CHADEMA yapoteza ushawishi mitaani. Sare zake hazivaliki

CHADEMA yapoteza ushawishi mitaani. Sare zake hazivaliki

Utazani× utadhani
Hadhina× hazina
Kwa maneno hayo unathibitisha pasipo shaka kuwa wewe ni mmoja kati ya wale wanaccm waliosemwa na twaweza.
 
Hainizuii kuandika habari za chadema maana wametafuna Sana Kodi zetu walizokuwa wanapokea Kama ruzuku
Kama una uchungu sana na kodi kazae..lakini pia unaweza kufungua kesi mahamakani kama ushahidi unao......kubwata na kuandika utumbo mitandaoni haikusaidii chochote zaidi ya kujipa maumivu ya moyo
 
Hata mikutano ya hadhara ikianza bado Chadema Haina ushawishi wowote ule kwa sasa
Haya ndio matamanio ya kila mwanaccm, na CDM wakilianzisha utasikia CCM wanaanza kulialia na matumizi ya vyombo vya dola yanarejea rasmi. CCM sio chama cha kizazi hiki, hata ifanye nini ni rahisi kuzidiwa pindi ushindani ukianza.
 
Kama una uchungu sana na kodi kazae..lakini pia unaweza kufungua kesi mahamakani kama ushahidi unao......kubwata na kuandika utumbo mitandaoni haikusaidii chochote zaidi ya kujipa maumivu ya moyo
Utapeli wenu huo ndio umepelekea wananchi wawapuuze kwa kila kitu
 
Haya ndio matamanio ya kila mwanaccm, na CDM wakilianzisha utasikia CCM wanaanza kulialia na matumizi ya vyombo vya dola yanarejea rasmi. CCM sio chama cha kizazi hiki, hata ifanye nini ni rahisi kuzidiwa pindi ushindani ukianza.
Hakuna chama Cha kuisumbuaa CCM nchi hii maana vyama vyote vimejikatia tamaa na kuandamwa na migogoro isiyo Keisha kutokana na ubadhirifu wa viongozi ndani ya vyama vya upinzani inayofanywa na viongozi wanaovitumia vyama Kama Saccos zao au miradi yao binafsi
 
Bwana Mwashambwa huwa nikiangalia maandiko Yako huwa najipa majibu mawili
1. Ama unajitoa ufahamu Ili UONE mwitikio wa umma kwa manufaa ya watawala kwa gharama ya walio wengi
2. Au unajipendekeza kwa kuandika mambo dhahania au ya kufikirika ambayo hayaakisi uhalisia wa maisha ya watanzania wa kawaida.

Nikirejea katika andiko Lako ambalo badala ya kuonesha ni kwa namna Gani serikali na chama Cha mapinduzi vimejikita katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya watanzania kisiasa na kijamii na kiuchumi umeifanya chadema na Sio chama vingine kama stepping stone kwa ajili ya kuwasilisha maudhui Yako.

Utaratibu huu ni wa kijinga ashakumu Sio matusi, kutumia wait wengine kuhalalisha mapungufu ya chama na serikali, JF ni GT platform Sio fb. Unachokifanya ni kujijengea fame kwa watu ambao wanawaza mara tati ZAIDI Yako!.

Umerejea wanafunzi wa vyuo vikuu kukiunga mkono chadema Ila umesahau kuwa Kuna wanavyo vikuu wengi waliunga mkono CCM.
Hii ni kwa sababu University ilikua ni think tank ya Taifa. Viongozi wa chama na serikali waliweza kuwasikiliza wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa vyuo vikuu vilikua na hoja za nguvu!
Kitendo Cha hata bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa misingi ya uanachama katika nchi ya vyama vingi ni sababu tosha ya kushusha morali ya wanachadema vyuoni, rejea kauli ya Bwana Pole pole ya kuwataka wanafunzi amabao ni uvccm ambao hawajapata mikopo wajioridheshe majina Yao.

Lakini pia kitendo Cha mwenyekiti wa ccm (mwendazake) kuwakataza wanafunzi wa vyuo vikuu kujihusisha na siasa na kwa kuwa alikua na mkono wa chuma isingekua rahisi kwa vijana wa chadema kujihusisha na siasa pamoja na siasa kwa sababu ya mkono wa Dola!

Kwa ulichokitaja(miaka kadhaa) umekua mvivu wa kutaja miaka ipi? Mingapi? Ukweli ni kwamba vijana walihamasika kuikataa CCM na wataikataa sababu kubwa ilikua ni utekelezaji usioridhisha wa ahadi zake katika uchaguzi na pili ni kukithiri kwa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma huku wananchi walio wengi wakiendelea kutokea katika umaskini.

Hayo hapo Juu ndio yaliyofanya vijana wa ccm na wanachama wengine kuona aibu kubwa sare za Cha chama au kwenda mikutanoni kwa kificho Jambo ambalo umeshindwa kulieleza au kwa makusudi umekaataa kuliandika.
Kwa maana Hiyo vijana wa chadema walikua na uwezo wa kutembea kifua mbele hasa ukizingatia aliyekua rais wa wakati huo hakua na siasa za mkono wa chuma na alikubali serikali yake kuwajibika pale ilipokosolewa. Rejea kashfa Mbali Mbali za ufisadi halo kadhalika uhuru wa vyombo cya habari kuelezea kwa umma Juu ya halo halisi ya nchi ambayo mwendazake alibinya kwa mkono wa chuma! Rejea alipolionya gazeti la Mwananchi "you are not free to such a extent" rejea wahariri Mbali Mbali wa magazeti walivyofukuzwa kazi pamoja na kufungia kwa baadhi ya magazeti ya habari za uchunguzi !

Kwakua mwendazake aliyafanya hayo kwa kutumia mkono wa chuma na Dola Nani asiyependa kuishi uraiani au kuishi na apoteze uhai wake? Au umesahau kuwa Kuna kipindi nchi hii MTU akitoa mawazo tifauti na ya watawala alionekana mhaini?

Umesema vijana wa ccm wakipata mashambulizi yasiyo ya kawaida! Lakini labda kwa sababu ya uchama umeshindwa kusema mashambulizi hayo ni ya hoja au ya kimwili kudhuru mwili. Kimsingi vijana wa ccm hawana uwezo wa kuhimili hoja zenye nguvu na maswali ya msingi yanayogusa wananchi wa kawaida badala yake wanasubiri watu Fulani wawaeleze Nini Cha kusema na kukanusha yale Yale waliyosyesma wao "mlininukuu vibaya"
Hali hii ilifanya hata mwenyekiti wa chama asiwaamini na kuamua kuufifisha UPINZANI ama kwa kuwanunua (rejea ya nasari arusha) au kuwateua katika nafasi za uongozi rejea (mtatiro na katambi)

Umeipongeza ccm kwa kujisahihisha dhidi ya chadema (sio Sahihi) ccm inashika madaraka ya nchi hii kwa miaka ZAIDI ya 60 Sasa. Na ccm haiitaji kuungwa mkono na wananchi Ili isalie madarakani! CCM inahitaji uwepo wa utii wa vyombo cya ulinzi na Usalama hasa jeshi la polisi Ili kibakie madarakani. Rejea kauli ya mwenda zake kuhusu uteuzi wa wakurugenzi (nikuteue, nikupe gari, nikupe mshahara) halafu umtangaze mpinzani ameshinda?

CCM imekua na utaratibu wa kutengeneza matatizo na Kisha kutatua Ili ionekane inawajibika hili alitahadharisha sana Mh Jk kwamba msitegemee nguvu ya Dola wakati wote. Hali kadhalika matumizi ya low political consciousness ya watanzania walio wengi Ili kuendelea kubaki madarakani.

Kulinganisha ushawishi wa chadema na ccm yakufaa Kwanza ujiulize Kwanini kilipata ushawishi na baadae ushawishi ukapotea. Ukweli ni kwamba sababu sio mambo yakiyomo ndani ya chadema Bali yanayotoka nje ya chadema ambayo ni mkono wa dola na sio kwamba CCM imeweza kukidhi matarajio ya watanzania walio wengi.

-Bado elimu tuliyo nayo ni elimu ya idadi na sio elimu Bora inayomsaidia mtanzania kukabiliana na changamoto za kimaisha akiwa ndani ya nchi au nje ya nchi.

Bado huduma za afya ni za gahrama ya Juu kulingana na hali ya maisha ya mtanzania wa kawaida kiuchumi. Uwepo wa vituo vya afya ni Jambo moja lakini upatikanaji wa huduma stahiki kama dawa na matibabu bado ni tatizo. Idadi ya matabibu na wahudumu wa afya bado ni ndogo, upatikanaji wa vifaa Tiba na dawa bado ni tatizo kubwa.

Usiitazame dar es salaam ukaiona Tanzania, bado huduma za usafiri wa uhakika kwa maeneo mengi ni tatizo kubwa hasa msimu wa mvua.

Upatikanaji wa maji Safi na Salama kwa uhakika ni tatizo sugu! Watawala wanazindua miradi ya maji lakini maji hutoka siku hiyo hiyo tu! Baada ya hapo maji hakuna, sasa hivi tunaingia Kwenye mgao wa maji ilihali nchi Ina rasilimali za kutosha kuhakikisha maji yanapatikana. Lakini wanasiasa wanaogelea Kwenye utajiri.

Mfumuko wa Bei unaochagizwa na kupanda kwa Bei za Mafuta (vyakula hasa nafakanhazishikiki) hapa tunatengeneza Taifa la watu wenye lishe duni kiasi kwamba akili zao zitadumaa! Licha ya kushuka kwa Bei za Mafuta hakuna government intervention kuhakikisha gharama za usafirishaji zinashuka Ili watu wapate angalau nafuu ya maisha.

Mawasiliano ndio kiungo muhimu Cha mawasiliano lakini hivi sasa kutumia data ni anasa, wakati data (bundles ) ni Mafuta ya watu kufanya Biashara kidijitali nje na ndani ya nchi! Ni sehemu mojawapo ya vijana kujiajiri lakini makampuni kila uchwao yanapandisha gaharama za data na hakuna government intervention!

Kwahiyo bwana Mwashambwa kama ulivyo mshamba jitahidi kutokuishindanisha ccm na chadema huku ukijua kwamba CCM kwa kutumia dola imeifunga chadema mikono isiwasemee wananchi ama bungeni au nje ya bunge na mwasisi wake alishatangulia hell!
Tumia muda mwingi kuieleza serikali Yako Ni mambo Gani ambayo inapaswa kuyaaadress Ili ikubalike!
Upinzani wa kutokuongea ni hatari kuliko wa kuongea!
________________
 
Hakuna chama Cha kuisumbuaa CCM nchi hii maana vyama vyote vimejikatia tamaa na kuandamwa na migogoro isiyo Keisha kutokana na ubadhirifu wa viongozi ndani ya vyama vya upinzani inayofanywa na viongozi wanaovitumia vyama Kama Saccos zao au miradi yao binafsi
Kwakua Uzi WAKO umelenga Chadema ni vyema utueleze hapa sisi tusiojua:
-migogoro ndani ya chadema ni ipi ambayo bila shaka yoyote imewagawa wananchi.
-Taarifa yoyote ya CAG inayoonesha ubadhirifu wa viongozi wake hali inavyofanya chadema kigawangike na kikose ushawishi kwa wanachama!
-Na mammlaka ya serikali yani tukianzia Bot pamoja na TRA ikiwemo pia msajili wa vyama vya kuweka na kukopa aliwahi kuisajili Chadema kama Saccos na wanachama wepi wanaweka na kukopa fedha huko Ili tuone namna Gani kilivyo chama Cha hovyo.
 
Toka 2015 nafasi ya Chadema ilichukuliwa na Magufuli.

Hawajawahi kuirejesha.
 
Mimi Ni Lucas Hebel Mwashambwa na mzalendo kweliii kweliii na Nina Imani kubwa Sana Na mama Samia na serikali yangu na sitachoka kuitetea
Wazazi WAKO walivyokua wanakusomesha ingawa uandishi WAKO bado unaonesha uchanga uliotopea hawakuwahi kuamini kwamba utakuja kuwa hivi:
-Maana halisi ya uzalendo ni kunipenda na kuitetea nchi Yako
-Mzalendo yeyote ni mwema Kweli daima wakati wote kwa maana ya makamilifu na mapungufu Ili kuwepo na marekebisho.
Umekaririshwa kwamba kukosoa ni usalifi na uhaini, na makosa wapaswa kuona wewe na sio kuoneshwa.
Kwa hiyo wewe sio mzalendo Ila ni msaka tonge na mlamba viatu kwa sababu unamsifia MTU (mama na kesho akija mwingine utamsahau mama KABISA)
Kiufupi ni kwamba kwa sababu siasa nayo ni ajira hasa kwa nchi maskini kama Tanzania unatafuta namna yoyote ya kuwa recognized na system.
Kwa bahati mbaya you are not a good analyzer not even a writer.
Nakushauri mtafute THADEI OLE MUSHI akufundishe namna Bora ya uandishi inayofurahisha watawala! Kwa mtindo huu huaminiki na hata mwenyekiti wa Tawi.
 
Kwakua Uzi WAKO umelenga Chadema ni vyema utueleze hapa sisi tusiojua:
-migogoro ndani ya chadema ni ipi ambayo bila shaka yoyote imewagawa wananchi.
-Taarifa yoyote ya CAG inayoonesha ubadhirifu wa viongozi wake hali inavyofanya chadema kigawangike na kikose ushawishi kwa wanachama!
-Na mammlaka ya serikali yani tukianzia Bot pamoja na TRA ikiwemo pia msajili wa vyama vya kuweka na kukopa aliwahi kuisajili Chadema kama Saccos na wanachama wepi wanaweka na kukopa fedha huko Ili tuone namna Gani kilivyo chama Cha hovyo.
Rejea migogoro ya chadema na wabunge wake wa Viti maalumu, Rejea migogoro kuanzia Enzi za Zitto kabwe Samsoni mwigamba kitila mkumbo mpaka wakati wa Dr Slaa, Rejea malalamiko ya akina Peter lijualikali juu ya udikteta uliopo chadema, Rejea juu ya migogoro inayoibuka kila mwanachama anapoonyesha Nia ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama Taifa, Rejea migogoro ya Bavicha namna walivyokuwa wakimsakama mch Peter msigwa mitandaoni Kama alivyofanya Daniel Naftari, Rejea migogoro Mbeya mjini Kati ya akina China wa China na kundi la mzee wa upako, migogoro Ni mingi Sana inayokuwa inatokana na uchu wa madaraka na ubadhirifu
 
Wazazi WAKO walivyokua wanakusomesha ingawa uandishi WAKO bado unaonesha uchanga uliotopea hawakuwahi kuamini kwamba utakuja kuwa hivi:
-Maana halisi ya uzalendo ni kunipenda na kuitetea nchi Yako
-Mzalendo yeyote ni mwema Kweli daima wakati wote kwa maana ya makamilifu na mapungufu Ili kuwepo na marekebisho.
Umekaririshwa kwamba kukosoa ni usalifi na uhaini, na makosa wapaswa kuona wewe na sio kuoneshwa.
Kwa hiyo wewe sio mzalendo Ila ni msaka tonge na mlamba viatu kwa sababu unamsifia MTU (mama na kesho akija mwingine utamsahau mama KABISA)
Kiufupi ni kwamba kwa sababu siasa nayo ni ajira hasa kwa nchi maskini kama Tanzania unatafuta namna yoyote ya kuwa recognized na system.
Kwa bahati mbaya you are not a good analyzer not even a writer.
Nakushauri mtafute THADEI OLE MUSHI akufundishe namna Bora ya uandishi inayofurahisha watawala! Kwa mtindo huu huaminiki na hata mwenyekiti wa Tawi.
Natumia Uhuru wangu katika kutoa maoni yangu binafsi na siyo kumfurahisha mtu, Mimi naongea ukweli kwa hoja za ukweli
 
Natumia Uhuru wangu katika kutoa maoni yangu binafsi na siyo kumfurahisha mtu, Mimi naongea ukweli kwa hoja za ukweli
Tunaokusoma ndio tunapima maandiko Yako na kutoa mrejesho! Narejea JF sio fb ni great thinkers platform! Na I must tell you this no frog that jumps in day light without a reason
 
Rejea migogoro ya chadema na wabunge wake wa Viti maalumu, Rejea migogoro kuanzia Enzi za Zitto kabwe Samsoni mwigamba kitila mkumbo mpaka wakati wa Dr Slaa, Rejea malalamiko ya akina Peter lijualikali juu ya udikteta uliopo chadema, Rejea juu ya migogoro inayoibuka kila mwanachama anapoonyesha Nia ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama Taifa, Rejea migogoro ya Bavicha namna walivyokuwa wakimsakama mch Peter msigwa mitandaoni Kama alivyofanya Daniel Naftari, Rejea migogoro Mbeya mjini Kati ya akina China wa China na kundi la mzee wa upako, migogoro Ni mingi Sana inayokuwa inatokana na uchu wa madaraka na ubadhirifu
Naomba usijibu haraka haraka hakuna tunapowahi kwa sasa! Jibu hoja Moja baada ya nyingine na uoneshe namna Gani zimesababisha mpasuko ndani ya chama Cha Chadema!
Na hoja nyingine nilizoweka katika hiyo post uzijibu!
 
Hakuna chama Cha kuisumbuaa CCM nchi hii maana vyama vyote vimejikatia tamaa na kuandamwa na migogoro isiyo Keisha kutokana na ubadhirifu wa viongozi ndani ya vyama vya upinzani inayofanywa na viongozi wanaovitumia vyama Kama Saccos zao au miradi yao binafsi

Ni kweli hakuna chama cha kuisumbua CCM maana hivyo vyama vingine havina Backup ya vyombo vya dola. Nje ya vyombo vya dola CCM ni takataka kama takataka nyingine. Hivyo hapa hujivunii ccm kama chama cha siasa, bali unajivunia vyombo vya dola.
 
Najivunia CCM kutokana na kuwa Ni chama kilichojikita katika kututumikia watanzania wanyonge
 
Naomba usijibu haraka haraka hakuna tunapowahi kwa sasa! Jibu hoja Moja baada ya nyingine na uoneshe namna Gani zimesababisha mpasuko ndani ya chama Cha Chadema!
Na hoja nyingine nilizoweka katika hiyo post uzijibu!
Kwani wewe hukuona mpasuko uliotokana na Dr slaa kuondoka? Hukuona hata John Mnyika alivyobakigi chamani Kama kimvuli tu? Hukuona watu Kama mzee mwanakijiji waliamua kuitupa mkono Chadema? Huoni Hadi leo chadema siyo Ile ya 2010-2015? Huoni Hadi leo chadema ilishapoteza ajenda yake iliyoitambulisha kwa watanzania na kuipa umaarufu kutokana na kupinga ufisadi na kuibua ufisadi? Lakini Leo haina nguvu hiyo kutokana na kuwa 2015 waliamua kuwabeba na kuwanadi wote waliowaita mafisadi na hivyo kuwakatisha Tamaa watanzania ambao wakaamua kuwapuuza chadema mpaka leo
 
Back
Top Bottom