CHAN Finals: Live from Ivory Coast

CHAN Finals: Live from Ivory Coast

Kuanzia kesho huko Bongo jina linabadilika na wataanza kuitwa JK BOYZ .

Hilo ndilo huwa linanikera eti wakishindwa Taifa Stars ,wakishinda JK boyz, hatuna kitu kinachotuunganisha kama Taifa , ila kila mahali ni siasa tuu.
 
JF bana inaboa sometimes......sasa iko kwenye siasa........kulikuwa hamna haja ya kuweka majukwaa mengine basi.....
 
Sasa na wewe mkuu issue ni breaking news au hii thread kuwa hapa?

Halafu inashangaza mtu unapinga kitu at the same time unafanya kitu hicho hicho.Unapinga thread kuwa hapa at the same time unasema "kwa habari zaidi ya yaliyojiri Gonga hapa " halafu unarudi kulekule.Duh,kubisha kwingine noma,unoko!

Thread imeshaunganishwa mazee.

Hapa ndipo tunaposhangilia ushindi wa Taifa Stars, sio Jukwaa la Siasa.
 
watanzania bwana, hii inadhihirisha, kuna watu wanapenda sana hii inchi iendelee kurubuniwa na kuibiwa mabilioni ya wananchi ili mradi wapate sababu ya kuongea siasa. ushindi wa stars is a true test kwa washabiki wa siasa ila wasioitakia mema nchi. TUBADILIKE JAMANI.......... leo ni kushangilia, kesho tutaendelea na hizo EPA, BOT, DC NA BAKORA ZAKE, NA AKINA LIYUMBA. Stars oyeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
wana JF, kama kumbu kumbu zangu zipo saya. Nadhani huu utakua ndiyo first major Win in continental tournaments... Mwaka 80 kule Nigeria tuliambulia sare na vipigo tu. its history.........

Ingekuwa haya ni mashindano ya AFCON, ningekubaliana na wewe, ila hii CHAN ni michezo michezo ya kombe la "mbuzi au mchele", wachezaji wa kimataifa hamna humu hawa ni local players tu kwenye nchi zao
 
Ingekuwa haya ni mashindano ya AFCON, ningekubaliana na wewe, ila hii CHAN ni michezo michezo ya kombe la "mbuzi au mchele", wachezaji wa kimataifa hamna humu hawa ni local players tu kwenye nchi zao

Ndo maana hakuana mchezaji wa kimataifa (ni Local players)........ ila hao wote international players waliaanza kua local kwanza. Everything has a beginning, mfano KOLO TOURE ametoka Asec Mimosas kwenda Arsenal kwa Pound 500,000/=
 
ukikaa sana majuu akili zenu zinakuwa kama bata......

.....kwani ivory coast walikuwa 7 uwanjani?

......wewe ianekana huu mshabiki hujui soka na kama sikosei umeanza kujua soka enzi hizi za DSTV na timu yako itakuwa ama liverpool ama chelsea.....

Sasa majuu na DSTV vinaingilianaje? Dogo ukitaka shule ya soka nijulishe tu nikushushie, nimecheza mpira kabla dingi yako hajapata hata wazo la kumtokea maza wako, na kwa taarifa tu naifukuzia badge ya FIFA!
Haya mashindano ya CHAN yananikumbusha enzi hizo tukicheza chandimu bush, kwa kuwa wengi tulikuwa hatuna viatu- wachache waliokuwa wanatoka familia bora tulikuwa tunawakomalia wavue iatu vyao la sivyo hakuna kucheza. Utakuwa ni uvivu wa kufikiri kama huoni kwamba hapa ni kama Tanzania (na nchi nyingine zote zisizokuwa na wachezaji wenye majina ulaya) inapigana na mpinzani ambaye amefungwa mkono mmoja huku yenyewe ikitumia viungo vyote, jiulize itakuwaje jamaa akifunguliwa mkono wa pili? Usiangalie mambo juu juu. Sawa ni ushindi lakini tufahamu ya kwamba labda tulikuwa tunacheza na timu C kama sio D ya Ivory Coast, na tulifungwa na timu C ya Senegal- na kuna watu kama nyie wanaodai wanaujua mpira na wanaona hiki ni kitu cha kukeshea bar! Kuna improvement but am not over the moon. Ikifika time ya World Cup au African nations qualifiers hao wasenegal na Ivorians watawaleta wataalamu wao walioko huko Chelsea, Madrid na Milan kama kawaida tu.
 
Hata wanazi wa liver leo tumekamua jamani, hata walipokuwepo kina etoo, tulionyesha tunaweza kwa hiyo Kana-ka-nsungu kubali tu tunajitahidi, kuwa mzalendo kidogo kaka

Haya mashindano ni mazoezi tu kwa timu ya Taifa, nitafurahi tuki qualify for African Nations and World Cup. Inanisikitisha kuona our first 11 ina struggle na kushinda kwa kagoli kamoja tu against team D ya Ivory Coast.
 
Watu wengine bwana mnasisitiza tusinhangilie leo tusubiri Jumamosi Usipofika.
Furahia vitu kadri vinavyokuja ndio busara. Mafanikio madogo ndio yanayokupa nguvu ya kuthubutu makubwa. Na kwa mwenye busara mafanikio yoyote anajipongeza. Taifa starz oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!! Tuserebuke mla mla leo mla jana na kesho kala nini?
 
Jana walau Wabongo tulipata faraja Baada ya Mrisho Ngasa kufunga bao lililowazamisha Ivory Coast na kutupatia pointi tatu. Sasa Kazi ni namna ya Kuwaua Wazambia kwani bila hivyo hakitaeleweka kwetu. Maximo Jiandaeni vema. Kila lakheri
 
Ahsanteni vijana kwa kazi nzuri na kubwa mlioifanya jana.
Kazen but na mjitume mara mbilizaidi ya jana ktk mechi ya jumamosi ijayo dhidi ya zambia.

All the best Starz
 
Haya mashindano timu karibu zote ni vibonde ile game ya kwanza tulifungwa kwa sababu ya woga wa mashindano,naamini hata sisi tunaweza kuchukua hili kombe hadi sasa sijaona timu ya kutisha
 
Utakuwa ni uvivu wa kufikiri kama huoni kwamba hapa ni kama Tanzania (na nchi nyingine zote zisizokuwa na wachezaji wenye majina ulaya) inapigana na mpinzani ambaye amefungwa mkono mmoja huku yenyewe ikitumia viungo vyote, jiulize itakuwaje jamaa akifunguliwa mkono wa pili? Usiangalie mambo juu juu. Sawa ni ushindi lakini tufahamu ya kwamba labda tulikuwa tunacheza na timu C kama sio D ya Ivory Coast, na tulifungwa na timu C ya Senegal- na kuna watu kama nyie wanaodai wanaujua mpira na wanaona hiki ni kitu cha kukeshea bar! Kuna improvement but am not over the moon. Ikifika time ya World Cup au African nations qualifiers hao wasenegal na Ivorians watawaleta wataalamu wao walioko huko Chelsea, Madrid na Milan kama kawaida tu.
Kijana hujui soka weye.....unaonekana ni limbukeni wa soka la majuu......ndio maana nikakuambia umeanza kuangalia soka juzi juzi DSTV ilipoingia........nachukia mijitu ya namna hii yaani yenyewe soka eti lipo ulaya tu na vitumi vyao uchwara ass nal atal....

......ungekuwa unajua soka ungeangalia viwango kijana......mcheza kama Ngassa ana kiwango cha juu sana huwezi kumlinganisha na bito drogba......

.......najua watu type yako hata tanzania leo ikichukua world cup mtasema aah haikucheza na Brazili...ingekutana na England nusu fainali wasingechukua kombe.....mnaboa sana na vi club vyenu vya majuu......
 
Mimi binafsi siyafagilii kabisa haya mashindano, sioni maana yake ni nini, nahisi hii idea ilitolewa na nchi ambazo hazina wachezaji wanaocheza Ulaya ili tu nao wapate sababu ya kukenua. Ushindi wowote utakaopatikana- tujue kwamba itakapokuja time ya mashindano 'serious' bado tutaendelea kuburuzwa kwa kuwa wenzetu hawatumii 'vifaru' vyao hapa. Mimi nataka tukicheza na Ivory Coast iwe ni first eleven yao regardless wachezaji wao wanacheza ulaya au uchina, kama ni Cameroon iwe hivyo hivyo- Eto' awepo,ikiwa hivi ndo tutapata true reflection ya kiwango chetu cha soka. Tuelewe kwamba hapa timu yetu inayoshiriki ni 'the best 11 tanzanian footballers' ndo wanashuka dimbani wakati wenzetu wanatutoa kamasi na wachezaji ambao hata hawajulikani and we are still struggling- lakini kama kawaida yetu- tunashangilia!!!
Kana ka Mzungu na KASUMBA. Wachezaji waliokosa fursa hii sio wale wa ulaya pekee hata kama unacheza soka la kulipwa hapo Msumbiji na ni ligi ya daraja la tatu, huna nafasi katika mashindano haya. Kwa hiyo mkuu huu ni ushindi tuu, acha watu waufurahie!
 
Jana timu ya taifa, Taifa Stars ilitoka kifua mbele pale ilipoipiga Ivory Coast bao moja kwa yai. Sikutegemea hadi pale Injini ya Stars Mrisho Ngassa alipotia mpira kimiani na kuwanyanyua watanzania kwenye viti vyao na kushangilia ushindi huo mwepesi. Ninategemea pia Marcio Maximo na wapenzi wa mpira wa miguu walifurahi kwa ushindi huo kwani Tanzania imechoka kuwa msindikizaji na kichwa cha mwendawazimu kwenye michezo ya kimataifa. Hoja hii iliwahi kutolewa na aliyekuwa raisi wa awamu ya pili Mheshimiwa Ali Hassani Mwinyi. Kilichabaki sasa ni kuiombea Taifa Star ili ishinde mechi ifuatayo.
 
......ungekuwa unajua soka ungeangalia viwango kijana......mcheza kama Ngassa ana kiwango cha juu sana huwezi kumlinganisha na bito drogba......

Kweli nimekubali unalijua soka....hii ni pure fantasy football, keep on dreaming boy. Wee naona utakuwa hukosi pale jangwani kila siku jioni kubishana kwa mambo ya kusadika kama haya!
 
Kana ka Mzungu na KASUMBA. Wachezaji waliokosa fursa hii sio wale wa ulaya pekee hata kama unacheza soka la kulipwa hapo Msumbiji na ni ligi ya daraja la tatu, huna nafasi katika mashindano haya. Kwa hiyo mkuu huu ni ushindi tuu, acha watu waufurahie!

Chakaza ujue timu kama Senegal, Ivory Coast, Cameroon na Nigeria wachezaji wao wa first 11 wote wanacheza nje! Sasa kwa mataifa kama haya yatakuwa yanashirikisha timu D zao. Nasema hivyo kwa kuwa -timu A ndo hao first 11, timu B ni 'spare parts' za timu A, wao wanakaa bench na kusubiri lolote litokee kwa wale wa timu A ndo nao wapate cheza- hawa nao wanacheza Ulaya! Timu C ni wale wote wanaocheza nje ya nchi kwenye viligi uchwara duniani na madaraja ya chini Ulaya- hawa nao hawamo. Timu D ndio hao walioko nyumbani- ambao tukicheza nao wanatufunga na tukishinda ni 1-0! Na katika nchi za West Africa kama unaweza mpira -msimu wako ni mmoja tu kwenye local league manake kuna ma agents kibao huko na kuuza wachezaji ndio shughuli yao kubwa, sasa you can imagine uwezo wa wachezaji ambao wanabaki kucheza kwenye local leagues uko vipi. Mind you sisi tunaingia na full squad letu huko, huoni kuwa ni bakora vs bunduki lakini bado mwenye bunduki anatolewa manundo? Jamaa wa bakora naye akiruhusiwa kushika mtutu si itakuwa kiama?
 
sare ya zambia na senegal ni ahueni, now we stan almost equal chances....... twahitaji ushindi dhidi ya zambia

sare ya Senegal na Zambia si ahueni hata kidogo ni mbaya ajili kama ikitokea tukatoka droo mechi ya mwisho sisi na zambia halafu sengali akafungwa na wenyeji ivory coast hali itakuwa ngumu kwetu, ila mmoja wao angefungwa afu mechi ya mwisho hata tukitoka droo basi tunakuwa na nafasi ya pili, lakini sasa tunalazimika kumshinda Zambia na Droo yoyote ile haitusaidii hata kama senegal akifungwa.
 
Back
Top Bottom