mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
kwamba lisu hataki uchaguzi.?
sasa bila uchaguzi kutakuwa na chadema kweli.
sasa bila uchaguzi kutakuwa na chadema kweli.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa taarifa, wahariri tupo na hatuna hofu.
P
Hayo mambo ya tundu lisu anayoongea mtatekeleza lini...Mtoa mada kuwa makini na hy bangi unapouziwa, itakuwa wanachanganya na makapi.
Hayo mambo ya tundu lisu anayoongea mtatekeleza lini...Mtoa mada kuwa makini na hy bangi unapouziwa, itakuwa wanachanganya na makapi.
Hata Wewe ni hazinaKuhusi Kinachoongelewa Hapa. Ni Dhahiri Tundu Lissu ni Hazina ya Taifa.
Hazina zinazidiana ukubwaHata Wewe ni hazina
Hatujasema bila Reforms tutasusia, tumesema bila reforms tutahakikisha Uchaguzi haufanyiki kabisa.Ikitokea huo "Umma" ukakataa au ukishindwa kuzuia huo uchaguzi, CHADEMA Bado itashiriki?
Mimi pia sielewi mantiki ya huyu Mwejyekiti.Mimi simjui huyo Mwekiti wa Jukwaa ni nani; lakini kwa kusoma tu madokezo yake hapo juu, huyu siyo mwenye nia njema na chama.
Mara hii anachokonoa mambo na kuyafanya yawe kipaumbele cha viongozi wapya. Yeye ni nani?
Huyu atakuwa anawagongea nyundo CCM, bila shaka kwa fadhila za akina Abduli!
Viongozi wa CHADEMA wanayo mambo ya muhimu zaidi kuliko kusikiliza wanafiki wa aina hii.
Hakuna kipaumbele kwa viongozi wa CHADEMA sasa hivi kuliko kuzungumza na wananchi wa Tanzania; hasa kuhusu haki yao ya kupiga kura kwa uhuru wote na kura zihesabike kwa haki.
Kwanza muda wenyewe uliopo ni mfinyu sana kuitimiza hiyo kazi. Jukumu la vibaraka kama huyu ni kupotzea muda ajenda hiyo muhimu isifanyike kwa ufanisi kabla ya Oktoba.
Nasikia huko kuna chawa kaambiwa nonsense Kwa ujinga wakeKumekucha!
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ametoa maoni yake kuhusu hali ya ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akisisitiza kuwa chama hicho kilikumbwa na majeraha makubwa wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita na sasa kinahitaji kujenga umoja na mwelekeo mpya wa kisera.
"Siku moja nilisema wakati mnafanya kampeni zenu za uchaguzi CHADEMA, mlijeruhiana sana na sisi tunajua kazi yetu ni kama fundi nyundo, ukiwa unaezeka bati huangalii kwamba ni saa sita mchana huwezi kupanda juu kugonga msumari. Kufikisha ujumbe ndilo jukumu letu la msingi," amesema Balile.
"Mpaka ikafika hatua nikasema ama Tundu Lissu ama Mbowe atakayeshinda baada ya uchaguzi huu ninaamini ataanza kuzungumza kama Mwenyekiti. Wakati ule mlikuwa hamzungumzi kama Mwenyekiti bali kama wagombea."
"Nimeona CHADEMA ya Wenyeviti wote waliotangulia na sasa Tundu Lissu, mlikuwa na sera yenu ya majimbo, lakini haizungumzwi sana siku hizi," amesema Balile, akitaka kufahamu ikiwa sera hiyo bado ni nguzo muhimu kwa chama hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu akizungumza wakati wa mkutano kati ya CHADEMA na Jukwaa la Wahariri (TEF)
"Hapa hatutazungumza sera zingine tutazungumza habari ya uchaguzi kwasababu tunatekeleza maamuzi ya chama chetu (CHADEMA), tunataka (Wahariri) mtuelewe, tunataka mkituelewa kama mnakubaliana na sisi na nyinyi muwe sehemu ya mapambano haya,"
"Vyombo vya habari ni sehemu muhimu sana ya mapambano haya na ni sehemu muhimu vilevile ya ukandamizaji, kwasababu wanaokandamiza si tu wanakandamiza vyombo vya habari lakini vilevile wanataka kuweka vyombo vya habari viwasaidie katika ukandamizaji wao. Vyombo vya habari vinaweza kutumika kama daraja la ukombozi na vinaweza kutumika na vimetumika katika historia kama vyombo vya ukandamizaji. Tunataka vyombo vya habari vya Tanzania vichague upande wa kuwa vyombo vya ukombozi, vyombo vya kuleta demokrasia katika nchi ya Tanzania."
"Sasa shida iko wapi? Kwanini kila tume inayoteuliwa (Ikiwamo Tume ya Jaji Warioba) inasema tufanye mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi? Huu mfumo wa uchaguzi una shida gani hasa? Na hii shida hii ndiyo inayoelezea sababu ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi."
"Hiyo shida ndiyo tunayosema isipotatuliwa hakutakuwa na uchaguzi. Mheshimiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, lugha yangu ilikuwa bayana kabisa, tumesema siyo hatutasusia uchaguzi, tutazuia uchaguzi, lugha siyo kususia uchaguzi lugha ni kuzuia uchaguzi, na tumesema tutazuia uchaguzi kwa nguvu ya umma, tutawaalika Watanzania wahakikishe uchaguzi huu haufanyiki."
"Bila mabadiliko hakuna uchaguzi na siyo bila mabadiliko hatutashiriki uchaguzi, hiyo siyo lugha yetu, lugha yetu ni bila mabadiliko uchaguzi hautafanyika, ndiyo lengo letu. Sasa ni kwanini, hii lugha mbona kali sana, ni kwanini? Mfumo wetu wa uchaguzi una shida gani? na kwanini wazee waliopendekeza ubadilishwe kwanini walipendekeza hivyo? Una shida gani? Shida ya kwanza kabisa, mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo wa Rais, ambao unadhibitiwa kutoka juu mpaka chini ya Rais na mnafahamu Rais wa nchi hii ni Mwenyekiti wa CCM, na Marais wa CCM wametumia udhibiti wao wa mfumo wa uchaguzi kuhakikisha kwamba CCM inabaki madarakani kwa njia zozote, nyingi haramu"
"Majimbo haya yametengenezwa kwa upendeleo mkubwa sana – upendeleo kati ya Tanganyika na Zanzibar, kati ya miji na vijijini, na kati ya mikoa na mikoa. Matokeo yake, dhana ya usawa wa uwakilishi wa umma imevurugwa kabisa,"
"Jiulize, haya majimbo ni kwa ajili ya uchaguzi wa binadamu au kwa ajili ya kuangalia wapi tutaweka barabara na umeme? Kwa nini idadi ya watu haizingatiwi?"
"Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Jimbo la Temeke lilikuwa na wapiga kura 478,000 waliomsimamisha mbunge mmoja. Lakini kwa upande wa Zanzibar, majimbo yote 50 yalikuwa na wapiga kura 566,000 tu, ambao waliwachagua wabunge 50. Hii ina maana kwamba mbunge mmoja wa Temeke anawakilisha watu wengi zaidi kuliko wabunge wote wa Zanzibar kwa pamoja, lakini bado wote wanalipwa mshahara sawa na posho sawa."
"Utaratibu mzima wa kupiga kura umevurugwa na namna ya kuutengeneza kwanza ni kubadilisha Katiba ili kuwe na Haki ya Kikatiba ya kupiga kura, na pili Katiba iseme wapigakura na raia wa nchi hii na vyama vyao vya siasa wana haki ya kuthibitisha chochote inachokifanya Tume ya Uchaguzi, na ikikosea ishitakiwe mahakamani, sasa hivi haiwezekani."
"Utaratibu huu ndiyo uliokuwepo katika Katiba tuliyopewa na Waingereza mwaka 1961, katiba ya Waingereza ilikuwa bora kwenye masuala haya kuliko katiba ya Nyerere kuanzia mwaka 1962 mpaka hapa tulipo. Tumevuruga mambo muhimu kama haki ya kupiga kura"
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Upo nyuma ya mudaMkuu mi nadhani kwa maoni yangu na mtazamo ninavyouona, mbinu pekee ambayo Chadema wanaweza kuzuia uchaguzi ni kutengeneza "unrest" situation. Napata mashaka hayo baada ya kuanza kuona tuvikundi kundi kama hawa vijana wanaoibuka hivi sasa wa NATO sijui. Maana narejea hali kama hii kipindi cha JK mara usikie sijui CWT wana hili mara kule kuna hili.
Lakini kwa yote hayo binafsi siyaungi mkono. Chadema ingeshiriki uchaguzi na kutumia namna zote kulinda kura. No Reform No Election I don't think if it will work out.
TANZANIA KWANZA!
MAJADILIANO NDIO SULUHU
MUNGU TUSAIDIE..
We mbweha unaogopa mapambano?Huyu jamaa hawezi kuongea kitu bila kuweka neno "Mapambano" akili yake imekaa ki mawazo ya kupiganapigana tu na sio kiungozi wa hekima na busara.
True.Mungu awalinde hawa viongozi wenye upeo mkubwa namna hii...
Ukimsikiliza Tundu Lissu, unaona ukweli mtupu....
Kutekwa?Balile naye anaogopa jamani.
Mbweha mama yako aliyekuzaa , "Mbaanyoko"We mbweha unaogopa mapambano?
We mbweha tu, tena mwogaMbweha mama yako aliyekuzaa , "Mbaanyoko"
Mbweha mama yako, mwoga babaako aliyekuzaaWe mbweha tu, tena mwoga
We mbweha tu, hahahahaaaaMbweha mama yako, mwoga babaako aliyekuzaa
Umeshaharibiwa kama Bosi wako huko Belgium walivyomuharibuWe mbweha tu, hahahahaaaa