Kwani wewe hukuona mpasuko uliotokana na Dr slaa kuondoka? Hukuona hata John Mnyika alivyobakigi chamani Kama kimvuli tu? Hukuona watu Kama mzee mwanakijiji waliamua kuitupa mkono Chadema? Huoni Hadi leo chadema siyo Ile ya 2010-2015? Huoni Hadi leo chadema ilishapoteza ajenda yake iliyoitambulisha kwa watanzania na kuipa umaarufu kutokana na kupinga ufisadi na kuibua ufisadi? Lakini Leo haina nguvu hiyo kutokana na kuwa 2015 waliamua kuwabeba na kuwanadi wote waliowaita mafisadi na hivyo kuwakatisha Tamaa watanzania ambao wakaamua kuwapuuza chadema mpaka leo
Mpaka sasa naamini Chadema haijapasuka kwa sababu hakuna chama kilichoundwa kutokana na chadema Ila Kuna watu wachache wameondoka chadema kutokana na kutoelewana katika baadhi ya mambo.
Mnyika kubaki kama kivuli ndani ya chadema nadhani hayo ni maoni Yako kwa sababu wewe sio mwanachama wa chadema au miongozo ambae unaweza kutuambia kwamba amebaki kama kivuli na hatimizi majikumu yake ipasavyo. Kuondoka kwa wanachama ni Jambo la kawaida kama walivyoondoka kina membe ccm na wengine wengi!
Naomba sasa nijibu hoja hizi:
-Ni lini kumetokea malalamiko Rasmi ya ubadhirifu wa fedha za chadema ambapo wa kuthibitisha Hilo ni CAG, na namna Gani ubadhirifu huo umechangia katika kudhoofisha chama.
-Ni lini ambapo BOT TRA na mammlaka nyingine ziliwahi kuisajili CHADEMA kuwa chama Cha kuweka na kukopa na wanachama wake wanaweka na kukopa kwa utaratibu Gani?
-kuhusu kitu kuwakuta wanaogombea nafasi ndani ya chama, utueleze ni lini Msajili wa vyama vya siasa alishawahi kukichulia hatua chama hicho kwa kukiuka misingi ya demokrasia ya nchi, ya chama na kanuni za uendeshaji wa vyama vya siasa pamoja na sheria zake!
-mwalimu alikaa madarakani miaka 27 na aliendelea kuwa mwenyekiti wa chama kwa miaka mitano baadae! (32) mfumo hii ccm iliona unafaa kwa sababu Rais akiwa mwenyekiti wa Chama ni rahisi matakwa na matarajio ya chama kufikiwa na hata Rais akikosea chama hakiwezi kumwajibisha. Kwahiyo uchaguzi wa nchi unaenda sanjari na uchaguzi wa chama!
Hii umeifanya ccm kudanganya umma kwamba IPO demokrasia wakichagiza na kupokezana vijiti kwa mwenyekiti wakati sio Kweli! Chama kinachofanya ni kupitisha jina la mwenyekiti na sio kuchagua mwenyekiti,.
Umeinagalia chadema sana sasa tuambie hapa bila kupepesa maandishi
Mrema Amekua mwenyekiti wa chama kwa muda Gani
Shibuda, Mbatia? Na wengine kama Rungwe?