzi lugha ni kuzuia uchaguzi, na tumesema tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya umma, tutawaalika Watanzania wahakikishe uchaguzi huu haufanyiki."

"Bila mabadiliko hakuna uchaguzi na siyo bila mabadiliko hatutashiriki uchaguzi, hiyo siyo lugha yetu, lugha yetu ni bila mabadiliko uchaguzi hautafanyika, ndiyo lengo letu. Sasa ni kwanini, hii lugha mbona kali sana, ni kwanini? Mfumo wetu wa uchaguzi una shida gani? na kwanini wazee waliopendekeza ubadilishwe kwanini walipendekeza hivyo? Una shida gani? Shida ya kwanza kabisa, mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo wa Rais, ambao unadhibitiwa kutoka juu mpaka chini ya Rais na mnafahamu Rais wa nchi hii ni Mwenyekiti wa CCM, na Marais wa CCM wametumia udhibiti wao wa mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kwamba CCM inabaki madarakani kwa njia zozote, nyingi haramu"

"Majimbo haya yametengenezwa kwa upendeleo mkubwa sana – upendeleo kati ya Tanganyika na Zanzibar, kati ya miji na vijijini, na kati ya mikoa na mikoa. Matokeo yake, dhana ya usawa wa uwakilishi wa umma imevurugwa kabisa,"

"Jiulize, haya majimbo ni kwa ajili ya uchaguzi wa binadamu au kwa ajili ya kuangalia wapi tutaweka barabara na umeme? Kwa nini idadi ya watu haizingatiwi?"

"Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Jimbo la Temeke lilikuwa na wapiga kura 478,000 waliomsimamisha mbunge mmoja. Lakini kwa upande wa Zanzibar, majimbo yote 50 yalikuwa na wapiga kura 566,000 tu, ambao waliwachagua wabunge 50. Hii ina maana kwamba mbunge mmoja wa Temeke anawakilisha watu wengi zaidi kuliko wabunge wote wa Zanzibar kwa pamoja, lakini bado wote wanalipwa mshahara sawa na posho sawa."

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akifika kwenye kujadili muungano naomba mnijuze..
 
wana shida sana tena sana, lakini bado ni class ile ile ya Lumpen proletariat! They resist changes as long as wanapata bamia na mlenda wanakula na jioni wanapata K kwa wake zao...all is over!
😀😀😀we jamaa
 
sidhani........ yafute matumaini hayo....tafuta njia sahihi za kuzuia uchaguzi na si watanzania waoga kama tulivyo wewe na mimi......
Mkuu mi nadhani kwa maoni yangu na mtazamo ninavyouona, mbinu pekee ambayo Chadema wanaweza kuzuia uchaguzi ni kutengeneza "unrest" situation. Napata mashaka hayo baada ya kuanza kuona tuvikundi kundi kama hawa vijana wanaoibuka hivi sasa wa NATO sijui. Maana narejea hali kama hii kipindi cha JK mara usikie sijui CWT wana hili mara kule kuna hili.
Lakini kwa yote hayo binafsi siyaungi mkono. Chadema ingeshiriki uchaguzi na kutumia namna zote kulinda kura. No Reform No Election I don't think if it will work out.

TANZANIA KWANZA!
MAJADILIANO NDIO SULUHU
MUNGU TUSAIDIE..
 
Watanzania wazalendo kwa nchi yao wanajiuliza kwa jinsi jua lilivyokali mwaka huu hivi ingekuwaje mgao wa umeme kama Hayati Magufuli asingejenga bwawa la umeme la mwl Nyerere?.
Ni majenereta mangapi yangeingizwa? Zingezaliwa Richmond ngapi?
Mwaka huu mvua ni chache nchi nzima na jua linatandika kwelikweli kiasi kwamba wakulima wamekosa mazao yao kwa kukauka shambani, lakini bado mafisadi yanaona aibu kutangaza mgao wa umeme kwa sababu wanaogopa watawaambia nini Watanzania kwa sababu wanajua bwawa lao la umeme walilojengewa na Rais wa wanyonge limekamilika na linauwezo wa kutoa megawati 2115.
Mafisadi kwa vikao vyao yanajiuliza sasa tutakula wapi? Na yanapofikia hiyo hatua humlaani Hayati Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo na yakimaliza yanamlaani pia Rais Samia kwa kukubali kumalizia miradi yote iliyoachwa na Magufuli ikiwemo hilo bwawa la umeme.
Matarajio ya mafisadi ilikuwa ni kwamba pale tu Magufuli alipofariki na ujenzi wa bwawa ungeishia hapo.
 
Mkuu mi nadhani kwa maoni yangu na mtazamo ninavyouona, mbinu pekee ambayo Chadema wanaweza kuzuia uchaguzi ni kutengeneza "unrest" situation. Napata mashaka hayo baada ya kuanza kuona tuvikundi kundi kama hawa vijana wanaoibuka hivi sasa wa NATO sijui. Maana narejea hali kama hii kipindi cha JK mara usikie sijui CWT wana hili mara kule kuna hili.
Lakini kwa yote hayo binafsi siyaungi mkono. Chadema ingeshiriki uchaguzi na kutumia namna zote kulinda kura. No Reform No Election I don't think if it will work out.

TANZANIA KWANZA!
MAJADILIANO NDIO SULUHU
MUNGU TUSAIDIE..
1. CCM will never heed to majadiliano. Forget about that, CCM acknowledging "defeat" in the sense that, to them, accepting free and fair elections is a defeat jeopardizing their grip of power!
2. Unrest situation will be met by police fierce brutality! This is the obvious!
3. NATO and the like ...a big question: are they ready to sacrifice Life?
4. Only M23 can make sense as Shisekedi is calling for serikli ya umoja wa kitaifa..coalition government!
 
Back
Top Bottom