Hii ni kikasuku kweli kweli.
Yaani kwa tafsiri nyingine; ukizingatia sifa ya kuwa Ubilionea ni ngeni, sambamba na kuwa Ukiitwa bilionea unafananishwa na kuwa umeshafanya talaka na tamaduni zako/zenu na kukumbatia tamaduni za watu wanaojiita bilionea na hivyo kufanya swali hili kuwa kama .....
"Umekubali kuitwa billionea, je unakubali kuacha/kutelekeza tamaduni zako?"
au
'Toka umekubali kuitwa bilionea ni Vyakula gani kwenye tamaduni yenu umeachana navyo?"
..... kumbukeni huko nyuma Tanzania tulikuwa na Mabilionea(kwa lugha ya kigeni) ila waliitwa Wafanyabiashara Maarufu.!
Isitoshe nishakula vyakula na Wafanyabiashara maarufu wengi tu(Mabilionea sasa kwa lugha ya kigeni) na asikudanganye mtu.....nimelishwa Chai na Mihogo Asubuhi, au Uji wa Ulezi ikifuatiwa na.....mchana- tulikula Ugali na mboga ya Kisamvu chenye mbaazi na samaki wa kukaanga, siku nyingine Ugali Dagaa na mazagazaga mengine. Au Ugali mlenda na nyama ya kuchemsha na kitunguu na nyanya ya kutupiwa-yaani nyanya ndio zinakuwa zinaelea kwenye chungu badaala ya mafuta! We acha.
Usiku Wali maharage, nyama ya Kuchoma na kisusio! Na mchunga pembeni!
kinachonishangaza, ni kuona Ulimbukeni uliotokea hivi karibuni.
Ati mtu anataka kula soseji asubuhi, na baked beasn-wakati ukimwambia twende tunywe supu ya Utumbo ati anashika pua! Kumbuka soseji nyingi huwa ni mchanganyiko wa utumbo na vitu vingine, tena basi, huko Ulaya, ni mchanganyiko wa Utumbo wa Kuku, Nguruwe, Na Ng'ombe au Mbuzi.
Ati, Baked beans! Wakati ukila maharage na ubwabwa asubuhi na supu lako la utumbo ni Afya tele tu
Afrika kiboko kweli kweli