Chama cha ACT - Wazalendo chajiondoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Ni bahati mbaya sana kwamba lugha hii ndio inaanza kuwa kawaida yetu, na muda si muda, itazoeleka.

Serikali wao wanaamini kwa kuwa wana vyenzo zote, hawawezi kujisumbua kwa kuzitafakari kauli kama hizi. Wanachojua wao ni kwamba 'hawajaribiwi', hakuna mwenye uthubutu/ujasiri wa kuhoji utashi wao. Waziri Lugola shasikika akitamka hata kabla ya kusikia maneno kama haya toka kwa vyama vya upinzani. Maana yake ni kwamba wapo tayari kupambana.

Binaadam sio ng'ombe au mfugo unaoweza kuamua lolote juu yake. Hawa viongozi serikalini ni mhimu watambue hilo na waheshimu haki za wananchi waliowaweka madarakani.

Wananchi hawa ndio waliotumia haki yao kuwaweka madarakani; sasa wanatumia nafasi hiyo kuwanyima haki hiyo hiyo kuwaondoa madarakani? Wataweza kweli?
 
Kufuatia hujuma za kila aina zilizofanywa na serikali ya ccm dhidi ya vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, chama cha Chadema kiliamua kujitoa na kutoshiriki uchaguzi huo haramu ili kutouhalalisha uonekane ni uchaguzi halali. Wiki hii niliandika nyuzi tatu 1.Chadema wamekwepa mtego wa kuwa wasaliti wa watanzania. Je Zitto Kabwe na Act yake wataukwepa huu mtego Au ndio tutaijua rangi halisi ya Zitto. 2.Vyama vya upinzani vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni wasaliti wa watanzania. 3.Wapinzani watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni wasaliti wa watanzania. Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Zitto Kabwe na Act Wazalendo yake kwa uamuzi mgumu na busara waliouchukua . Laiti Zitto Kabwe na Act Wazalendo yake wangeshiriki watanzania tusingewaelewa, yaani kwa figisu zote hizo, hila, hujuma unashiriki uchaguzi huu ili upate nini? Maana mpaka matokeo yameshapangwa. Mungu akubaliki sana Zitto na viongozi wenzako ili tupambane pamoja kuikomboa hii nchi toka mikononi mwa Bahima empire.Naomba huu uzi usiunganishwe.
 
Kususa nako kuna kanuni zake, wewe ukisusa, wenzio twala.
.
P
 
MUVI ipo mwishoni saivi staring CCM ,ndiyo anaenda kukomboa majimbo take
Ndo ndindi
 
Vingine haviliki.
Achana na haki za watu mkuu. Huwa haziombwi. Ipo siku watazidai.
Haya sio mambo ya kushabikia hata kidogo.
Mambo ya kugusa jamii moja kwa moja ni ya kuyaogopa kabisa
 
Pascal Mayalla ifikie pahali tuukubali ukweli...wewe unaona haya yaliyotokea ni mazuri?
Kwa nini chama kiogope ushindani huru?
Maaana yake chama hakijiamini.fujo zilizofanywa safari hii ni aibu kubwa..
Pascal hili si swala la kulichukulia juu juu ujue athari zake ni kubwa mno na huenda zikadumu hadi 2025.
Niseme tu kama ni amani ya nchi hii watakaoivuruga ni hiki hiki chama chenye nguvu.
 
Tunaunga mkono juhudi ya serikali ya awamu yatano chini ya uongozi wa daktari kuwezesha Samata kuifunga goli livapuuli
 
Tunaunga mkono juhudi ya serikali ya awamu yatano chini ya uongozi wa daktari kuwezesha Samata kuifunga goli livapuuli
....
....Mkuu umevunja bendi huku watu WAMETAWANYIKA ...hahahhahaaa
 
Ipitishwe sheria

Chama kikisusia Uchaguzi kinafutwa kabisa
Pitisheni sheria haraka mfute vyama vyote vya upinzani,ibaki ccm itawale milele hata mbinguni mkatawale pia.
 
Kwa wale wenye upeo wa kuona parefu hususani kwenye mambo ya kisiasa,naomba kuwauliza nini hatima ya vyama vya upinzani kujitoa katika chaguzi kama hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…