Chalamila: Akija Rais Samia mje na mabango hata ya matusi. Wananchi Washangilia kufukuzwa kwake

Chalamila: Akija Rais Samia mje na mabango hata ya matusi. Wananchi Washangilia kufukuzwa kwake

Mapema saana alipokelewa na gang la wahuni waliofungiwa baa ya the cask best ya kigwa na kuifungua baa hiyo kero kwa uasherati na makelele na maganstars wa mujini na kuamrisha watu wanywe mapombe
 
Hawa watakuwa wanaongelea Rehema Chalamila maarufu kama Ray C
 
KUNA MABANGO YA AINA TATU, PAMOJA NA YALE YA KAKA CHALAMILA.

Na: Philipo Mwakibinga.

Kuna aina tatu za mabango ikiwa ni pamoja na yale ya ndugu yangu kaka Chalamila, yanayoandikwa wakati wa mapokezi ya kiongozi anapofika pahala fulani kama ifuatavyo;
Mosi, ni mabango yanayoandikwa kwa lengo la kutoa pongezi na shukrani kwa kiongozi fulani. Haya humtia moyo kiongozi na kumpa haki yake ya kupewa hasante kwa kazi anayofanya.

Pili, ni mabango yenye kutoa kero, malalamiko na kila aina ya lawama mbalimbali mbele ya kiongozi husika. Haya hukumbusha na kuweka wazi baadhi ya mambo yanayoendelea na yanahitaji suluhisho fulani.

Tatu ni yale aliyohimiza kaka Chalamila mbele ya Waandishi wa habari, haya ni yale yenye matusi. Haya hujaa kashfa, kejeli na dhihaka kwa kiongozi fulani. Mabango haya huambatana na picha za kejeli na dhihaka wakati fulani. Haya mabango hutia hasira sana na pengine hudhalilisha na kushusha hadhi ya kiongozi. Mabango haya huchochea chuki na yamekua siyo suluhisho katika matatizo bali huleta mfarakano.

MSIMAMO WA MH RAIS DHIDI YA MABANGO.
Nakumbuka kuna wakati Mh Rais aliweka wazi msimamo wake juu ya mabango katika ziara zake kila atakapopita. Alihimiza juu ya wateule wake kushughulikia matatizo na kero za Wananchi huko alikowapangia na kuwatahadharisha kuwa kila atakapokuta bango hata kama ni moja basi mteule huyo ataondoka haraka sana.

Sasa anapotokea kiongozi katika wale aliowakataza juu ya mabango, yeye akahamasisha mabango tena kwenda mbali zaidi na kuhitaji YALE YA MATUSI ni dhahiri kuwa kunatatizo mahali.

Sitaki kuhusisha utenguzi wa nafasi aliyokuwanayo kaka Chalamila na mabango lahasha! Bali nahusisha katazo la mabango lililotolewa na Mteuzi dhidi ya uhamasishaji wa mabango tena ya Matusi uliofanywa na Mteuliwa.

Tuheshimu Mamlaka na tusisite kukataa teuzi kama hatutaki kulikokukubali kisha tukaendakufanya fujo za rejareja.

TUNAMPA KAZI MTEUAJI HUKU TUKIPOTEZA IMANI YAKE KWETU KWA SIKU SIJAZO.
 
Kama Taifa tumefika sehemu mbaya, tunashangilia vifo, watu kutumbuliwa, wakipata magonjwa, matatizo.

Utu, ubinadamu,ujirani, kusameheana vimepotea kwenye jamii. Kilichobaki ni chuki, wivu, kuombea wengine matatizo, matusi, dhihaka, kejeli, kutafuta umaarufu mitandaoni kwa gharama yoyote ile.

Mitandao tungeweza kuitumia vizuri, kukosoa kwa staha (constructive criticism) networking, business deal, advertising our product, kuwakutanishi wateja na wauzaji, kushirikiana.
 
Unategemea nyumbu wawe na constructive criticism? Aliyewapa jina la nyumbu alifikiria sana.
 
Back
Top Bottom