MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
- Thread starter
- #61
Mkuu, hii vita ni ya Marekani/ Israeli dhidi ya Russia, Iran na China ambapo Marekani yataka kuhodhi vyanzo vya mafuta katika eneo lote la ghuba.
Lakini pia naona wasahau Uturuki na nafasi yake katika vita hivi vya sasa na harakati za Israeli dhidi ya Syria na Assda.
Wiki ilopita (jummane) Benjamini Netanyahu alisema Syria yacheza na moto pale alipomshutumu Assad kwamba awasaidia Hezbollah kupitisha silaha hapo Damascus.
All in all ni kwamba hii yatuonyesha udhaifu mkubwa wa Syria na Lebanon kwamba zimekuwa pale kama nchi waangalizi. Pia idara zao za ujasusi zimekuwa dhaifu mno kiasi cha kuweza kupenyezewa majasusi kutoka pande zote Israeli, Uturuki na CIA.
Iran nayo imeonyesha udhaifu mkubwa kwenye medani za ujasusi khasa baada ya raisi wao Raisi kuuawa huko milimani chopa lake lilipodunguliwa na pia kabla ya hapo yule Sulemani kudunguliwa, kushindwa na kumlinda Naslallah kutokana na mfumo mzima wa Ujasusi kuingiliwa na Mossad.
Pia Hezbollah kuanza kudunguliwa kwa zile pagers na baadae kiongozi mmoja baada ya mwingine hiyo ni ishara ya ujasusi ulokomaa wa Mossad.
Wakati huohuo kwa mara ingine tena hii yatuonyesha uwezo mkubwa wa Idara za usalama za Mossad na ile ya CIA kwa kazi zao nje ya mataifa yao ambazo ni pamoja na kushirikiana kupalilia vitalu vya magaidi mseto.
Russia na China wao wataendelea kuangalia hali yaendaje lakini Russia wao wana uhakika na kuchukua Donbass na hapo Syria au mashariki ya kati walikuwa ni kama vile wapo sokoni wakiangalia nyanya ipi ni bora.
Nakusoma vizuri mkuu, japo Syria alikuwa hana njia ya kujitoa kwenye mgogoro.
Jambo la kwanza kabisa, NATO na EU walianza kumzorotesha kwa vikwazo vya kiuchumi. Kiufupi serikali ya Assad ilikuwa haina fedha za kutosha kwasababu vyanzo vyake vikubwa vya fedha ni mafuta. Kabla ya vita, Syria ilikuwa inazalisha mapipa 400,000 ya mafuta kwa siku, lakini baada ya vita na visima vingi vya mafuta kukaliwa na USA, Turkey na Kurds, Syria inazalisha mapipa 100,000 tu kwa siku huku asilimia 75% ya hayo mapipa yakizalishwa na USA na Kurds.
Waasi wamepambana vita kwa urahisi kwasababu faida ya mafuta hayo ndiyo imetumika kuwafadhili, huku serikali ya Syria ikiwa haina kabisa fedha na inategemea hisani ya Russia na Iran.
Lakini kubwa zaidi ni kwamba, hata kufika mwaka 2024 tokea mwaka 2011, Assad amejitahidi mno. Kumbuka ukitoa Misri, Syria ndiyo lilikuwa taifa tishio kijeshi kwa Israel. Wengi tunaamini huu ugomvi umeanza 2011, ila ukweli huu ugomvi ulianza 1948 na umechukua sura tofauti mara nyingi. Yom Kippur War 1973 ambayo Israel alipigwa vibaya sana akapona alivyookolewa na Marekani, kinara alikuwa ni Assad Senior. Hivyo kinachoendelea sasa ni mwendelezo tu.
Kuhusu ujasusi, kuna jambo la msingi kabisa ambalo wengi tunaliacha. Mambo haya yote yalianza mwaka 1916 kwenye The Sykes-Picot Agreement, ambapo Britain, France na Russian Empire walikubaliana kuigawa Ottoman Empire kihuni. Wakaanza kuwaunga mkono waarabu ambao walidai uhuru kutoka kwa Ottoman Empire na mwishowe mataifa mengi ya kiarabu, ikiwemo Syria yakazaliwa. Hivyo hili ni eneo ambalo Britain, Marekani, Zionists hawawezi kuliacha tu.
Mwaka 1948, mwaka mmoja mbele baada ya shirika la kijasusi la CIA kuundwa, mapinduzi ya kwanza kabisa yaliyofanywa na CIA yalikuwa ni kupindua serikali ya Syria. CIA walifanya hivyo wakiwa na mikakati ya mbali, maana mwaka huohuo waliunda nchi ya Israel ambayo ndiyo kambi yao kubwa Middle East. Hivyo kuhusu ujasusi, Syria, Hizbullah, Iran, Iraq, Libya na Lebanon hazipambani na MOSSAD tu, zinapambana na CIA, MI6, DIA, NSA, BND, DGSE + THE FIVE EYES ALLIANCE, mashirika makubwa yenye rasilimali nyingi, utaalamu mkubwa na uzoefu wa muda mrefu. Syria taifa lenye watu wasiozidi milioni 25 na rasilimali kidogo lisingeweza kabisa kupambana na hawa watu.
Marekani kabla hajaanza uvamizi wa kijeshi, mbinu yake kubwa ni VIKWAZO kuhakikisha anazorotesha uchumi wako, kisha anakuletea vikundi vya waasi, na mwishowe vita. Iraq, Libya, Afghanistan wote walifanywa hivi kabla ya kuvamiwa. Iran amefanyiwa hivi tokea mwaka 1979, maana bila vikwazo, Iran lingekuwa ni taifa tajiri kuliko hata Saudi Arabia. Marekani hawezi kuruhusu Iran awe tajiri hivyo ni vikwazo mwanzo mwisho.