Changamoto kubwa ya Kiusalama kwa Urusi na hatma ya Usalama barani Ulaya

Nakusoma vizuri mkuu, japo Syria alikuwa hana njia ya kujitoa kwenye mgogoro.

Jambo la kwanza kabisa, NATO na EU walianza kumzorotesha kwa vikwazo vya kiuchumi. Kiufupi serikali ya Assad ilikuwa haina fedha za kutosha kwasababu vyanzo vyake vikubwa vya fedha ni mafuta. Kabla ya vita, Syria ilikuwa inazalisha mapipa 400,000 ya mafuta kwa siku, lakini baada ya vita na visima vingi vya mafuta kukaliwa na USA, Turkey na Kurds, Syria inazalisha mapipa 100,000 tu kwa siku huku asilimia 75% ya hayo mapipa yakizalishwa na USA na Kurds.

Waasi wamepambana vita kwa urahisi kwasababu faida ya mafuta hayo ndiyo imetumika kuwafadhili, huku serikali ya Syria ikiwa haina kabisa fedha na inategemea hisani ya Russia na Iran.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba, hata kufika mwaka 2024 tokea mwaka 2011, Assad amejitahidi mno. Kumbuka ukitoa Misri, Syria ndiyo lilikuwa taifa tishio kijeshi kwa Israel. Wengi tunaamini huu ugomvi umeanza 2011, ila ukweli huu ugomvi ulianza 1948 na umechukua sura tofauti mara nyingi. Yom Kippur War 1973 ambayo Israel alipigwa vibaya sana akapona alivyookolewa na Marekani, kinara alikuwa ni Assad Senior. Hivyo kinachoendelea sasa ni mwendelezo tu.

Kuhusu ujasusi, kuna jambo la msingi kabisa ambalo wengi tunaliacha. Mambo haya yote yalianza mwaka 1916 kwenye The Sykes-Picot Agreement, ambapo Britain, France na Russian Empire walikubaliana kuigawa Ottoman Empire kihuni. Wakaanza kuwaunga mkono waarabu ambao walidai uhuru kutoka kwa Ottoman Empire na mwishowe mataifa mengi ya kiarabu, ikiwemo Syria yakazaliwa. Hivyo hili ni eneo ambalo Britain, Marekani, Zionists hawawezi kuliacha tu.

Mwaka 1948, mwaka mmoja mbele baada ya shirika la kijasusi la CIA kuundwa, mapinduzi ya kwanza kabisa yaliyofanywa na CIA yalikuwa ni kupindua serikali ya Syria. CIA walifanya hivyo wakiwa na mikakati ya mbali, maana mwaka huohuo waliunda nchi ya Israel ambayo ndiyo kambi yao kubwa Middle East. Hivyo kuhusu ujasusi, Syria, Hizbullah, Iran, Iraq, Libya na Lebanon hazipambani na MOSSAD tu, zinapambana na CIA, MI6, DIA, NSA, BND, DGSE + THE FIVE EYES ALLIANCE, mashirika makubwa yenye rasilimali nyingi, utaalamu mkubwa na uzoefu wa muda mrefu. Syria taifa lenye watu wasiozidi milioni 25 na rasilimali kidogo lisingeweza kabisa kupambana na hawa watu.

Marekani kabla hajaanza uvamizi wa kijeshi, mbinu yake kubwa ni VIKWAZO kuhakikisha anazorotesha uchumi wako, kisha anakuletea vikundi vya waasi, na mwishowe vita. Iraq, Libya, Afghanistan wote walifanywa hivi kabla ya kuvamiwa. Iran amefanyiwa hivi tokea mwaka 1979, maana bila vikwazo, Iran lingekuwa ni taifa tajiri kuliko hata Saudi Arabia. Marekani hawezi kuruhusu Iran awe tajiri hivyo ni vikwazo mwanzo mwisho.
 
Mataifa karibia yote ya Middle East yametengenezwa na Britain, USA na France hivyo huo umoja ni jambo gumu sana. Pitia, The Sykes-Picot Agreement 1916, The Balfour Declaration 1917 na McMahon Letters to Hussein Bin Ali, The Sherrif of Mecca and Madina. Utafahamu kwamba haya yanayotokea 2014 ni muendelezo wa kile kilichotokea 1917-1924.

Ugunduzi wa mafuta na maamuzi wa Winston Churchill mwaka 1911 kwamba British Navy itaacha kutumia Coal na kuanza kutumia Oil-Power Engines yamechangia kwa kiwango kikubwa huu ukanda kutokuwa na amani. Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa kwamba, Waarabu wana shida, lakini sehemu kubwa hata NATO+EU ni wahandisi wa haya matatizo. Middle East ni kama Congo (DRC), kuwa na amani siyo jambo rahisi.

Kina Nasser, Saddam, Mossadegh, Gaddafi, Ayattollah walijaribu kujitoa kwenye mfumo na umeona nini kiliwakuta. Hivyo ni ngumu mno huu ukanda kuwa na amani ilhali rasilimali zao ndizo zinaendesha dunia. Anachofanyiwa Middle East ndicho Britain na Western Powers wamejaribu kukifanya Russia tokea karne za 19 na 20, lakini bahati mbaya ni kwamba Russia is too powerful.

Yote tisa, muda ndiyo utasema, maana Israel ashaanza kuvamia Syria kwa kupeleka vifaru mpakani. Sasa kama HTS wataweza kuitawala Syria na kuifanya kuwa nchi huru ni jambo la kusubiri tujionee.
 
Bila kusahausevere financial crisis inakuja severe pandemic inakuja so watu wajipange na vita kibao zinakuja pia
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu adolf hitler alijaribu kuiteka urusi akiamini urusi ni heartland ukiikotro urusi basi umeitawala dunia nzima lakini ndo ukawa mwisho wake.
 
Ni kweli Syria haikuwa na njia ya kujitetea kwa muda mrefu ila pia ni uzembe wa hali ya juu kushindwa kujitetea na kiitegemea Iran, Russia na Hezbollah.

Mbona Hamas na Hezbollah wapo na changamoto kubwa ila waliweza kutoa upinzani na limitations zote walizokuwa nazo. Mbona Wagner walikuwa na budget ya kawaida na wapiganaji sio wengi ila impact yao Syria ilikuwa inaonekana na kule Bakhmut walifanya kazi inayoonekana.

Serikali ya Assad na jeshi lake ni wavivu. Hakuna kuwakwepesha lawama.
Assad senior alipigwa na Israel ule mwaka 1973. Unaposema Syria iliipiga Israel unashangaza watu, how comes Syria iliipiga Israel na wakati huohuo Israel ikapokonya Golan heights za Syria?

Mwaka 1970 wakati Hafez al Assad ni senior commander within Syrian Airforce ranks, jeshi lao la ardhini liliishambulia Jordan kwenye Black September. Ingawa Syrian Airforce haikushiriki kwani Jordan iliomba ulinzi wa anga wa Israel endapo Syria italeta ndege zake. Ground offensive Syria ilileta wanajeshi 10,000 wakapigwa na Jordan ambayo muda uleule ilikuwa ikipigana na Wapalestina.

Jordan ikawashinda Wasyria wakarudi kwao, wanamgambo Wapalestina wakapigwa na wengine wakaingia Lebanon kuchafua usalama. Kule wakasababisha civil war mpaka leo nchi haijatulia.

Kwahiyo hakuna wakati wowote kihistoria ambapo modern Syria iliwahi kuwa na jeshi competent. Hata vita ya zamani kwenye caliphates Syria walikuwa mabingwa wa kujisalimisha.

Syria kama nchi haijawahi kuwa tishio kwa Israel, ni tishio kwa kufuga makundi hasimu wa Israel. Hata kwenye airstrikes Israel huwa haijisumbui na jeshi lao dhaifu.
 
Bwana Armata, hili la kulazimisha kwamba Israel alipambana peke yake ilhali tunafahamu kwamba Operation Nickel Grass ndiyo ilibadilisha mwelekeo mzima wa vita ni Propaganda. Richard Nixon Foundation wanasema ndani ya wiki tu, Israel ilipoteza vifaru 500 (Just Imagine). 400 on the Egyptian Front, 100 on the Syrian Front, huku Airforce ikiwa totally depleted.

Ilifika wakati Golda Meir alitaka kutumia nuclear weapons kuitandika Syria as the last option, lakini Henry Kissinger na Richard Nixon waliipeleka silaha nzito kwelikweli ambazo zilibadili mwelekeo mzima wa vita hadi kupelekea waarabu kumwekea Marekani vikwazo, The 1973 Oil Embargo.

Unaposema Syria haijawahi kuwa tishio kwa Israel unapingana na ushahidi wa kihistoria kwamba kuna wakati, Syria na Misri zilikuwa nchi moja, The United Arab Republic iliyotawala hadi GAZA. Namna moja au nyingine, Syria was a vassal of Nasserian Egypt iliyotumika kuvuruga Middle East. Isingekuwa ni tishio wala Golda Meir na Moshe Dayan wasingefikiri kutumia nuclear bombs kutandika Syria.
 
Yote tisa, muda ndiyo utasema, maana Israel ashaanza kuvamia Syria kwa kupeleka vifaru mpakani. Sasa kama HTS wataweza kuitawala Syria na kuifanya kuwa nchi huru ni jambo la kusubiri tujionee.
Syria Democratic Forces walishajitangazia uhuru muda ila Uturuki haiwataki na hawa wnasapotiwa na Marekani na Israel.

HTS wanaonekana kuungwa mkono na kikosi kingine cha waasi wanaoungwa mkono na Uturuki.

SDF hawawaamini hawa HTS ijapokuwa hawa nao wanasapotiwa na Marekani.

Bado mambo ni magumu! Naona hii nchi inaweza ikagawanywa au ikakosa utulivu.
 
Syria ni second Libya naliona hilo kwa mbali kutokana makundi yaliyopo.

HTS wamemuondoa Assad ila bado hawajatawala Syria.
 
Syria ni second Libya naliona hilo kwa mbali kutokana makundi yaliyopo.

HTS wamemuondoa Assad ila bado hawajatawala Syria.
Ni kweli Mkuu!

Natizama Aljazeera hapa naona jumuiya ya kimataifa inawaomba hivyo vikundi vifanye maongezi na vikubaliane namna gani ya kuiendesha nchi.

Kwa akili za waarabu hili suala kwao ni gumu sana! Ila ngoja tuone mambo yatakuwaje!

Mbaya zaidi wameshatengenezeana makundi ya kidini (shia vs sunni).
 

Nakataa kwa dhati kabisa Mkuu! Chokochoko za Lebanon kipindi hiki hazikuanziswa kabisa na NATO! Unajua wazi nini kilitokea October 7! Kwa hiyo Yahyah Sinwar alitumwa na NATO?
 
Ni kweli Mkuu!

Natizama Aljazeera hapa naona jumuiya ya kimataifa inawaomba hivyo vikundi vifanye maongezi na vikubaliane namna gani ya kuiendesha nchi.

Kwa akili za waarabu hili suala kwao ni gumu sana! Ila ngoja tuone mambo yatakuwaje!
Leo hii Libya imegawanywa kila taifa lenye maslahi limechukua upande wake na kusupport kundi lake kila siku vita.

Afghanistan ilieleweka ni Taliban ndio wanapambana kurudisha utawala wao na ndio maana transition of power Afghanistan mpaka leo hakuna mzozo mkubwa kwa Syria hali ni tofauti.

Sidhani kama Israel watakubali kuona Turkey pekee anafurahia mabadiliko haya vivo hivyo kwa Iran,Russia,U.S wote hawa wana maslahi na hilo eneo mmoja wao akilitwaa maana yake wengine wote wamekosa nani kati yao yupo tayari kukubali hili ?

Mimi bado naendelea kuona kuwa HTS bado wapo honeymoon wiki hili acha waendelee kufurahia ushindi kuitawala nchi hapa ndipo ilipo kazi ngumu na yana kumbuka ya Libya.
 
Kama Syria iliipiga Israel kwenye vita ya 1973, kwanini Syria kwenye vita ile ilishindwa kuikomboa Golan heights mpaka leo???

Maana malengo ya Yon Kippur war ni Waarabu kukomboa maeneo yao. Mbona sasa Syria haikukomboa na unasema iliipiga Israel.

Kama Syria ndio ilishinda vita, ilikuwaje majeshi ya Israel yalikuwa deep within Syria yako 40km kutoka mji mkuu Damascus. Ilikuwaje mpaka Henry Kissinger anafanya mazungumzo kushawishi majeshi ya Israel yaondoke Syria?

Kissinger sio aliyeikataza Israel kutumia nuke. Syria hata Jordan river hawakufika sasa nuclear kwao ingekuwa ni overkill, kamati ya usalama ilikataa. Na kama ni suala la misaada hata Syria ilisaidiwa. Iraq ilituma wanajeshi 30,000 vifaru 400 na armoured personnel carriers zaidi ya 600. Bado Jordan iliichangia silaha Syria. Na USSR iliitishia Israel kuwa ikiiteka Damascus basi na jeshi la USSR linaingia vitani. Mbona unafanya as if Syria ilipigana pekee haina allies.
 
SWALI: Je, Mrusi anaweza kukubali kupoteza kambi zake muhimu za kijeshi kule Tartus na kukubali maslahi yake mengine ya kiusalama yapotee kwa kukubali kuachia serikali ya Assad ianguke ???
Swali: Mara baada ya serikali ya Assad kuanguka, nini kinafuata??

Je,huu siyo mchezo wa kutuzuga?? Urusi chukua maeneo Ukraine, achia maeneo Syria tugawane hizo rasilimali!Usile peke yako,tule wote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…