CHADEMA yapoteza ushawishi mitaani. Sare zake hazivaliki

CHADEMA yapoteza ushawishi mitaani. Sare zake hazivaliki

Jibu hoja na usiulize maswali yasiyokua na majibu ambayo hata wewe huwezi kuyajibu maana ni ya kufikirika -nge- ni nadharia tunaangalia kilichopo sasa! Chama kilichofanyika baada ya migogoro ndani ya chadema hakipo. Chama kilichopo kutokana na mgogoro ndani ya CUF ni ACT, Chama kilichofanyika kutokana na kuvuta ndani ya CCM ni CCK
Nimeshakupa hayo maswali nataka unijibu siyo kuhamisha magoli na kuchimbia kwingine,Nijibu hayo maswali niliyokuuliza
 
Kwani unafikiri Kama Rais asipokuwa na weledi na umakini katika usimamaizi wa fedha za umma unaweza kuona miradi ikisimama na kukamilika? Mama yetu mpendwa mama Samia tunampongeza kwa usimamaizi mzuri wa fedha zetu watanzania
Na hukuna chuo cha kusomea urais! Hata wewe pamoja na u-mediocre wako unaweza kuwa Rais na watu wenye uelewa mdogo kuliko wewe wakakusifia!
Rais anatumiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi na miongozo yake.
Jiwe mlimsifia sana na mkataka atawale milele na mkamfananisha na malaika au Mungu! Na kwa namna ya uwasilishaji wako unamlinganisha mama na mtu x tuambie ni Nani na umetumia scales gani za rating
 
Kipindi Cha mama ndio kipindi ambacho wakulima wanafaidika na jasho lao na nguvu zao
Wewe ni mjinga (ashakumu Sio matusi) wapaswa kuelimishwa.
Unajificha mgongoni kwa wakulima, as if watu wameingia kwenye kilimo Juzi!
Sasa hivi nchi inaingia kwenye ukame hakuna intervention measures! Sijui mwakani utaongea Nini.
Wakati wa jiwe mazao ya nafakanyalipanda Bei jiwe akasema wakulima wauze Bei wanayotaka ilinwafaidike au umesahau?
Umesahau jinsi jiwe alivyokua anasisitiza watu walime hatatoa chakula?
Napenda kujua unamlinganisha mama na Nani?
Wakati wa JK kulikua na sera ya kilimo kwanza na usambazaji wa power tillers vijijini ikisimamiwa na mh pm Pinda au umesahau! Inatia kinyaa
 
Karibu mkuu kwa hoja , Tanzania itajengwa na sisi wenyewe, Tuendelee kumuunga mkono mama
Kimsingi na kiuhalisia wewe hujengi hoja Bali unasifia kwa gaharama ya watu wengine na unawaosifia hawaligani na unwabeza au kuwashutumu kwa sababu hawako katika level moja ya operation!

Mathalani huwezi kulinganisha Utendaji wa serikali na Chadema mana chadema haina serikali.
 
Serikali yoyote Ile duniani lazima ifanye juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa kundi nyonge linakuwa la kwanza kuguswa katika mipango yote ya kimaendeleo inayofanyika maana ndio kundi linalohitaji kupewa kipaombele ya kisera na kisheria ili kuwawezesha kukua kiuchumi, huku lile la juu likiwekewa mazingira mazuri ya kuhakikisha linaendelea kutoa mchango wake kwa jamii kupitia ulipaji wa Kodi na utoaji wa ajira kwa vijana,kazi hii ndio imekuwa ikifanywa na serikali ya CCM na ndio sababu ya Kuendelea kuaminika na kuungwa mkono na watanzania wote
Bado nakushauri kabla hujajibu kuwa na critical reading between the lines na ujibu hoja hapa hujajibu kile nilichouliza naomba rejea tena Kisha andika wala usiwe na haraka kihivyo Jenga mazingira ya kueleweka kuliko kuonekana kasuku! Maswali yangu ni mazuri sana kama ukiyajibu vyema

Je wajua Jiwe ambaye alikua mwenyekiti wa Ccm aliwahi kusema atahakikisha matajiri wataishi kama mashetani? Huoni kama unajipinga mwenyewe au alikua mwenyekiti wa chadema ambae aliamini katika uporaji wa kidola akiitumia ofisi ya dpp kuwapa matajiri za uhujumu uchumi huku akichukua fedha zao?
rejea alivyokua anafanya General Sabaya ambaye sasa anapambana na mahakama!
je hicho lilikua chama kipi au chama huwa kinabadili misingi ya uanZishwaji wake kila awamu!
 
Chadema haipo katika mioyo ya watanzania kwa Sasa ndio maana unaona haiungwi mkono katika azimio lolote lile au tamko lolote lile inalolitoa kwa watanzania
Sasa nakwambia, na wafikishie viongozi wako wa kitaifa, ni wakati wa ccm kuandaa chama mbadala wa ccm, hii itawasaidia Sana pale mtakapo pigwa chini na kutafuta nafasi ya kurudi Madarakani Kama wapinzani, na ieleweke nchi na Chama ambacho kimeunda serikali bila kutokuepo na chama pinzani imara ,jua iyo nchi imekufa ,

Wakati wa ccm Kama chama kuunda serikali tena haupo, naongea KWa ujasiri mkubwa
 
Sasa nakwambia, na wafikishie viongozi wako wa kitaifa, ni wakati wa ccm kuandaa chama mbadala wa ccm, hii itawasaidia Sana pale mtakapo pigwa chini na kutafuta nafasi ya kurudi Madarakani Kama wapinzani, na ieleweke nchi na Chama ambacho kimeunda serikali bila kutokuepo na chama pinzani imara ,jua iyo nchi imekufa ,

Wakati wa ccm Kama chama kuunda serikali tena haupo, naongea KWa ujasiri mkubwa
Hakuna chama chenye uwezo wa kuitoa Wala kuitikisa CCM hii ya mama Samia, mizizi ya CCM imefika hata usikoweza kufika wewe, Ni chama kilicho imara na kuimarika kila idara, Ni chama kilicho na viongozi wenye sifa za kiuongozi
 
Huu
Wewe ni mjinga (ashakumu Sio matusi) wapaswa kuelimishwa.
Unajificha mgongoni kwa wakulima, as if watu wameingia kwenye kilimo Juzi!
Sasa hivi nchi inaingia kwenye ukame hakuna intervention measures! Sijui mwakani utaongea Nini.
Wakati wa jiwe mazao ya nafakanyalipanda Bei jiwe akasema wakulima wauze Bei wanayotaka ilinwafaidike au umesahau?
Umesahau jinsi jiwe alivyokua anasisitiza watu walime hatatoa chakula?
Napenda kujua unamlinganisha mama na Nani?
Wakati wa JK kulikua na sera ya kilimo kwanza na usambazaji wa power tillers vijijini ikisimamiwa na mh pm Pinda au umesahau! Inatia kinyaa
Huu Ni uongozi wa mama Samia Suluhu Hassan
 
Hata mikutano ya hadhara ikianza bado Chadema Haina ushawishi wowote ule kwa sasa
ushawishi? yaonekana ni neno geni sana kwako?
hembu tuambie hapa ukisema ushawishi uanamaanisha nn? nini kimesababisha huo ushawishi ukapotea
 
Hakuna chama chenye uwezo wa kuitoa Wala kuitikisa CCM hii ya mama Samia, mizizi ya CCM imefika hata usikoweza kufika wewe, Ni chama kilicho imara na kuimarika kila idara, Ni chama kilicho na viongozi wenye sifa za kiuongozi
Nakwambia Sasa mtakuja kutana kitu kizito nyie ccm ,na mtakaa ndani mpaka mwezi bila kuoga nakwambia, Kuna mda wa mtawala dictator angamiza chama kama kinaonekana kuwa tishishio katika utawala wa chama kilichomadarakani KWa akili kubwa ila sio zile nyepesi ambazo mmekua mkitumia ccm,

Ni KWa bahati mbaya ccm ilishindwa mwanzo kabisa kumuweka mfukoni chadema, hii ni bahati mbaya Sana Sana KWa ccm na wanajua wakubwa wako that's

KILA uchaguzi ukimalizika katika makabidhiano pamoja na Mambo mengine ,ila yapo yale yakuonyesha Mambo ya kisiasa ,hii ni kitu muhim Sana, na ndo maana mwendazake alikuja na nguvu za ajabu akikisha analeta Umwamba, yako wapi?

Leo Chadema nataka nikwambie , FAM ni mstarabu ,mpole, Kuna vichwa vipo ndani ya chama ichi ,wakipewa kuwa wenyekiti may be mtakua mnaua KILA siku pitia watu wenu ambao mmewaingiza huko ila wanalipwa na uma,

Leo hata Mbowe anaongopa hata ingetokea kufika bei ya ccm kwamba ataanzia wapi ulaghai wake ,hii ndo maana ya nguvu ya umma,

Mpeni offer cash ya trion 5, Kama atakubali, KWa jinsi chadema ilivyosukwa leo ukichukua chako kesho unaamuka Kama mzoga huna Chako ndani ya chama, na utakutana na laana 300 kidogo,

Sasa wewe ndugu yangu na jirani yangu unakuja na vitu vyepesi eti ccm imejichimbia , haya ni mawazo mfu na hamkisaidii chama chenu, na hasara kubwa ni kwamba yule anae kuwa na mawazo tofauti ndani ya chama chenu yatampata ya kumpata Kama sio kufungwa.
Yani unamkuta mtu k
Lijali,anafamilia eti anajivunia kuwa na no ya mwenezi taifa, (Shaka),spika,pm ,vp , kinana, Chongolo) hao ni Mungu ? Na Kama sivyo tuwaiteje Hawa watu mnaoabudu Mambo haya,?

Binafsi katika Taifa Hili bila kujali mtu anatoka chama GANI ila akiwa na fikra pevu bila kujali twajuana namuona rafiki ila si yule wamihemuko
 
Inatia aibu Sana kwa kijana mwenzetu kuzungumzia ushawishi wa vyama na kuvaa nguo za vyama !!

Maisha yamebadilika Sana ,,Imani ya vijana na wananchi ju ya maisha bora na yenye uwiano sawa imepotea .

Hii yote imesababishwa na ccm ,ambapo utawala ulio pita uli amua kuwa surubu na hata kuwapoteza watu walio onekana hawaiungi mkono ccm ,hofu ilijengwa kwa wananchi ju ya kuikosoa ccm .

Nisi andike mengi ,Ila jua kuwa watu wanataabika na hali ngumu ya maisha hivyo kufikiria kuvaa Sare za vyama haina maana , watu wanapambana na hali za maisha hasa kipindi hiki ambacho maisha yapo ju,ukame ,na ukosefu wa ajira.
 
Hata mikutano ya hadhara ikianza bado Chadema Haina ushawishi wowote ule kwa sasa
Hakuna kitu kibaya kama kukosa uoga na aibu unakuwa kituko.
Hivi kama hakina ushawishi hao wanaokulipa buku 7 kwa siku wangehangaika hata kutumia pesa za walipa kodi kuunda kamati feki ya raisi ili kuwazuia kufanya mikutano ya siasa kinyume na katiba?
 
Hakuna kitu kibaya kama kukosa uoga na aibu unakuwa kituko.
Hivi kama hakina ushawishi hao wanaokulipa buku 7 kwa siku wangehangaika hata kutumia pesa za walipa kodi kuunda kamati feki ya raisi ili kuwazuia kufanya mikutano ya siasa kinyume na katiba?
Silipwi na mtu Mimi zaidi ya kutumia Uhuru kuwasilisha mawazo yangu
 
Ndugu zangu miaka kadhaa iliyopita hakika chama hiki kilijizolea umaarufu mkubwa Sana hasa kwa kundi la vijana, Vijana walijiona fahari Sana kujiita makamanda, vijana wengi hasa wa vyuo vikuu na vyuo vya Kati walikuwa mtaji mkubwa Sana wa chama hiki, Hakika vijana walikuwa na hamasa kubwa Sana na kuhamasika kujiunga na chadema.

Tulio kuwa CCM na kuweka Imani yetu kwa CCM kutokana na Sera zake na itikadi yake tulionekana Kana kwamba Ni vijana tuliopitwa na wakati, tulionekana Ni vijana wakizamani katika Zama mpya, Tulionekana Ni wazee katika umri wa ujana.

Nguo na magwanda ya Chadema yalivaliwa na vijana hao kwa mbwembwe Sana, Wana CCM wakawa wanaona aibu kuvaa sare na kupita nazo mitaani, Wana CCM waliona uoga kujitambusha UCCM wao katikati ya kundi maana ilikuwa unapata mashambulizi yasiyo ya kawaida.

Wana CCM wakawa Wana vaa tisheti ndani ya mashati ya mikono mirefu na kufunga vifungo Hadi shingoni utazani mtu anayetaka kujinyonga, kofia za chama zikawa hazivaliwi Sana maana wanachama waliogopa kuvuliwa kwa nguvu, kofia zikawa zinakunjwa na kufichwa, wanachama wakawa wanakwenda mikutanoni kupitia vichochoroni Hadi uwanjani na kila mtu kurudi kwa njia yake, Tukawa tunaishi utazani sisi ndio wapinzani na wapinzani ndio chama Tawala.

Asante CCM chama kikongwe chenye kila aina ya mbinu, chenye hadhina ya viongozi, chenye kujuwa historia yake,chenye kujuwa wapi kimetoka na wapi kimejikwaa na chenye kujisahihisha.kikaamua kurejea mezani kuangalia wapi kimejikwaa,wapi kiliwakosea watanzania,wapi kiliwaumiza watanzania,wapi kiliacha misingi yake,wapi hakikutenda haki,wapi kiliteleza,wapi kiliwapa kisogo wananchi, wakina Nani walikiangusha,walikifedhehesha,walikinyima kura,walikisaliti,walikipaka matope,waliokichafua,wakina Nani walikifanya kichukiwe na watanzania, Nini kilikifikisha hapo,mambo gani yalikipa doa chama chetu?

CCM ikajisahihisha na kurejea katika misingi yake, Misingi ya kuwatumikia watanzania wanyonge, misingi yakutokutekwa nyara na wachache, misingi ya kuwa chama kiongozi,misingi ya kutenda haki katika michakato yake ya ndani,misingi ya kutanguliza mbele Taifa letu, misingi ya kusikilizana na kushirikiana,misingi ya kuhakikisha kuwa chama kinakuwa Sauti ya wanyonge,misingi ya kuhakikisha chama kinakuwa masikio na mdomo wa watanzania wanyonge,Misingi ya kuwapa nafasi vijana, misingi ya kukiweka chama mikononi mwa wanachama,Misingi ya kusema kweli na kuondoa ufitini

Hatimaye watanzania wamerejesha matumaini ndani ya CCM, hatimaye watanzania wamesamehe yote yaliyopita, hatimaye watanzania wametambua mzazi Ni mzazi tu ,Hatimaye watanzania wameona namna CCM inavyowatumikia kwa upendo na bidii kubwa, wameona namna CCM na serikali yake inavyogusa maisha yao, hatimaye watanzania wameona namna serikali ya CCM inavyokesha ikifanya kazi, hatimaye wameona namna serikali ya CCM ilivyo sikivu na makini katika kuwatumikia.

Kibao kimegeuka, Sasa chadema haieleweki Wala haisikilizwi, haifuatiliwi Wala haipewi masikio na watanzania, chadema kwa Sasa haina ngome ya aina yoyote Ile, Haina ushawishi kwa watanzania, Haina mizizi yoyote Ile, imebaki imening'inia hewani tu, Haina matumaini ya aina yoyote maana hakuna wa kuipa matumaini.

Wanachama wake wachache waliobakia wanaogopa kuvaa hata Sare zake, wanaogopa hata kusema juu ya chama Chao, wanaogopa hata kutetea chama Chao maana hakuna wa kuwasikiliza na hawaelewi watetee Nini, wenye akili walishawakimibia,walishawapa mkono wa kwa heri, walishabeba akili zao na mikakati yao, walishaondoka na ajenda zao,kimebaki Ni chama kisicho na dira Wala muelekeo, kimebaki Ni chama chenye safu ya uongozi iliyojikatia Tamaa na isiyotoa matumaini hata kwa wanachama wake yenyewe na haina ushawishi kwa watanzania, Hakina viongozi wenye mvuto wa kihoja, hawana maono Wala misimamo ya aina yoyote Ile na hawaeleweki wanasimamia Nini na wanapigania nini.

Chadema kimebaki Ni chama ambacho hakina uwezo wa kuandaa hata ilani ya chama, hakina watu wenye kufanya utafiti wa kisera , Kimebaki Ni chama kilichojaa viongozi wenye mihemuko tu, Kwa heri Chadema wakati si wako Tena na haupo upande wako Tena, Karibuni CCM Tuijenge nchi yetu, Vijana wenye kujitambua wamesharejea ccm na Kuendelea na kazi ya kuijenga nchi yetu.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
CCM YENYEWE MAMBO BAMBAM

SUBIRI MIKUTANO YAA ADHARA

UTASIKIA MSUMARI UKIKUINGIA VYEMA KABISA
 
Back
Top Bottom