Changamoto kubwa ya Kiusalama kwa Urusi na hatma ya Usalama barani Ulaya

Si kwa ubaya lakin MWAKA 2025 utachangamka sana kimatukio, kuanzia huko duniani(developed Countries) mpaka huku bara la kiza(developing Countries).

mambo ya chaguzi, kupinduana, visasi, kusalitiana, chokochoko na vitisho, kiufupi mambo yatachangamka sana, kuanzia kisiasa, kijamii mpaka kiimani na kiuchumi kiujumla tujipange na yajayo, Kila mtu akae upande sahihi.

Natia nukta.
 
Kuanguka kwa Assad na kuondoka kwa mshirika wa Urusi hapo Syria ni hasara kubwa kwa Urusi kwani haiwezi project power Middle East na Africa kisawasawa.

Urusi inaitaka Syria kama transit, airlifters za Urusi zote haziwezi toka Urusi zikafika Afrika bila kufanya refuering. Huwa zinatua Latakia pale Khmeimim airbase kwanza kisha ndio zinapeleka mizigo Libya kwa Khalifa Haftar, au zinapeleka mizigo Sudan vitani, au zinaenda Algeria au hizi military junta mpya za West Africa. Ikiwa Syria itaangukia mikononi mwa waasi basi Urusi itakosa access ya kutua Latakia labda wapate access ndani ya Iran.
Sasa sera za kimataifa za Urusi na Iran sio sawa kwa kila kitu, lakini kwa upande wa Syria ya Assad pale Latakia, Urusi ilikuwa ni kama inajitawala. Hivyo kuna limitations ya kipi Urusi atapitisha na kipi hawezi.

Pia Urusi kuikosa Tartus naval base ni hasara kubwa zaidi. Urusi mpaka sasa Afrika haina mshirika ambaye anampa access ya base, mazungumzo na Eritrea au Sudan bado yanaendelea na hayatimii hivi karibuni. Kwahiyo meli za Urusi zitakosa makazi Middle East nzima na Afrika endapo Tartus itaanguka.

Washirika wa kijeshi wa Urusi waliopo Afrika watapata hasara. Sina imani kama waasi wa Syria watakubaliana na Urusi kuipa access ya hizo bases sababu Urusi ilizitumia hizohizo kuwashambulia. Kwa hili labda kwa mbali Urusi inaweza pata temporary access pale Libya upande wa Haftar endapo watafanya makubaliano, ingawa Haftar ni very opportunist and very demanding.

Na kwa namna nyingine, Syria inaungana na Armenia kama nchi zilizopotezwa na ushawishi wa Russia kwenye hii 2020s. Assad alikuwa ni mtu pekee ambaye amekingiwa kifua na Urusi na akabaki anasimama, kuondoka kwake kutapunguza imani kwa strongman mwingine atakayeta kuitegemea Urusi.

Najibu hivi nikiwa na imani Assad anaanguka within few days.
 
Sasa Mkuu, watu wameshuhudia Russia imepoteza kwenye Collective Security Treaty Organisation (CSTO).

Washuhudie tena iipoteze Syria, kiushawishi itashuka pakubwa na hili nalo ni pigo katika sura ya kimataifa.
SOMO KUTOKA LIBYA: Kuangusha serikali ni jambo moja, na kuanzisha utawala wa kiraia ambao unakubalika ndani na nje ya mipaka ya nchi ni jambo jingine kabisa. Syria ni taifa gumu sana kuliko hata Lebanon ukizingatia kuna jamii kama za kishia, kisuni, kikristo, kikurdi na kiarabu. Unadhani HTS wanaweza kutawala nchi ya namna hii ndani ya usiku mmoja kwa kutumia mabomu ya NATO peke yake ???

You may win the war but lose the peace!

KUHUSU CSTO: Nakupa mfano mmoja tu. Baada ya miaka 20 nchini Afghanistan Marekani iliamua kuondoka kwa aibu mwaka 2020-2021 na Taliban wakarudi. Lengo lilikuwa siyo kushindwa peke yake, bali Marekani ilibidi ajikite na kuidhibiti China kupitia mkakati wake The Pivot to Asia.

Ni suala la vipaumbele, japo nadhani changamoto kubwa kwa Syria siyo HTS bali Israel na Turkey ambao wanataka kuimega Syria kwa kisingizio cha kutengeneza Buffer Zones. Sasa Mrusi atafanyaje, nadhani muda ndiyo utasema.
 
Sasa Mkuu, watu wameshuhudia Russia imepoteza kwenye Collective Security Treaty Organisation (CSTO).

Washuhudie tena iipoteze Syria, kiushawishi itashuka pakubwa na hili nalo ni pigo katika sura ya kimataifa. Atakuwa haaminiki!
Hivi karibuni Uturuki ana mafanikio kidiplomasia kuliko Urusi.

Uturuki kaiunga mkono Azerbaijan dhidi ya Armenia iliyoungwa mkono na Urusi na Iran, akashinda.

Uturuki ndio aliiokoa serikali ya Libya ile Government of National Accord kwa kuipa silaha na mafunzo na baadad kafanikisha kuiunganisha na kundi wakaunda Government of National Unity. Turkey ndio sponsor wao na mlinzi wao mkubwa.
Urusi pale Libya inashirikiana hasa na UAE kuunga mkono na Misri kuunga mkono serikali ya kundi la Khalifa Haftar. Bado Uturuki inashinda.

Uturuki anaelekea kuishinda influence ya Urusi na Iran hapo Syria.

Kiufupi calculations za Uturuki zinaleta majibu positive kila ikijipa majukumu magumu.
 

Mwaka huu 2024, Mrusi katengeneza The North-South Corridor, inayopotia Russia-Iran-India, hivyo kumfanya Mrusi kuwa moja ya mataifa wadau wa The Persian Gulf. Sasa Mrusi ataweka kambi yake Iran au India ili kufika Afrika na Mashariki ya kati, sifahamu.

Ukisoma historia utafahamu kwamba hii njia, The Persian Route, ndiyo ilitumika sana kipindi cha WW2 na USA, Britain na USSR kuunganisha Asia-Europe-Afrika. Hii njia iliwahi kusababisha ugomvi mkubwa baina ya USSR na USA hadi kupeleka Truman kuwatisha USSR waondoke Iran ndani ya masaa 48, ili kuwazuia wasiweze kupata sehemu ya kimkakati ambayo itawapa uraisi wa kufika Middle East-Central Asia-Far East-Afrika.

Sasa kipindi hiki kina Mullah wa Iran wanawaogopa NATO, unadhani nini kitawazuia kuwaruhusu Warusi wasiweke kambi kwenye The Persian Gulf, jambo ambalo litakuwa na hatari zaidi ukizingatia ni World's Oil Choke Point.

What a Time To Be Alive......
 
Kuhusu India hiyo option tuiondoe mkuu.
India nayo itataka kuwa superpower muda si mrefu ujao hivyo haitaki kuwa subjugated kwenye maamuzi ya superpower mwingine. Power dynamics za India ni kuwachanganya washirika wake na isitegemee nchi moja kwa wingi lakini pia isinunue ugomvi. Iliweza kununua mafuta ya Urusi akiwa na vikwazo, hapohapo ni adui na China, hapohapo inanunua silaha Urusi lakini pia na Marekani.

Tubaki na Iran, ndio maana pale nikaandika endapo Khmeimin airbase itaponyoka mikononi mwa Urusi, basi Iran ndio inaweza kuwa suluhisho. Hata hivyo Urusi haitokuwa na autonomy kama ilivokuwa Syria.

Kwanza, Urusi ina mahusiano mazuri na Israel, kuweka kambi Iran watapishana.

Pili, Iran na Urusi sio kila sehemu ya kiusalama wanakubaliana.

Tatu, Iran itataka benefits kubwa kwenye makubaliano ya kuweka base ya Urusi kwao. Kwa Assad yeye Urusi ilikuwa inatumia kisingizio cha kumlinda, Iran haihitaji kulindwa na Urusi hivyo lazima kuna kitu kikubwa kiwekwe mezani na Urusi ndio Iran iingie risk ya kuweka airbase ya Urusi. Pia hata bandari inaweza kaa Iran, changamoto ibaki Bosphorus.

Hasara nyingine ni kuwa Iran inatafutwa. Urusi ingepata nchi yenye mgogoro uliojifia kama ilivyokuwa Syria ingekuwa bora zaidi kuliko Iran ambako pako very active.

Au basi Urusi iunde "People's Repuplic" hapo Syria jambo ambalo ni gumu mno kwa sasa.
 
Nafikiri wakimbizi huwa hawachagui mahali pa kwenda na kujihifadhi. Wanajibanza popote pale penye usalama kuliko kule walikokuwa.

Labda wahamiaji (immigrants) ndio ambao huwa wanachagua mahali au nchi ya kukimbilia.
Utakuwa mjinga, utoke bongo nchi yenye asili ya Oligarchy uende ugenini kwenye Oligarchy tena? Tofauti ya urusi na bongo ni maendeleo tu ila mikandamizo inayoendelea kule na hapa bongo ni sawa tu. Ukiisema CCM ya urusi umeisha.
 
Waache wachezeane draft sisi tuendelee kushangaa
 
Mkuu kiaje?

Sasa kinotokea Syria ni mpango wa kuwatanua Russia na mgogoro wake na Ukraine jambo ambalo Russia limestukia.

Russia walikuwa wameleke vikosi vya Wagner pale lakini wamebadili mawazo na wataendelea kulinda base yao hiyo ya Turtus. Pia wameona SMO yakaribia kuchukua Donbass yote hivyo kasi yake isipungue.

Hivyo kilibakia na hao HTS na wakurdi na Sunni kuingia Damascus kisha kuwafungulia mlango Israeli ambao siku zote wamekuwa wakisema wataka kuhakikisha Hezbollah hawapati silaha kutoka Iran kupitia Syria.

Kwahiyo Russia, Iran na China wameona wamwachie Erdogan aende Damscus na kundi lake huku wao wakiangalia tu maana walimwonya Assad kuhusu Cells zilizokuwa zikiandalwia na Mossad.

Syria haina tofauti sana na Lebanon kwani ni nchi ambazo kwa jina zajulikana hivo lakini kiuhalisia hazina nguvu yoyote ile na mwisho wake ndo kama unavyouona.

Israeli anaingia hapo Syria na IDF watakuwa wakiangalia pande hiyo kutokea milima ya Golan ambayo tayari wameichukua na kuanzia hapo Syiria hadi Palestione upande wa kaskazini itakuwa yatawaliwa na Israeli na hakutakuwa na shida yoyote kwake.

Lakini bado vita kubwa imepangwa kutokea mjini Damascus na Assad alionywa na Russia walipomsaidia 2015 lakini hakutaka kufuata ushauri wao wa kuhakikisha ajijenga na kujenga Syria mpya.
 
Syria, Lebanon na Iraq zimeshaanguka unadhani Iran atakuwa na nguvu kubwa ya kupambana na NATO na Israel peke yake hali wamemzunguka pande zote kuanzia Saudi Arabia, Bahrain, Qatar na Pakistan ???

Huu ni ushindi mkubwa mno kwa Israel na Netanyahu. Binafsi naamini Iran inaweza kujilinda japo bila kushirikiana na mataifa kama Russia na China, ni suala la muda tu nayeye. Hivyo kama Russia wataweka kambi nchini Iran, jambo ambalo naamani linawezekana sana hasa kipindi hiki, litakuwa A Desperate Move & An Alliance of Convenience.

Kuhusu India, nakubaliana kabisa na wewe, kutakuwa na bandari peke yake ambayo inaweza kuwa na Dual-Use, japo kambi ya jeshi ni ngumu kama ulivyosema.

Either Way, Syria has fallen,
Another Major Win for the Empire.
 
Uko sawa kabisa anetafutwa hapo ni Iran.

Israeli keshafanikisha kuwamaliza nguvu Hezbollah na uwezo wao wa kujigroup na kupata silaha kutoka Iran.

Pili, Israeli akiwa hapo Syria ataweza kabisa kuingalia Iran kwa karibu zaidi kwa kuweka Buffer zone.
 
Assad ameshapinduliwa Mrusi amedhalilika sana kwa hili. KAMA mshirika wako mhimu anaangushwa kwa vita ya week moja huwezi kuwa na maana kujiita Super Power ni hovyo tu..

Putin kumbe hana lolote ni mbabaishaji tu Syria pale Urusi ana kambi zake 2 kama Waasi wamechukua na wamesaidiwa na Israel na UK basi ni aibu kubwa
 
inaelekea tunafikiri tofauti,mimi nafikiri hasira za mataifa ya ulaya kwa russia kama ufaransa,ni kupoteza ushawishi wao kwa makoloni yao africa magharibi,na kufungwa kambi zao,kisha kuwaalika wagner ili washirikiane nao,
Vita vya ukraine,vinamnufaisha USA,lakini sio mataifa ya ulaya,ambayo hutegemea gas ya urusi kuendesha mitambo yao ya udhalishaji viwandani na matumizi mengine
Pia chakula kwa sehemu kubwa ulaya inategemea urusi na ukraine,na kwa sasa mifumuko ya bei ni mikubwa sana huko ulaya kama sio duniani.
Urusi ni taifa kubwa,likitikisika hata wale wanaompinga,kwa namna moja nao wataathirika tu.
 
Assad ameshapinduliwa Mrusi amedhalilika sana kwa hili. KAMA mshirika wako mhimu anaangushwa kwa vita ya week moja huwezi kuwa na maana kujiita Super Power ni hovyo tu
Unataka warusi wafanyaje kam askari wa assad hawatak kupigana hao waasi wana silaha duni jeshi lina kila kitu then wanaachia tu maeneo hio imewakatisha tamaa urusi na irani. Urusi pia ana vita kwake.
 
1.Nafikiri warusi sio wajinga kiasi hicho - haya mambo lazima waliishayaona na wamecalculate risk na maamuzi bila shaka wazee wa wazee wa SVRna GRU waliishafanyia kazi kitambo sana.
2.Urusi katulia tuliii hapo Syria. Hatujaona akiangaika sana au kupanick kisa hao waasi wanaingia..na kitu cha ajabu - HATUJASKIA mpaka sasa hao waasi wakitamka RUSSIA MUST GO- Wote wapo kimya kabisa.
3.Behind the scene hii awamu ya pili ya movement ya waasi ni muendelezo wa vita kati ya Hezbollal na Israel.Syria imekuwa ikiwapatia silaha Hezbollah - kupitia Damascus na kwingineko. Ili kuimaliza kabisa Hezbollah ni lazima njia za panya zote zizibwe.- Ndo hapo Damascus kwa Assad - So Russia hajihusishi na migogoro ya Syria na Israel..hili aliweka wazi kitambo sana na ndo maana ingawa Russia yupo Syria bado aliwapa Israel waendelee na operation zao hapo.
4.Hii operation watu wengi watakua wamehusika au kuna makubaliano yamewekwa kati ya ISRAEL,TURKEY, IRAN, RUSSIA. Ndo maana husikii kelele kote huko.
HIvyo sioni Urusi akiwa kwenye hatari yoyote zaidi hatujaona wala jusikia viashiria vyovyote kutoka kwa waasi vikisema Russia waondoke.
Ikumbukwe kuwa hawa waasi wanapiga mpaka interview na tv za Israel na wanawashukuru Wayahudi - Wayahudi na Warussi hata kama wanautofauti but wapo wanawasiliana at least for now : Putin & Netanyahu wako karibu sana - so Israel will not do kitu ambacho kitamuumiza Russia maximumly...
 
Mkuu, hii vita ni ya Marekani/ Israeli dhidi ya Russia, Iran na China ambapo Marekani yataka kuhodhi vyanzo vya mafuta katika eneo lote la ghuba.

Lakini pia naona wasahau Uturuki na nafasi yake katika vita hivi vya sasa na harakati za Israeli dhidi ya Syria na Assda.

Wiki ilopita (jummane) Benjamini Netanyahu alisema Syria yacheza na moto pale alipomshutumu Assad kwamba awasaidia Hezbollah kupitisha silaha hapo Damascus.

All in all ni kwamba hii yatuonyesha udhaifu mkubwa wa Syria na Lebanon kwamba zimekuwa pale kama nchi waangalizi. Pia idara zao za ujasusi zimekuwa dhaifu mno kiasi cha kuweza kupenyezewa majasusi kutoka pande zote Israeli, Uturuki na CIA.

Iran nayo imeonyesha udhaifu mkubwa kwenye medani za ujasusi khasa baada ya raisi wao Raisi kuuawa huko milimani chopa lake lilipodunguliwa na pia kabla ya hapo yule Sulemani kudunguliwa, kushindwa na kumlinda Naslallah kutokana na mfumo mzima wa Ujasusi kuingiliwa na Mossad.

Pia Hezbollah kuanza kudunguliwa kwa zile pagers na baadae kiongozi mmoja baada ya mwingine hiyo ni ishara ya ujasusi ulokomaa wa Mossad.

Wakati huohuo kwa mara ingine tena hii yatuonyesha uwezo mkubwa wa Idara za usalama za Mossad na ile ya CIA kwa kazi zao nje ya mataifa yao ambazo ni pamoja na kushirikiana kupalilia vitalu vya magaidi mseto.

Russia na China wao wataendelea kuangalia hali yaendaje lakini Russia wao wana uhakika na kuchukua Donbass na hapo Syria au mashariki ya kati walikuwa ni kama vile wapo sokoni wakiangalia nyanya ipi ni bora.
 
Syria Wasuni ni majority, Iraq uko wako almost nusu kwa nusu Wasuni na Washia ila kwa sasa wenye mamlaka ni Wasuni na Washia wana wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran, Saudi Arabia Wasuni ni wengi zaidi, Yemen Washia hao Houthi ndio wana madaraka.

Mpaka sasa Iran imebaki na Iraq kwa uchache na Yemen ambayo haina faida kiuchumi labda kiusalama pale ghuba. Iran huwa inapenda kuitumia Iraq kama corridor endapo itawekewa vikwazo vya kiuchumi, Iran haitokubali kuipoteza Iraq na huwa inaitia hasara sana hata former PM wa Iraq niliona anapambana mno na Iranian influence.
Ukichunguza hata Assad hakuwa anataka silaha za Iran zipite kwenda Lebanon na Israel ilikuwa ikimuonya azuie au atalipa usumbufu. Tatizo la Iran akikusaidia unakuwa mtumwa wake.

Iran inasponsor makundi ya Kishia hapo Middle East ndio sababu nchi nyingi zinaungana kuihofia. Israel na NATO zamani hawakuwa na kauli dhidi ya umoja wa Kiarabu, enzi za kina Hafez al Assad.

Tatizo lilikuja kwa ME wenyewe kupigana, Saddam kawapiga Kuwait na akatishia kuivamia Saudi Arabia. Saddam kaivamia Iran. Mara Muslim Brotherhood ina wadhamini Uarabuni na wakati huo bado ni kundi la kigaidi kwa serikali nyingine za Kiarabu.

Kujiimarisha kwa NATO na Israel lawama ziende kwa Middle East wenyewe kutoaminiana na kutunishiana mabavu. Wakishindwana watakuja North Afrika kama ambavyo UAE imeanza kila mgogoro ipo.
 
Russia ya Putin kwa sasa unaionaje Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…