Sehemu ya pili
2.MALEZI kwenye makuzi
Kutokana na utandawazi maendeleo ya tech na harakati za maisha siku hizi wazazi hawana muda wa kukaa na vijana wao na kuwapa ABC za maisha ukikuta familia imekaa pamoja basi kama sio wakati wa chakula basi ni kuangalia tv nk
Maisha ya sasa pia hayatoi nafasi kwa vijana kushiriki shughuli za kujijenga kimwili na kiakili, uwajibikaji nk.. Wazazi, watoto wote wako busy kutafuta maisha na muda kidogo unaopatikina basi unaishia kwenye starehe na mambo yasiyojenga uwajibikaji wala ukomavu wa akili, maono na mitazamo
3. Uchumba wa muda mfupi, ndoa katika umri mdogo, ndoa bila kujiandaa
Kampeni kubwa ya kataa ndoa mifano yake inasababishwa pamoja na mengineyo lakini na hayo hapo juu
Ndoa si kitu cha kukimbilia ni jambo la kuleta muunganiko wa kudumu wa kihisia maono na mapenzi.. Hivyo uchaguzi wa mwenza sahihi sio jambo la dharura
Japo kuna mengine yatagundulika mbele ya safari, lakini walau kaa na mtu si chini ya miaka mitatu, ukichukua muda wa kutosha kumchunguza kwenye kila kitu
Hisia zake kwako
Mapenzi yake kwako
Utayari wake kwako
Maono yake
Kiwango chake cha akili, maarifa na ufahamu
Hamu zake
Tamaa zake
Madhaifu yake nknk
Unaenda mbele zaidi kwa kuangalia background yake hasa kupitia familia yake, ndugu zake jamaa na marafiki
Haya mambo yote yanakuhitaji muda wako wa kutosha tuu.. Usiamini kwa asilimia mia yote anayokuambia kuhusu yeye! Mchunguze mood yake ukiwa huna, ukiwa na stress ukiwa unazo ukiwa na furaha nknk
Vijana wengi hukimbilia ndoa katika umri mdogo.. Ndoa katika umri mdogo nyingi huvunjika baada ya muda mfupi
Ndoa inataka maandalizi hasa na kutambua baadhi ya mambo ya msingi
Unaoa binadamu na sio mnyama wa kufuga ama mdoli..
Uchumba ni tofauti kabisa na ndoa
Mtashare sasa chumba kimoja, kitanda kimoja, nyumba moja kila siku.. Mtaonana kila usiku mnataka hamtaki
Passion of love ikiisha mnabaki na hisia zenyu halisi na hapo sasa ndio ndoa inaanza rasmi
Unaanza kuyaona mapungufu ya mwenzako
Unaanza kumchoka
Unaanza kujilaumu nknk.. Wengi hushindiwa hapa na kukimbilia mitandaoni kulaumu na kuomba ushauri kwa wasio wana ndoa ama walioshindwa kwenye ndoa zao
Ndoa ni ya wawili tuu wa tatu ni Mungu wa nne ni shetani.. Ndani ya hiyo cycle wengine wooote hawahusiki kabisa na kama wakihusika wana mipaka yao
Mwisho wa sehemu ya pili.. Nitaendelea sehemu ya tatu