Changamoto kubwa ya Kiusalama kwa Urusi na hatma ya Usalama barani Ulaya

Na ISS itaibuka tena maana maelfu ya wapiganaji walio kuwa wameshikiliwa kwenye magereza wameachiwa.
Watu wanacheka sasa ila tuupe muda nafasi.

Nahofia Syria kugeuzwa Libya kila kikundi kujitwalia eneo lake na vita visivyo koma.
 
NATO wamecheza mchazo mkali sana wa kisiasa dhidi ya MRUSI.

Mosi, wameanzisha mtafaruku Lebanon kwa kumtumia mshirika wao mkubwa Israel, jambo ambalo limepelekea vikosi vingi vya Hizbullah kuondolewa nchini Syria na kurudishwa Lebanon kuzuia uvamizi wa Israel. Jambo hili limechangia kwa kiasi kikubwa Syria kukosa ulinzi katika eneo la Aleppo.

Pili, NATO kutumia mwanachama wake Turkey wamefanya shambulio zito dhidi ya Syria kwa kutumia mgongo wa makundi ya waasi na makundi mengina ya kigaidi. Jambo hili limewaweka Warusi na Wairani njia panda kwasababu kwasasa Iran anasaidia washirika wake Hizbullah kupambana nchini Lebanon, hivyo ni ngumu kurudisha au kuvigawanya vikosi vya Hizbullah baina Syria na Lebanon kama ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo vikosi vya Hizbullah vilijazana nchini Syria.

Tatu, Urusi ndiye aliyetoa mchango mkubwa kwa Syria mwaka 2015 ili Assad asipinduliwe. Kipindi hiki yuko kwenye wakati mgumu kwasababu hawezi kutuma vikosi vyake ilhali yuko anapambana na Ukraine na NATO kule Donbass. Mwaka 2015 alitumia vikosi vyenye wanajeshi wasiopungua 60,000 hadi kukamilisha ile vita dhidi ya waasi na magaidi. Kipindi hiki kupeleka wanajeshi 60,000 siyo jambo rahisi.

Nne, NATO na EU wameanzisha chokochoko nyingine nchini Georgia kama zile za Maidan nchini Ukraine mwaka 2014 ambazo ndiyo chanzo kikubwa cha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Serikali iliyopo Georgia ina mahaba na Moscow, EU, Ukraine na NATO hawataki hili litokee kabisa. Upande mwingine Urusi hataki kabisa Georgia igeuke Ukraine nyingine. Hivyo kama mambo yakiwa mabaya na serikali ikapinduliwa itabidi avamie kijeshi. Mwaka 2008 alivyovamia Georgia alitumia vikosi vyenye wanajeshi 75,000. Kipindi hiki sidhani kama itakuwa rahisi.

Tano, NATO wanamtumia Turkey kwasababu wanafahamu fika kwamba, ili Urusi afanye oparesheni zake za kijeshi za anga ni lazima atumie anga la Turkey. Lakini pia, Turkey ni nchi jirani na Georgia, hivyo Urusi akivutana Turkey ina maana NATO wataitumia nchi hiyo kama njia ya kufanya vurugu dhidi ya Urusi kupitia Georgia.

Kubwa zaidi na hatari, ili manowari za kijeshi za Urusi zitoke Black Sea na kufika kwenye kambi ya kijeshi ya Urusi iliyoko Syria, ni lazima wapite nchini Uturuki kwenye mfereji wa The Bosphorous. Wakivutana Urusi atazuiwa kupita kama ambavyo mwaka 2015 nchi ya Malta ilizikataa manowari za Urusi kupita kwenye mipaka yake. Kazi ngumu.

Sita, kama Iran ataingilia moja kwa moja basi lazima Israel na Turkey wataingia kwenye vita dhidi ya Syria moja kwa moja kwasababu nchi zote hizi hazimpendi Iran. Israel na Turkey wakiungana madhara makubwa sana yatatokea nchini Syria na Israel hasahasa ukizingatia uwezo wa kijeshi ambao Iran kauonesha hivi karibuni.

Saba, Urusi na Iran wanaweza kutumia mgambo wa Houthis, japo hili nalo ni changamoto kwasababu tayari baadhi ya mgambo wako Urusi wanapambana kule Donbass, lakini pia Houthis wamekabwa koo hivi karibuni baada ya UK, USA na ISRAEL kuongeza nguvu ya mashambulizi dhidi yao kuvisaidia vikosi vya serikali.

MRUSI ATAFANYA NINI SASA ????

Anaweza kuhusika moja kwa moja kwa kupeleka vikosi vyake, japo hili ni jambo la hatari mno hata kama mpaka sasa ana vikosi vya wanajeshi milioni 1.15 (Active Personnel), hili litasababisha nguvu zake kule Ulaya kupungua.

Mchezo kama huu USSR alichezewa mwaka 1969 na NATO, baada ya kuona vikosi vyake vizito viko Eastern Europe, waliamua kuitumia China kuvamia mpaka wa kusini wa USSR ambao haukuwa na wanajeshi wengi. Ilikuwa ngumu kwa USSR kupeleka vikosi mpaka wa kusini kupambana na CHINA ndani ya usiku mmoja ilhali kule Ulaya kuna vikosi vizito vya NATO.

AU, Mrusi anaweza kufanya jambo la hatari zaidi ambalo wazungu hawawezi kulipenda. Kukodi maelfu ya mamluki kutoka Asia na Afrika wajazane Ulaya kuua maelfu ya Wazungu, jambo ambalo litakuwa ni hatari mno kwa bara la Ulaya.

Ila kubwa zaidi ni kwamba vita ikiendelea basi, UE itaendelea kupokea wimbi kubwa mno la wakimbizi kama ilivyokuwa 2011-2016, jambo ambalo litakuwa siyo zuri hasa kwa kipindi hiki ambacho uchumi wa mataifa ya UE umegubikwa na mfumuko mkubwa wa bei.

ENDAPO MATAIFA YATAHUSIKA MOJA KWA MOJA: Mfano Iran aende Syria basi lazima The Persian Gulf yote itahusika kwasababu hakuna taifa linaloweza kupambana na Iran bila kutumia korido za nchi kama Qatar, Saudi Arabia na Bahrain. Nchi hizi ambazo zina kambi za jeshi za Marekani zikitumika kuishambulia Iran, lazima nazo zitashambuliwa vibaya.

NB: Mpaka sasa, kwenye huu mchezo mwenye THE UPPER HAND ni Benjamin Netanyahu na Israel yake. Akizichanga karata zake vizuri (Jambo ambalo sidhani kama ataweza) basi anaweza kupata suluhu kubwa kabisa ya kidiplomasia hasa kule GAZA na WEST BANK, lakini pia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kumtenga IRAN kutoka Lebanon na Syria.

SWALI: Je, Mrusi anaweza kukubali kupoteza kambi zake muhimu za kijeshi kule Tartus na kukubali maslahi yake mengine ya kiusalama yapotee kwa kukubali kuachia serikali ya Assad ianguke ???
Wewe Kafir, subiri mpate kipigo makafir nyie, hamna lolote hamumjui Mrusi. nyie mashoga mtakiona cha moto sasa...mmyavagaa huo ni mtego mtachakazwa sana kama hamulewi na mtafutwa duniani mashoga nyie.
 
Hilo la kukodi mamluki tayari limeshafanyika. Wengine maelfu wamesafirishwa kutoka North Korea, of all places!

Naona waasi wa Syria wameamua kumpa darasa Mrusi jinsi ya kufanya "Special Military Operation". Things are escalating so quickly, Waingereza wanasema.

Wengine acha tuendelee kuwa bize na kutafuta ugali kwa ajili ya familia. Tuendelee ku-pretend kama vile hakuna kinachoendelea.
Perfomance ya HTS imekuwa nzuri sana hasahasa kwenye matumizi ya teknolojia na uwezo wa kutengeneza silaha zao wenyewe. Wataalamu wanasema wanatumia mbinu za jeshi la Uingereza hivyo tunafahamu kwamba British SAS ndiyo wamekuwa wakiwafundisha tokea 2020 baada ya mkataba wa Astana. Changamoto zinazowakumba HTS ni ileile ambayo iliwakumba Ukraine baada ya 2022.

Mosi, wameanza vizuri na kwa haraka mno. Inabidi wafanikishe kuitoa serikali ya Assad kipindi hikihiki ambacho upepo uko upande wao, na wakishindwa walau wailazimishe serikali hiyo kukaa mezani na kufanya makubaliano maana kwasasa wana The Upper Hand. Wakishindwa kuitoa serikali ya Assad hii vita itageuka kuwa A War of Attrition kama Ukraine.

Pili, A War of Attrition inategemea vitu vikubwa viwili, Ability to Produce Artillery at an industrial scale na Ability to mass mobilise personnel. Mpaka sasa, HTS wana wanajeshi wasiopungua 30,000, huku Syria ina wanajeshi 170000 na ina uwezo wa kukusanya wanajeshi wengi zaidi kupitia Conscription. HTS wameonesha uwezo mkubwa mno wa kutengeneza Drones na silaha za kisasa, lakini sidhani kama wana uwezo wa kuwashinda Iran na Urusi katika kuzalisha silaha za kijeshi.

Changamoto kubwa ambayo imewakuta NATO kule Ukraine ni ability to supply Ukraine with armaments on time. NATO wamesema kwasasa Russian Arms Industry is on full capacity na imeajiri watu milioni 3 wanaofanya kazi kubwa kulisaidia jeshi la Mrusi kule Ukraine. Inakadiriwa Mrusi anazilisha silahaa mara 10 zaidi ya NATO kwa kipindi hiki. Ukizingatia na anavyosaidiwa na Arms Industry za China, Iran na North Korea ndiyo tatizo zaidi.

HTS watapambana, lakini itafika kipindi watahitaji silaha kutoka nchi za Magharibi. Israel mwenyewe wakati anapambana na Hamas na Hizbullah aliishiwa na silaha akaenda kwenye Congress kuomba, sembuse HTS. Hivyo wasipoweza kumtoa Assad kwasasa au kumlazimisha kukaa meza ya makubalioni kipindi hiki na washirika wake kama Iran, Russia, China na North Korean wakaanza kumpa silaha, sidhani kama NATO wataweza kuwapa silaha Israel, Ukraine na HTS kwa pamoja, kwasababu ni jambo la gharama mno.

Kubwa zaidi ni kwamba ili HTS wazalishe silaha zao itabidi wategemee supply lines ambazo China na Japan hawawezi kwepeka. Sasa, jiulize itakuwa rahisi kama China ataweka ugumu ?

War is just boring!
 
Uchambuzi mzuri sana ila ngoja tuone
Mwisho wa hili hauwezi kuwa mzuri kabisa, hasa ukizingatia tabia za warusi za mwaga mboga, mimi namwaga ugali. Mchezo kama huu ndiyo ulipelekea Cuban Missile Crisis 1962 ambapo mwaka 1959, Marekani aliweka makombora yake ya Jupiter & Thor nchini Turkey, USSR akalipiza kwa kuweka makombora nchini Cuba. Mwaka 1969 NATO waliitumia China kuvamia Urusi, wachina wakajua yameisha kumbe warusi wana kinyongo.

Mwaka 1979, China akajichanganya akavamia Vietnam, akakiona chamoto. Alitandikwa mno hadi akakimbia kwa aibu. USSR ilimpa Vietnam silaha za kisasa kabisa, mafunzo na taarifa za kijasusi hadi kupeleka nchi ile kuwa na jeshi bora kabisa Asia ambalo liliweza kuwashinda Marekani na Wachina katika nyakati tofauti.

North-Korea na Iran, ni mataifa ambayo yako kwenye vikwazo vya UNSC ambavyo China na Russia wanashiriki katika kuhakikisha hizi nchi hazipati silaha za kisasa ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa dunia. Ukizingatia mchango wa North Korea na Iran kwenye vita ya Ukraine ni dhahiri kabisa Mrusi atawalipa.

Iran na Korea wakipewa teknolojia kama zile za Mrusi walau kwenye kutengeneza makombora, nyambizi na satellaiti, hali itakuwa mbaya kwa washirika wa NATO kama Israel, Saudi Arabia, Japan na South Korea. Leo hii Mrusi akiamua kujitoa kwenye vikwazo vya Iran na North Korea, NATO na EU watasemaje ?

Ndiyo maana nikasema, Netanyahu akichanga karata zake vizuri ataondoka na ushindi mkubwa sana wa kidiplomasia. Japo sidhani kama ataweza kufanya hivyo ukizingatia his ZERO-SUM MINDSET.
 
Mwisho wa hili hauwezi kuwa mzuri kabisa, hasa ukizingatia tabia za warusi za mwaga mboga, mimi namwaga ugali. Mchezo kama huu ndiyo ulipelekea Cuban Missile Crisis 1962. Lakini, hata ambavyo NATO waliitumia China kuvamia Urusi mwaka 1969, wachina wakajua yameisha kumbe warusi wana kinyongo.

Mwaka 1979, China akajichanganya akavamia Vietnam, akakiona chamoto. Alitandikwa mno hadi akakimbia kwa aibu. USSR ilimpa Vietnam silaha za kisasa kabisa, mafunzo na taarifa za kijasusi hadi kupeleka nchi ile kuwa na jeshi bora kabisa Asia ambalo liliweza kuwashinda Marekani na Wachina katika nyakati tofauti.

North-Korea na Iran, ni mataifa ambayo yako kwenye vikwazo vya UNSC ambavyo China na Russia wanashiriki katika kuhakikisha hizi nchi hazipati silaha za kisasa ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa dunia. Ukizingatia mchango wa North Korea na Iran kwenye vita ya Ukraine ni dhahiri kabisa Mrusi atawalipa.

Iran na Korea wakipewa teknolojia kama zile za Mrusi walau kwenye kutengeneza makombora, nyambizi na satellaiti, hali itakuwa mbaya kwa washirika wa NATO kama Israel, Saudi Arabia, Japan na South Korea. Leo hii Mrusi akiamua kujitoa kwenye vikwazo vya Iran na North Korea, NATO na EU watasemaje ?

Ndiyo maana nikasema, Netanyahu akichanga karata zake vizuri ataondoka na ushindi mkubwa sana wa kidiplomasia. Japo sidhani kama ataweza kufanya hivyo ukizingatia his ZERO-SUM MINDSET.
Na hapa kazi ipo kweli maana ila naungana na wewe nyau atakua either bet looser au best winner ngoja tuone
 
Samahani mkuu Mchina na Mrusi mahusiano yao ya kuwa karibu ilikuwa ni wakati gani? Je, ni baada ya kuvunjika kwa USSR?
Natamani sana Urusi yenye nguvu kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya hizi nchi zinazoongozwa na wapumbavu.
 
Kuanguka kwa Syria hakuwezi kuifanya Russia kuwa dhaifu, japo italeta changamoto kubwa sana kwake..........

USSR na China waligombana baada ya Iosiph Stalin kufa. Ugomvi wao uliitwa Sino-Soviet Split, na uliisha miaka ya 90's ambapo walipatana tena.......
 
NATO wamecheza mchazo mkali sana wa kisiasa dhidi ya MRUSI.

Mosi, wameanzisha mtafaruku Lebanon kwa kumtumia mshirika wao mkubwa Israel, jambo ambalo limepelekea vikosi vingi vya Hizbullah kuondolewa nchini Syria na kurudishwa Lebanon kuzuia uvamizi wa Israel. Jambo hili limechangia kwa kiasi kikubwa Syria kukosa ulinzi katika eneo la Aleppo.

Pili, NATO kutumia mwanachama wake Turkey wamefanya shambulio zito dhidi ya Syria kwa kutumia mgongo wa makundi ya waasi na makundi mengina ya kigaidi. Jambo hili limewaweka Warusi na Wairani njia panda kwasababu kwasasa Iran anasaidia washirika wake Hizbullah kupambana nchini Lebanon, hivyo ni ngumu kurudisha au kuvigawanya vikosi vya Hizbullah baina Syria na Lebanon kama ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo vikosi vya Hizbullah vilijazana nchini Syria.

Tatu, Urusi ndiye aliyetoa mchango mkubwa kwa Syria mwaka 2015 ili Assad asipinduliwe. Kipindi hiki yuko kwenye wakati mgumu kwasababu hawezi kutuma vikosi vyake ilhali yuko anapambana na Ukraine na NATO kule Donbass. Mwaka 2015 alitumia vikosi vyenye wanajeshi wasiopungua 60,000 hadi kukamilisha ile vita dhidi ya waasi na magaidi. Kipindi hiki kupeleka wanajeshi 60,000 siyo jambo rahisi.

Nne, NATO na EU wameanzisha chokochoko nyingine nchini Georgia kama zile za Maidan nchini Ukraine mwaka 2014 ambazo ndiyo chanzo kikubwa cha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Serikali iliyopo Georgia ina mahaba na Moscow, EU, Ukraine na NATO hawataki hili litokee kabisa. Upande mwingine Urusi hataki kabisa Georgia igeuke Ukraine nyingine. Hivyo kama mambo yakiwa mabaya na serikali ikapinduliwa itabidi avamie kijeshi. Mwaka 2008 alivyovamia Georgia alitumia vikosi vyenye wanajeshi 75,000. Kipindi hiki sidhani kama itakuwa rahisi.

Tano, NATO wanamtumia Turkey kwasababu wanafahamu fika kwamba, ili Urusi afanye oparesheni zake za kijeshi za anga ni lazima atumie anga la Turkey. Lakini pia, Turkey ni nchi jirani na Georgia, hivyo Urusi akivutana Turkey ina maana NATO wataitumia nchi hiyo kama njia ya kufanya vurugu dhidi ya Urusi kupitia Georgia.

Kubwa zaidi na hatari, ili manowari za kijeshi za Urusi zitoke Black Sea na kufika kwenye kambi ya kijeshi ya Urusi iliyoko Syria, ni lazima wapite nchini Uturuki kwenye mfereji wa The Bosphorous. Wakivutana Urusi atazuiwa kupita kama ambavyo mwaka 2015 nchi ya Malta ilizikataa manowari za Urusi kupita kwenye mipaka yake. Kazi ngumu.

Sita, kama Iran ataingilia moja kwa moja basi lazima Israel na Turkey wataingia kwenye vita dhidi ya Syria moja kwa moja kwasababu nchi zote hizi hazimpendi Iran. Israel na Turkey wakiungana madhara makubwa sana yatatokea nchini Syria na Israel hasahasa ukizingatia uwezo wa kijeshi ambao Iran kauonesha hivi karibuni.

Saba, Urusi na Iran wanaweza kutumia mgambo wa Houthis, japo hili nalo ni changamoto kwasababu tayari baadhi ya mgambo wako Urusi wanapambana kule Donbass, lakini pia Houthis wamekabwa koo hivi karibuni baada ya UK, USA na ISRAEL kuongeza nguvu ya mashambulizi dhidi yao kuvisaidia vikosi vya serikali.

MRUSI ATAFANYA NINI SASA ????

Anaweza kuhusika moja kwa moja kwa kupeleka vikosi vyake, japo hili ni jambo la hatari mno hata kama mpaka sasa ana vikosi vya wanajeshi milioni 1.15 (Active Personnel), hili litasababisha nguvu zake kule Ulaya kupungua.

Mchezo kama huu USSR alichezewa mwaka 1969 na NATO, baada ya kuona vikosi vyake vizito viko Eastern Europe, waliamua kuitumia China kuvamia mpaka wa kusini wa USSR ambao haukuwa na wanajeshi wengi. Ilikuwa ngumu kwa USSR kupeleka vikosi mpaka wa kusini kupambana na CHINA ndani ya usiku mmoja ilhali kule Ulaya kuna vikosi vizito vya NATO.

AU, Mrusi anaweza kufanya jambo la hatari zaidi ambalo wazungu hawawezi kulipenda. Kukodi maelfu ya mamluki kutoka Asia na Afrika wajazane Ulaya kuua maelfu ya Wazungu, jambo ambalo litakuwa ni hatari mno kwa bara la Ulaya.

Ila kubwa zaidi ni kwamba vita ikiendelea basi, UE itaendelea kupokea wimbi kubwa mno la wakimbizi kama ilivyokuwa 2011-2016, jambo ambalo litakuwa siyo zuri hasa kwa kipindi hiki ambacho uchumi wa mataifa ya UE umegubikwa na mfumuko mkubwa wa bei.

ENDAPO MATAIFA YATAHUSIKA MOJA KWA MOJA: Mfano Iran aende Syria basi lazima The Persian Gulf yote itahusika kwasababu hakuna taifa linaloweza kupambana na Iran bila kutumia korido za nchi kama Qatar, Saudi Arabia na Bahrain. Nchi hizi ambazo zina kambi za jeshi za Marekani zikitumika kuishambulia Iran, lazima nazo zitashambuliwa vibaya.

NB: Mpaka sasa, kwenye huu mchezo mwenye THE UPPER HAND ni Benjamin Netanyahu na Israel yake. Akizichanga karata zake vizuri (Jambo ambalo sidhani kama ataweza) basi anaweza kupata suluhu kubwa kabisa ya kidiplomasia hasa kule GAZA na WEST BANK, lakini pia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kumtenga IRAN kutoka Lebanon na Syria.

SWALI: Je, Mrusi anaweza kukubali kupoteza kambi zake muhimu za kijeshi kule Tartus na kukubali maslahi yake mengine ya kiusalama yapotee kwa kukubali kuachia serikali ya Assad ianguke ???
Hakuna kitu hapo..NATO wamesha tema bungo sikunyingi kwa sasa wanajititimua tu urusi ipo stable zaidi sasa kuliko kabla ya kuvamia ukrain ..mbinu pekee wanazotumia NATO zilizo kuwa zinawapa tija ni mbinu za choko choko kwa kulivuruga taifa lolote ndani kwa ndani ...hiyo mbinu kwa sasa ni ngumu maana urusi ..kaacha kupuuza chokochoko za NATO.
 
Kwa ufupi Russia ipo kwenye wakati mgumu.

Syria ni eneo ambalo ana air base yake ya Khmeimim na naval facility huko Tartus.

Mbali na hilo Syria kwa Russia ni eneo muhimu kwa energy strategy.

Ikiwa akiruhusu kupoteza Syria, ukizingatia ameshapoteza allies kwenye mkataba wa CSTO, ushawishi wake kimataifa utapungua sana!

Russia ana wakati mgumu sana! Sijui hata akili gani itakayotumika ila ngoja tuone itakuwaje!
 
Kuanguka kwa Syria hakuwezi kuifanya Russia kuwa dhaifa, japo italeta changamoto kubwa sana kwake..........
Sasa Mkuu, watu wameshuhudia Russia imepoteza kwenye Collective Security Treaty Organisation (CSTO).

Washuhudie tena iipoteze Syria, kiushawishi itashuka pakubwa na hili nalo ni pigo katika sura ya kimataifa. Atakuwa haaminiki!
 
Solution bado inaweza punguza manpower ukaongeza kuchapa kwa makombola.
Dunia imefikia mahala patamu sana,hasa ukiwa mfatiliaji wa mambo.
Tukumbuke SAA imeshapoteza maeneo tayari. Ukipiga makombora mwisho wa siku lazima upeleke askari wa miguu.

Kwa upande mwengine USA na Israel wanafanya kila namna kupunguza manpower ambayo Syria anaweza kuipata.

Israel anapunguza na kuzuia upande wa Hizbullah na USA upande wa Iraq wanaojaribu kuingia Syria.

SAA wanakimbia na kuacha maeneo kirahisi sana, na kwa upande wa Russia hawezi kupeleka jeshi lake moja kwa moja kwani ameshabanwa Ukraine na Georgia huko mambo si shwari.

Taarifa nyengine zinasema Syria amekataa msaada wa wanajeshi kutoka Iran akihofia Israel nayo inaweza ikaingia kwenye vita inayoendelea nchini mwake.

Hii vita ni ngumu sana!
 
Back
Top Bottom