Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Chakula gani ulikula mara moja na kwa mara ya kwanza hadi leo hutaki tena kukila?

Njugumawe si mboga.
Watu wa bara wana visa.
Mimi mwenyewe nikikuta umepika mboga sili.
Njugu ni mbogq kabisa..

Sema zisiwe na kale kakiini na ganda.. hivyo viwili ndivyo vyenye harufu. Ukivitoa .. inakuwa kitu safi mno.. zaidi hata ya dengu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Njugumawe si mboga.
Watu wa bara wana visa.
Mimi mwenyewe nikikuta umepika mboga sili.
Sasa tunapishana mimi njugu mawe nazipenda hasa pale zinapoungwa na nazi aisee ule na wali
 
Ni vingi sikumbuki jina ila kwa Sasa siku zinavyozid kwenda mlenda umeanza kunishinda si pe ndi
 
Mambo vipi wanaJF natumai mko poa. Kwenye misosi kuna kuwa na kile chakula una hamu nacho au tu umekuta sehemu kimepikwa kwasababu hujawahi kula unaamua kula huo msosi kwa mara ya kwanza lakini chakula hicho kina kushinda kabisa hata kukupelekea kujisikia vibaya.

Mimi miaka ya nyuma nilikuwa nasikiaga kuhusu supu ya kongoro siku na mimi nikaamua nijue ikovipi hiyo supu nikaenda sehemu nzuri tu nikaulizia nikaambiwa ipo basi nikaletewa pale nikaanza kuipiga lakini kidogo tu nilikula kama vipande viwili tu vya ile nyama nikajisikia kuchefuchefu vibaya sana hata hiyo nyama kumeza haimezeki nikaacha supu karibia yote pale hadi leo hii sitaki tena kusikia kuhusu hiyo supu

Nyingine hii ilikuwa ni juisi ile ya rozela nilikuta imetengenezwa sehemu nikanywa glasi moja ilikuwa na ladha nzuri tu lakini baada ya hapo nilijisikia vibaya sana kama kizunguzungu mara kama mwili unataka ku vibrate mara jasho linatoka japo kulikuwa na feni yaani ilikuwa ni shida mpaka leo nikiiona hiyo juisi naipitia mbali kabisa. Hata juisi ya miwa ilinishinda kabisa ni bora nile muwa kama muwa

Vipi kwa upande wenu wadau ni kitu gani ulikula lakini baada ya hapo hutaki tena kukila.
Chumvini
Sina tena hamu nako
 
3.KONGORO

natamanigi sana nikiona mtu anakula kongoro anahangaika na bomba lile,huku akpga kijiko cha supu,nahisi anakula kitu kitamu sana,siku moja isiyo na jina namimi nikaitsha kongoro,wapendwa hamna siku hela yangu iliniuma kiasi kwamba nikatamani kulia kama ile siku,maana ki ukweli lile kongoro ile nimeweka mdomoni tu nilirudsha chenchi,ikabd nisingizie naumwa,nikatoka eneo lile nikabadlisha kiwanja nikarudi kwenye supu zetu za ng'ombe.
Hii hata Mimi ilinikuta
Siji rudia tena kununua hii kitu maana ni mbaya mno
 
Back
Top Bottom