Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Sipo hapa kujadili sababu za watu kutungishana mimba.
Hoja yangu ni kwenye uwezekano wa watu kukosa elfu 50. Na pia, uzembe wa serikali kushindwa kufikisha huduma za afya ipaswavyo.

___

Kuhusu hoja yako ya sababu za masikini kuzaliana, tafiti mwenyeweni kwa nini hata katika nchi zenye vita ama wakimbizi wanaendeleana kupeana mimba hata katikati ya masaibu.
 
Unafikiri mtu anayekosa beseni na glove anaweza kuwa na ufahamu wa maswala ya BIMA .?


Kauli za viongozi zinafikirisha.
 
Mkuu ukiona mtu kashindwa kuweka akiba ujue ya kuwa huyo matumizi yake ni makubwa kuliko kipato chake. Imagine mtu uchumi wake haueleweki halafu anampa mwanamke mimba hapo obviously matumizi yataongezeka matokeo yake mtu anakuwa masikini wa kutupwa. Na ukichunguza masikini wengi wana idadi kubwa ya watoto ambao wanashindwa kuwahandle. Ukitaka kukwepa umasikini hakikisha kipato chako ni kikubwa kuliko matumizi.
 
Naona umeandika vitu usivyovijua
 
Trump kiongozi wa Afrika?
Sio kila muda anatakiwa kuongea Maneno ya Busara
Unazidi kuonyesha uboya wako. Kwa hiyo Trump ndiyo kipimo cha namna viongozi wanavyotakiwa kuzungumza? Kwa sababu Trump ana kauli mbaya basi ni halali wengine kufanya hivyo? Kwanza ujue Trump hasemi vibaya kuhusu raia wake.
 
Hiyo bima kwa sasa haipo tena wameshaifuta
 
Kuzaa ni mipango
laZima ujue Kuna mahitaji inatakiwa kuwa nayo ili kiumbe kizaliwe
Serikali tunailaumu Kwa upande wake
Lakini tunawalaumu wazazi kukosa kujiandaa Kwa ajili ya mama kujifungua
 
Huduma kwa mama mjamzito ni bure, Serikali kama haiwezi iseme. Hadi huduma za mama na mtoto zinawashinda, aibu iliyoje.
 
Siko mbali nawe...

Kuna watu wanafanya kazi DSM mshahara wa siku ni elfu sita. Hata akijibana vipi lazima matumizi yawe makubwa kuliko kipato. Pia, kuna kundi la watu wasio na ajira. Wanaishi kwa kudura tu, wakipata wanakula wakikosa wanalala.
___
Wanafahamu kuwa maisha yao ni magumu na watoto watateseka lakini hawawezi kuacha kuzaliana.

Kwanza, wana imani kuwa kila mtoto huja na sahani yake.
Pili, raha pekee ya masikini ni ngono.
Tatu, kuzaliana ni ASILI. Haijalishi kiumbe hai yuko katika mazingira gani, akipata nafasi ya kuzaa atazaa tu. Ndiyo maana licha ya mabomu ya Gaza lakini watoto wanazaliwa kila leo.
____
Muhimu ni serikali kuweka vizuri huduma zake.
 
Kuzaa ni mipango
laZima ujue Kuna mahitaji inatakiwa kuwa nayo ili kiumbe kizaliwe
Serikali tunailaumu Kwa upande wake
Lakini tunawalaumu wazazi kukosa kujiandaa Kwa ajili ya mama kujifungua
Kuna watu wanajipanga lakini kuna circumstances zinawaharibia. Na ni rahisi kuharibikiwa kwa kuwa vipato vyao vya uhakika; uchumi wa nchi hauko stable.

Sasa ili hayo yote yasitokee, serikali isinunue magoli ya Simba na Yanga, ipeleke gloves kwenye hospitali.
 
Huduma kwa mama mjamzito ni bure, Serikali kama haiwezi iseme. Hadi huduma za mama na mtoto zinawashinda, aibu iliyoje.
Serikali inunue nepi ya mwanao, blanket, besen, gloves, ndio, kanga, taulo
Kwani wewe baba ni marehemu
Kwanini mnapenda dezo
 
Serikali inunue vifaa beseni, gloves, ndio, blanket, net, vyakula lishe vya mzazi, mwanvuli, chandarua n. K
Kwanini mnapenda dezo
Hospital unakuta Dokta, wauguzi, wakunga, majengo, vitanda n
K
Unaombwa kuchangia unasema we masikini?
 
Kama angelijibu aende kwa wakunga wa kienyeji badala ya mumeo si ujumbe ungefika? Nani angelaumu wakati mume hakufanya maandalizi
 

Ndio maana kuna Bima Mkuu.
Kata Bima ili kujihami na hizo circumstances
 
Watu wanataka bure tu kila kitu!
Yani hata wakipeana mimba kwa starehe zao wanataka serikali iwahudumie bure!
Nina Bima ya Assemble lkn kipindi wife anaenda kujifungua tulikuta hizo zana hazipo Bahati nzuri nilikuwa nimeshajiandaa!! Kuna shida sana hospital za serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…