KERO Changamoto ya Kufungiwa Akaunti – Ajira Portal

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Napenda kuwasilisha malalamiko yangu hadharani kuhusu kufungiwa kwa akaunti yangu katika mfumo wa Mamlaka ya Ajira Tanzania (Ajira Portal) tangu mwezi Septemba 2025, bila kupatiwa maelezo ya kina wala taarifa rasmi inayoeleza sababu za hatua hiyo.

Tangu kufungiwa kwa akaunti hiyo, nimefika ofisini mara kadhaa kufuatilia suala hili kwa njia ya kistaarabu na kwa kuzingatia taratibu. Hata hivyo, hadi sasa hakuna suluhisho lililotolewa wala mrejesho wenye kueleweka kuhusu lini au kwa nini tatizo hili litatatuliwa.

Ikumbukwe kuwa Ajira Portal imeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha usawa, uwazi na upatikanaji wa fursa za ajira kwa Watanzania wote. Kufungiwa kwa akaunti ya mtumiaji bila maelezo ya maandishi wala utaratibu wa rufaa unaoeleweka, kunazua maswali ya msingi kuhusu uwajibikaji, haki na ufanisi wa huduma kwa umma.

Ninaiomba mamlaka husika:
1) Kutoa maelezo rasmi na ya maandishi kuhusu sababu ya kufungiwa kwa akaunti yangu.
2) Kuweka wazi utaratibu wa rufaa kwa watumiaji wanaokumbwa na changamoto kama hii.
3) Kuhakikisha mifumo ya umma inasimamiwa kwa misingi ya haki, uwazi na uwajibikaji kwa wananchi.

Lengo la ujumbe huu si kulalamika bila msingi, bali kutafuta haki na uwazi katika huduma ya umma ambayo inagusa mustakabali wa ajira za vijana wengi.

Natumaini mamlaka husika zitachukua hatua stahiki kwa haraka.
 
IKIWA unaruhusu maoni yetu au msaada wetu (tusio wa mamlaka hiyo)
Naomba uweke screenshot ya maelezo unayopewa kuhusu kufungwa kwa akaunti Yako.Pili,tuwasiliane kwa 0623446608 nikupe msaada wa kimawazo na kitaalamu (binafsi) I hope utasaidika.Asante!
 
Napenda kuwasilisha malalamiko yangu hadharani kuhusu kufungiwa kwa akaunti yangu katika mfumo wa Mamlaka ya Ajira Tanzania (Ajira Portal) tangu mwezi Septemba 2025, bila kupatiwa maelezo ya kina wala taarifa rasmi inayoeleza sababu za hatua hiyo.

Tangu kufungiwa kwa akaunti hiyo, nimefika ofisini mara kadhaa kufuatilia suala hili kwa njia ya kistaarabu na kwa kuzingatia taratibu. Hata hivyo, hadi sasa hakuna suluhisho lililotolewa wala mrejesho wenye kueleweka kuhusu lini au kwa nini tatizo hili litatatuliwa.

Ikumbukwe kuwa Ajira Portal imeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha usawa, uwazi na upatikanaji wa fursa za ajira kwa Watanzania wote. Kufungiwa kwa akaunti ya mtumiaji bila maelezo ya maandishi wala utaratibu wa rufaa unaoeleweka, kunazua maswali ya msingi kuhusu uwajibikaji, haki na ufanisi wa huduma kwa umma.

Ninaiomba mamlaka husika:
1) Kutoa maelezo rasmi na ya maandishi kuhusu sababu ya kufungiwa kwa akaunti yangu.
2) Kuweka wazi utaratibu wa rufaa kwa watumiaji wanaokumbwa na changamoto kama hii.
3) Kuhakikisha mifumo ya umma inasimamiwa kwa misingi ya haki, uwazi na uwajibikaji kwa wananchi.

Lengo la ujumbe huu si kulalamika bila msingi, bali kutafuta haki na uwazi katika huduma ya umma ambayo inagusa mustakabali wa ajira za vijana wengi.

Natumaini mamlaka husika zitachukua hatua stahiki kwa haraka.
Hii story mbona haijakamilika,
Wewe hata huko unapokwenda utapata tabu tubkusaidiwa,
Ebu kua muwazi Nini kilisababisha ukafufungiwa account,
Kuna kitu hutaki kusema
 
Back
Top Bottom