Changamoto ya ulevi: Jinsi inavyoumiza familia na jamii

Mwaka wa 20 huu nakunywa pombe,zamani ilikua ni kila siku lazima nile chombo ...kwa sasa nimepunguza nakunywa wkend tu kwa sababu kazi zinanibana.
Maini na Figo viko safi kama mtoto mdogo ..

Hao ndugu zako wanaoumwa kansa ya koo na maini wambie waache kunywa taputapu
Unaongea nini wewe? Huyu ndugu yangu aliyekufa mwaka jana kwa maradhi mabaya ya ini alikua bingwa wa kumaliza bapa za konyagi na kipindi cha sikukuu akija ilikua friji nzima inajaa bia za kila aina.Amekufa tumemsahau,sasa wewe unaongea nini hapa? Una uhakika gani kua ini na figo zako ziko salama? Nikuulizwe swali jingine moja la msingi,kwanini pombe haipo katika nutritional guide?Jibu.
 
Habari wapendwa,

Leo napenda tuzungumzie hili suala la ulevi na athari zake na jinsi linavyoumiza familia na jamii kwa ujumla.
Wapendwa ulevi ni tabia mbaya ambayo mtu hujijengea taratibu akizani ya kua yupo sawa kumbe anajimaliza siku hadi siku.

Kwa mfano ulevi wa pombe tuache bangi na sigara hivi pia nitavizungumzia mwishoni,sio siri madhara ni makubwa watu hujidangaya kunywa kwa kujilinda na kujipa matumaini kua mfano bia mbili tatu hazitanidhuru lakini ukweli ni kua unapokua katika utumwa huo jua fika unaharibu mwili wako mpendwa, akili zako utajidanganya kua zitakuwa salama zaidi unavyotumia pombe lakini ukweli wa kisayansi ni kua unapelekea kemikali aina ya dopamain kuzalishwa kwa wingi katika ubongo na kupelekea ubongo kuratibu matendo ya mwili vibaya, yaani kupungukiwa utimamu, huu ndio ukweli na uache ukuingie vizuri na uelewe na kubadilika wewe kama mtumiaji

Achilia mbali hizo athari za ubongo lakini ukweli ambao unauma na wengi hujipa matumaini na hawataki kuusikia ni kwamba mwili hau hitaji kemikali ya alcohol na sivyo Mungu alivyokuumba.

Binafsi nilishawahi kua mtu miaji wa vilevi laini kama bia hadi gin na whisky.Ukweli ni kuwa wakati nimeshatumia mwili ulikua ukipata shida hasa mfumo wa upumuaji, ile hali kuhisi hewa kubanwa puani na kuvuta hewa kwa shida.

Athari nyinginezo ni pamoja na kua mjinga mfano kupoteza concentration na mambo yako binafsi huku ukijali na kupigania muda wa unywaji zaidi.

Athari ni nyingine ni kuponea chupuchupu kupata ajali.Mifano niliyoishihudia kwa macho yangu mawili ni vifo kwa upande wa ndugu,mtu aliyekua akisifika kwa kugida chupa za bapa na pombe laini alifariki dunia mwaka jana mwishoni kwa maradhi mabaya ya ini.

Inasikitisha sana wapendwa kuona jinsi jamii inavyoumia na kupoteza nguvu kazi ya taifa katika ulevi, sasa hivi ulevi umekua ni kitu cha kujivuna na kuongeza status yaani kama wewe sio mlevi basi utaonekana mjinga na mpumbavu katikati ya watu na marafiki.

Mimi binafsi nilikua mlevi wa bangi na sigara kwa miaka sita sasa na pombe karibia miaka mitatu,ukweli ni kua hakuna faida niliyopata au cv niliyojenga kutokana matumizi ya vilevi hivyo zaidi yake ni hasara,kupoteza heshima na uhusiano wangu na familia na jamii kwa ujumla.

Nakusihi mpendwa kama wewe sio mtumiaji mwombe sana Mungu kwa kunia usiingie katika mtego huu ni hatari mno mno na tena mno kwa maisha yako mazuri hadi uzeeni, na kwa wale watumiaji jitahidi uache mara moja maana inawezekana mtu asikudanye kua eti punguza kidogo kidogo huo ni uongo na ni ngumu kuacha kwa namna hiyo,mimi binafsi ni shahidi na niliacha vyote mara moja kirahisi tu.

View attachment 2591129

Nakaribisha maswali.
Hiyo 'Paragraph' ya mwisho hapo ulipoandika tu neno 'mpendwa' nikajua chuki yako kwa walevi iko namna gani! Shikilia tu unachoamini, haya maisha mengine waachie wengine. Figo ni zao, utimamu wa hovyo ni wao, pia pesa ni zao!
 
Ni mzuri na mbaya pia
What a joke! Yaani pombe ni nzuri halafu tena ni mbaya pia? Hahaha umeona jinsi ulivyojikanyaga mwenyewe?Umeshaishiwa hoja, yaani ni hivi kitu kibaya siku zote ni sawa na uongo, ukiwekwa hadharani ni aibu na fundisho.
 
😂😂
 
Kama pombe ni nzuri kwanini haipo katika nutritional guide jibu haraka hapa.
Alcohol is not food!!
You don't need it!
You can live without it!

Especially if you misbehave when you drink it then you should definitely live without it.

I just googled it, wamei classify kama dawa!

So you see, you can have your strong ginger tea daily as dawa and I can have just one glass of wine for the same.

images (62).jpeg
 
Hiyo 'Paragraph' ya mwisho hapo ulipoandika tu neno 'mpendwa' nikajua chuki yako kwa walevi iko namna gani! Shikilia tu unachoamini, haya maisha mengine waachie wengine. Figo ni zao, utimamu wa hovyo ni wao, pia pesa ni zao!
"Figo ni zao,utimamu wa hovyo ni wao, pia pesa nia zao".mwisho wa kunukuu,sasa ni hivi, ukweli lazima usemwe na kitu kibaya lazima kipingwe na kiwekwe hadharani na iwe fundisho full stop.
 
Alcohol is not food!!
You don't need it!
You can live without it!

Especially if you misbehave when you drink it then you should definitely live without it.

I just googled it, wamei classify kama dawa!

So you see, you can have your strong ginger tea daily as dawa and I can have just one glass of wine for the same.

View attachment 2594096
Achana hizo perepeche zako ulizoandika hapo.The simple answer is if its not included in the nutritional guide then that means its harmful for your health full stop.
 
That's a "false dilemma" over there. If it's not listed in foods then it's Poison!

Nishakwambia imekuwa listed kama dawa (a depressant), Hii mitishamba tunayokula ni harmful kisa haijaandikwa kwenye nutrition guide?

Sikia you ex alcoholic, pole kwa kuteswa na pombe na hongera kwa kuacha na usirudie kunywa, usituletee mabalaa

stupid-drunk-girls-day.gif
 
View attachment 2594130
Huyu mjinga hatuache sisi tunywe beer hapa nimepata arosto tayari
 
Kuacha inawezekana na ni rahisi mno kama ukiamua kunia mamoja na kumwogopa Mungu.Mbona mimi nimeacha vyote kirahisi tu na nafurahia maisha zaidi ya hapo mwanzo, mimi bangi nimevuta hadi kuotesha na kuvuna for myself use only sio kuuza nimeitumia for almost 6 years,beer,gin na wisky kwa miaka 3, vyote nimeviacha kirahisi tu na sasa niko huru.
Oh kumbe pombe umetumia kwa miaka mitatu tu na ukafanikiwa kuacha? Sisi tunaongelea ambao tumekuwa kwenye matumizi hayo zaidi ya miaka 20 sasa. Sikatai kila kitu starts with NIA
Asante
 
Kwahiyo hapo ndipo akili yako ilipofikiria na kufikia mwisho?
Enjoy maisha jinsi uwezavyo mkuu, utakwepa pombe utakufa na mambo mengine. Risk is everywhere and we all do take risk everyday, knowingly or unknowingly! Cheers🍻🥂
 
Acha kupotosha watu dopemine sio athari za ubongo hiyo ni moja ya kazi ya ubongo ya kawaida tu pale unapofanya kitu chochote cha kukufurahisha hiyo chemical inakua released kwenye ubongo wako ili ujiskie vizuri mfano sex au kula kitu chochote ambacho wewe unakipenda , na ndio inaleta kitu kinaitwa addiction pale unapozidisha matumizi ya kitu

Na kunywa pombe ni entertainment, mtu anaweza chagua kitu chochote cha kufanya ili ajipe entertainment

Madhara yapo kwenye kila kitu as long as ume tumia kupita kiasi hivyo cha msingi ni kutumia vitu kwa level sawa hata kama sio pombe
 
Lahasha, mimi nilikua nanunua kwa bajeti yangu nzuri tu sio kwa pupa, nilicho kuja kugundua niku nilivyokua mwanzo sivyo nilivyokua baada ya vilevi vyote hivyo bangi kwa miaka 6, beer,whisky na gin kwa miaka 3, ukweli ndio huo nilijiona kua nipo gizani na kifungoni pia nikatoka huko kirahisi tu ndugu.

Labda nikuulize swali hapa..!!

Nini kilianza??
1. Kuvuta bangi kwa miaka 6 bila kutumia pombe kabisa halafu baadae ndo ukaanza pombe kwa miaka mi3? Au

2. Kuvuta bangi na pombe kwa pamoja, halafu baadae ukaacha bangi na kuendelea kunywa pombe kwa miaka mitatu..??

Maana ya maswali yangu ni kwamba; kama ulifanya vyote viwili kwa pamoja, na wala hujatuambia kiwango cha pombe ulichokuwa unakunywa na kiwango cha bangi ulichokuwa unavuta, basi UNA HAKI KABISA YA KUSEMA HAYA UNAYOSEMA…!!!

Na pia ikumbukwe kwamba KUTOKUNYWA POMBE SIO KIPIMO CHA KUWA MWEREVU kwa sababu wapo wasiokunywa na bado akili zao ni mbovu tu.

Ahsante…!!
 
walevi hovyo sana wanajazana ujinga bar mimi hupenda kwenda bar kupata mchemsho au juice huku nacheki mpira ukiwasikiliza mipango yao ya pesa wakiwa wamelewa na asubui wanavyo kwepana utacheka sana
Naenda kupataga mchemsho wa samaki pale small planet 16k walevi wanakaaga mbali na meza yangu
 
Habari wapendwa,

Leo napenda tuzungumzie hili suala la ulevi na athari zake na jinsi linavyoumiza familia na jamii kwa ujumla.
Wapendwa ulevi ni tabia mbaya ambayo mtu hujijengea taratibu akizani ya kua yupo sawa kumbe anajimaliza siku hadi siku.

Kwa mfano ulevi wa pombe tuache bangi na sigara hivi pia nitavizungumzia mwishoni,sio siri madhara ni makubwa watu hujidangaya kunywa kwa kujilinda na kujipa matumaini kua mfano bia mbili tatu hazitanidhuru lakini ukweli ni kua unapokua katika utumwa huo jua fika unaharibu mwili wako mpendwa, akili zako utajidanganya kua zitakuwa salama zaidi unavyotumia pombe lakini ukweli wa kisayansi ni kua unapelekea kemikali aina ya dopamain kuzalishwa kwa wingi katika ubongo na kupelekea ubongo kuratibu matendo ya mwili vibaya, yaani kupungukiwa utimamu, huu ndio ukweli na uache ukuingie vizuri na uelewe na kubadilika wewe kama mtumiaji

Achilia mbali hizo athari za ubongo lakini ukweli ambao unauma na wengi hujipa matumaini na hawataki kuusikia ni kwamba mwili hau hitaji kemikali ya alcohol na sivyo Mungu alivyokuumba.

Binafsi nilishawahi kua mtu miaji wa vilevi laini kama bia hadi gin na whisky.Ukweli ni kuwa wakati nimeshatumia mwili ulikua ukipata shida hasa mfumo wa upumuaji, ile hali kuhisi hewa kubanwa puani na kuvuta hewa kwa shida.

Athari nyinginezo ni pamoja na kua mjinga mfano kupoteza concentration na mambo yako binafsi huku ukijali na kupigania muda wa unywaji zaidi.

Athari ni nyingine ni kuponea chupuchupu kupata ajali.Mifano niliyoishihudia kwa macho yangu mawili ni vifo kwa upande wa ndugu,mtu aliyekua akisifika kwa kugida chupa za bapa na pombe laini alifariki dunia mwaka jana mwishoni kwa maradhi mabaya ya ini.

Inasikitisha sana wapendwa kuona jinsi jamii inavyoumia na kupoteza nguvu kazi ya taifa katika ulevi, sasa hivi ulevi umekua ni kitu cha kujivuna na kuongeza status yaani kama wewe sio mlevi basi utaonekana mjinga na mpumbavu katikati ya watu na marafiki.

Mimi binafsi nilikua mlevi wa bangi na sigara kwa miaka sita sasa na pombe karibia miaka mitatu,ukweli ni kua hakuna faida niliyopata au cv niliyojenga kutokana matumizi ya vilevi hivyo zaidi yake ni hasara,kupoteza heshima na uhusiano wangu na familia na jamii kwa ujumla.

Nakusihi mpendwa kama wewe sio mtumiaji mwombe sana Mungu kwa kunia usiingie katika mtego huu ni hatari mno mno na tena mno kwa maisha yako mazuri hadi uzeeni, na kwa wale watumiaji jitahidi uache mara moja maana inawezekana mtu asikudanye kua eti punguza kidogo kidogo huo ni uongo na ni ngumu kuacha kwa namna hiyo,mimi binafsi ni shahidi na niliacha vyote mara moja kirahisi tu.

View attachment 2591129

Nakaribisha maswali.
Weweee usitutishe bwana! Mbona wengine tunachangia tumekunywa na huwezi ona tofauti kati ya aliyetoka Kanisani au Msikitini na sisi tulio baa Sasa hivi?
 
Kwahiyo mnywaji yeye anakunywa ili asilewe sio?Yaani sio kulewa ni kunywa tu kama soda au maji au analenga kupoteza utimamu wake na kulewa? Usijidanganye lengo la kunywa pombe kwa chupa moja ya bia au glasi ya mvinyo lengo kuu ni kulewa na si vinginevyo hana tofauti na mlevi mwingine yeyote.
Uhuru wa kuishi ni mapamoja na kuchagua aina ya maisha, Wanywapombe hawana SHIDA. SHIDA INALETWA NA WALEVI. Tu upige vita ulevi.
 
Back
Top Bottom