Naunga mkno kuanzisha hicho chama kitakachokijikita kutatua kero za wananchi kwa dhati, kupambana na rushwa kwa vitendo, kuunganisha umoja wa watanzania bila kujali rangi, itikadi, eneo analotoka, dini, kabila au jinsia.
Kusisitiza kujitegemea sio misaa na mikopo kutoka nje yenye lengo la kunufaisha wenye nguvu za kiuchumi na kulinda mamlaka ya nchi
Kusikiliza kero za wananchi, kutafuta suluhisho kwa kuzingatia mazingira na tamaduni za nchi
Kuboresha maono ya ujenzi wa nchi kupitia falsafa za Nyerere na Mwinyi ndio itazaa umoja halisi kwa maslahi ya wananchi
Kuwa tayari kuandaa utaratibu wa marekebisho ya katiba na sheria za utendaji ili kumpa haki na mamlaka halisi mwananchi pindi anapokosewa kwa kuvunjwa ahadi za kisera
Kuwa tayari kuandaa mpango wa kuabdili mfumo wa kipolisi uliorithiriwa kutoka kwa wakoloni ili uendane na matakwa ya nchi kuhusu ulinzi wa kweli wa mali na maisha ya watu
*Mimi ningependekeza kiwe kiitwe "Chama cha Umoja, Haki na Uzalendo Tanzania-CHAUHUTA"
CCM kwa sasa hakifai kabisa kupewa dhamana ya kitu chochote kile