Changamoto wanazopitia vijana wetu mpaka wanakuja na kampeni za kataa ndoa

Kwa nini mnawaza zaidi kuachana badala ya kuwaza kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha? Mnahofia nini hasa?
Kuachana tunawaza kwa sababu ndoa ya cheti ipo kwasababu pia kuna kuachana , kusingekuwa kuna kuachana sizani kama hizo ndoa zingekuwepo.
 
Hakuna anaepinga kuoa na kujenga familia, kinachopingwa ni ndoa, hivi ni kweli hamuelewi au mnagandisha ubongo kwa makusudi?
Ukikaa na mwanamke kwa miezi mitatu na kuendelea kwa sheria za nchi yetu huyo ni mkeo kisheria na ana haki zote za ndoa.
Cheti ni karatasi tu.
Baba zetu kwa asilimia kubwa sana hawakuwahi kuwa na cheti cha ndoa lakini wameishi maisha ya ndoa yaliyotukuka hata uzeeni na kuzikana.
Hivyo kimsingi sijaona unachokataa katika ndoa ilhali umeoa.
 
Kuachana tunawaza kwa sababu ndoa ya cheti ipo kwasababu pia kuna kuachana , kusingekuwa kuna kuachana sizani kama hizo ndoa zingekuwepo.
Tanguliza positivity kila kitu kitaenda sawa.. Tanguliza negativity ndoa itakufa kiroho hata kabla haijafungwa
 
Vijana njoni hapa mtushukuru kwa yote tuliyowaasa.. Imbeni kwa kumaanisha huu wimbo
Your browser is not able to display this video.
 
Kwa nini mnawaza zaidi kuachana badala ya kuwaza kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha? Mnahofia nini hasa?
Wanahofia kugawana mali.
Sasa wengi wa hawa wanaohofia kugawana mali maana mawazo yao ni kuachana na huyo mwanamke hata kabla hawajaanza kuishi pamoja ni wapangaji.
Kwenye nyumba za kupanga kuna vitendea kazi tu kama fanicha na vyombo vya jikoni.
Msingi ukiwa kuachana kupo kisheria m katika mahakama zetu hofu yao ni nini?
Kampeni hii imekaa kiroho zaidi kuliko kifamilia katika mwili. Msingi mkuu wa uumbaji ni familia. Hivyo basi hili ni shambulio lililo silaha ya mwisho na ya juu kabisa ya adui.
 
Hicho ni kisingizio tuu kuna kimoja kikubwa wanaona haya kukisema hadharani wanaogopa kuchekwa na kubezwa
 

Kwa mujibu wa Dini ya Roma Ni kuwa wewe unaishi na hawara.Huna sakrament ya ndoa.Sujui Dini. Zingine zinasemaje.
 
Ni aibu Mwanaume mwenye akili timamu kukataa ndoa kwani ndoa ni ibada, mtu akisema anajipanga kwanza aoe hapo tutaelewa au akisema muda ukifika ataoa hapo sawa lakini wanaokataa ndoa hawana hoja kabisa,

Ni wale jamaa wanaosambaza ushoga TikTok
 
Umeenda mbali ishu zamani walitawalia na mila zilizo mnyima uhuru mwanamke na kumfanya asiwe na maamuz hata anapopitia magumu tofauti na sasa amepewa nguvu kuliko mwanaume na kuvanya ndoa kua ya mafahali wa wili ndo mana zizi (ndoa) hazikaliki
 
Kwani hakuna mashoga waliooa?
Wapo tena wengi yawezekana lakini hawana uhuru
Nikusaidie kifupi sio kama ushoga haukuwepo kabisa way back hapana lakini ulifanyika kwa kificho kikuubwa na ilipobidi kifo.
Sasa sikuhizi wanalazimisha uhuru tunasema hapana hatuutaki
 
Sijasoma maudhui (nimeishia heading pekee) lakini naomba kusema tu kwamba hawa watu hawana changamoto yoyote waliyopitia bali walichoamua ni kueneza kampeni ya kishetani ya uzinzi, ushoga na uasherati. Naam hujasoma vibaya ulichosoma ndo hicho hicho nilichokiandika, kukataa ndoa ni kampeni ya kuhamasisha uzinzi, ushoga na uasherati kwahiyo jichunge sana usije kutekwa na mbinu hiyo
 

Ndoa za siku hizi: Kuzimu kumesimamia ukucha
 
"Tafuta moyo ambao
utakupenda wakati mbaya
zaidi, na mikono ambayo itakushikilia ukiwa dhaifu."

Mke/mume mwema!
 
Ndoa ina miezi 2 anaataka aivunje kwa sababu hayupo tayar kuzaa na mume wake anampangia marafiki hivyo anaona kama alikurupuka[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mnaingia kwenye ndoa ili marafiki waone mmeolewa na hampo tayar kua wake[emoji174][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…