Mimi si mfuasi wa vyama bali ni mfuasi wa hoja zenye manufaa kwa ustawi wa watu na taifa.
Japokuwa aliyekuuliza ametumia kejeli ktk swali lake, lakini hii ni hoja kubwa Sana inayotuumiza Wananchi kutokana na serikali ya ccm kushindwa kuweka sera nzuri za kulinda mazingira na kutoa unafuu wa matumizi ya nishati asilia ambayo ni mbadala wa uharibifu wa mazingira hasa kwa Wananchi maskini.
Je, mpango wa gesi ya mtwara iliyotusababishia vifo na ulemavu kwa kutupiga kama wanyama uko wapi? Je hii siyo sera mbovu?
Ama kuhusu ccm kuimarika na upinzani cdm kukosa ushawishi, siyo kweli maana huku mitaani hakuna hata kijana anayejisikia uhuru au kujihisi furaha kwa kujinasibu na uccm.
Mfano mzuri kwa uchunguzi binafsi nilioufanya hapa Dar ktk chaguzi za viongozi wa uvccm kata, wengi wa vijana waliogombea ni wale wenye uelewa mdogo Sana wa masuala ya kijamii na wenye kiwango kidogo cha elimu. Vijana wengi walio na uelewa mpana wa kielimu hawajagombea.
Mwisho hata hayo mavazi ya ccm hawayavai mitaani isipokuwa tu ktk vikao vyao vya chaguzi na ziara za viongozi wao.