Maslahi yapi? Hayo ndio maelezo ya watu wa Tanesco na mie siko TanescoWewe bila shaka utakuwa unatokea tanesco. Umejitahidi kutetea masilahi yenu lakini wala haujaeweka unachokibishi.
Huu Ni ukweli mchungu,Ni ujinga tuu wa yule jamaa yenu.Endapo hela zilizotumika Mwalimu Nyerere zingewekezwa kwenye gas turbines hakika tungepata umeme mwingi sana
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kwa nini basi yasiendelezwe haya mabwawa yaliyopo, mfano Kihansi, Mtera hata na Hale?Jpm hakuendelea na gesi? Katika kipindi chake matumizi ya gesi kuzalisha umeme yaliongezeka kuliko vyanzo vingine.
Alichofanya ni kuongeza sources tu za umeme Kama hilo bwawa. Kutegemea gesi tu bila kuwa na mbadala ni hatari sana. Gesi sio renewable. Maji ni renewable. Hivyo alifanya sawa.
Ama kweli CCM ni janga kubwa kwa taifa hili. Na mnakiri kabisa utopolo wenu 🙆🙆🙆Harafu acha upotoshaji wa kipumbavu..
Awamu ya 3 ya Mkapa ulitaka kubinafsisha Tanesco so uamzi wa mwisho haukufikiwa ndani Baraza la Mawaziri baadae wakaja wakafuta huo mpango na kufanya modernisation ya management ya Tanesco ila kwa Miaka yote ile ya mchakato wa ubinafsishaji Hakuna uwekezaji mpya wa Serikali uliofanywa kwa sababu ya hiyo sintofahamu..
JK alirithi Nchi ikiwa Hakuna Tanesco yenye vyanzo vipya vya umeme na Uchumi unajua so tunrescue situation ndipo Sasa mitambo ya mafuta almaarufu majenereta ikakodiwa na kuketwa maana huwezi kaa bila umeme huku wakiendelea na uwekezaji wa umeme wa Gas..
So Hadi anaondoka Madarakani Umeme wa gas ndio ukawa na proportion kubwa kwenye energy mix ya 63%.
Mwendazake akaja akaishia kupuuza gas na kuanza mradi wa bwawa ambao haujulikani ungeisha lini,Miaka 5 ikapita bwawa liko 30%.
Amekuja Rais Samia akakutana na Hali Kama ya aliyoikuta JK, mvua zikapungua umeme wa maji ukapungua na gas ilipuuzwa , Sasa kaongeza Pesa Wizara ya Nishati ili kupata umeme wa gas wakati wanaendela na kukomaa na bwawa..
Naomba hapa muelewe awamu ya 4 haitaki.kuzima Moto inaenda na ufumbuzi wa kudumu,bwawa litakuwepo na gas na vyanzo vinginevyo vitaanzishwa ili kuanzia 2026 huko walau kazi ibaki ya mainatanance na sio generation.
Tena ili kukwepa usafirishaji wa gesi kutumia bomba.Huu Ni ukweli mchungu,Ni ujinga tuu wa yule jamaa yenu.
Hayo bado hayawezi kuzalisha megawatt nyingi. Kumbuka mahitaji yetu hadi kufikia 2030 yaatakua zaidi ya megawatt 2000. Hivyo hakuna namna bwawa jipya ilikua lazimaKwa nini basi yasiendelezwe haya mabwawa yaliyopo, mfano Kihansi, Mtera hata na Hale?
Capacity ya Kihansi ni 300 MW lakini sasa imewekewa mitambo ya 180, nimewahi kutembelea Hale na Mtera mitambo yake duh! ya mwaka 47! Imechoka hatari.
Kuendelezwa kwake maana yake waondoe tope lote kwa kufunga maji yasitiririke kwa muda fulani.Kwa nini basi yasiendelezwe haya mabwawa yaliyopo, mfano Kihansi, Mtera hata na Hale?
Capacity ya Kihansi ni 300 MW lakini sasa imewekewa mitambo ya 180, nimewahi kutembelea Hale na Mtera mitambo yake duh! ya mwaka 47! Imechoka hatari.
Kulipia bomba liwe letu alafu gesi unaendelea kununua kwa mwekezaji bado ni kazi bure. Wengi hadi sasa hamuelewi vizuri, kutegemea chanzo Cha umeme Cha kununua kwa mwekezaji ni jambo la ajabu. Labda ungesema tutafute pesa zaidi alqfu hiyo gesi tuanze kuchimba wenyeweTena ili kukwepa usafirishaji wa gesi kutumia bomba.
Tungejenga station ya kuzalisha umeme huko huko Mtwara, afu transmission line zilete umeme huku. Hii ingesababisha bei kuwa ndogo maana tungekwepa tumia bomba.
Au tungelipa mkopo wote wa bomba tulimiliki liwe letu
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ili uchimbe inabidi ufanye utafiti utafiti ni bahati nasibu.Kulipia bomba liwe letu alafu gesi unaendelea kununua kwa mwekezaji bado ni kazi bure. Wengi hadi sasa hamuelewi vizuri, kutegemea chanzo Cha umeme Cha kununua kwa mwekezaji ni jambo la ajabu. Labda ungesema tutafute pesa zaidi alqfu hiyo gesi tuanze kuchimba wenyewe
Mimi sikatai kwamba bwawa jipya ilikuwa lazima, lakini lilihitaji proper planning na hesabu hasa za matumizi ya maji, kwani mto rufiji unategemewa na viumbehai wengi sana kwa hivyo impacts za kuzuia maji kwenye bwawa zilitakiwa zifanyiwe kazi vizuri. Sisi kama wananchi tunataka kitu sustainable siyo bwawa limejengwa halafu hakuna maji ya kujaza.Hayo bado hayawezi kuzalisha megawatt nyingi. Kumbuka mahitaji yetu hadi kufikia 2030 yaatakua zaidi ya megawatt 2000. Hivyo hakuna namna bwawa jipya ilikua lazima
Gesi sio renewable, kuwekeza pekee huko ni hasara kubwa mno. Kwa nchi yetu hii ambayo tuna renewable sources nyingi ni ajabu sana kuziacha na kutumia nguvu kwenye gesi. Hata hivyo gesi bado tunainunua kwa gharama kubwa toka kwa mwekezajiEndapo hela zilizotumika Mwalimu Nyerere zingewekezwa kwenye gas turbines hakika tungepata umeme mwingi sana
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hizi story za bwawa hupotoshwa na wale ambao walikuwa hawataki ni Kama story za gesi pia wale walikua hawataki walipotosha.Mimi sikatai kwamba bwawa jipya ilikuwa lazima, lakini lilihitaji proper planning na hesabu hasa za matumizi ya maji, kwani mto rufiji unategemewa na viumbehai wengi sana kwa hivyo impacts za kuzuia maji kwenye bwawa zilitakiwa zifanyiwe kazi vizuri. Sisi kama wananchi tunataka kitu sustainable siyo bwawa limejengwa halafu hakuna maji ya kujaza.
Ni kweli. Hiyo gesi si yetu tena. Tulishanyang'anywa kitambo na mabepari aka wawekezaji kupitia mikataba mibovu ya miaka mia kama walivyotakaGharama za uzalishaji usifikiri gesi ni bure, inanunuliwa kutoka kwa mwekezaji
Mie nawaza tu ikiwa sa hivi ni msimu wa mvua lakini maji ya kuzalisha umeme bwawani tunaambiwa hakuna je ikifika kiangazi itakuwaje?Awamu ya baba wa taifa na ile ya mzee ruhusa hakukuwa na changamoto la katika katika kwa umeme maeneo ambayo huduma hii ilikuwa imeyafikia. Ni kweli kwamba maeneo hayo yalikuwa hasa kwenye miji mikubwa ya nchi. Shughuli za kiuchumi wa viwanda hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa ambapo tumesambaza huduma hii ya umeme hadi kwenye karibu kila kijiji.
Jinsi uchumi wa viwanda ulivyozidi kukua na idadi ya watu kuongezeka, ndivyo changamoto ya umeme ilivyojitokeza na kukua kila kukicha. Zilianza hasa katika kipindi cha awamu ya tatu ya Mzee Mkapa ambaye suluhisho lake lilikuwa ni kuwapa kampuni ya makaburu wa South Africa kutuendeshea Tanesco yetu. Matokeo yake hatutayasahau. Tulipigwa tukapigika.
Ikaja awamu ya nne ya Mzee Kikwete. Wao wakaona suluhisho lake ni kukodi majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka makampuni ya nje ya nchi kama yale ya Richmond, Dowans, Symbion na IPTL. Tukapigwa na kupigika hadi Waziri mkuu akatimuliwa na bunge la Mzee Sitta.
Ikaja awamu ya tano ya Mzee Magufuli. Nayo ikahangaika kwa kubana mafisadi na kuanzisha mahakama ya mafisadi kama suluhisho la changamoto hili la umeme. Kwa kiasi fulani kukawa na ahueni ya kuonesha kuwa ile ndoto ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025 labda ingaliweza kutimia.
Sasa imekuja awamu ya sita ya Mama yetu Mzee Salmia inayopenda kushirikisha wananchi wote kupata suluhisho la changamoto mbali mbali ya wananchi kidemokrasia. Kwa kuwa umeme wa bei rahisi kuliko wote ni ule unaotokana na maji. Na kwa kuwa nchi yetu imejariwa mito mingi na kuzungukwa na maziwa makubwa makubwa mengi: kwa nini maji ya ziwa kama lile la Victoria yasipekwe kwa mabomba huko kwenye bwawa la Mtera na lile la Nyerere ili wakati wa ukame kwenye mabwawa hayo, yakafunguliwa kuyajaza? Ethiopia wanatumia maji ya ziwa Victoria kupitia mto Nile kuzalisha maelfu ya maelfu ya MW za umeme hadi kuwauzia Wakenya.
Kwanini sisi tusitumie Ziwa hili ambalo liko kwetu? Kwani ni shilingi ngapi kupeleka maji ya ziwa letu huko? Kama hatuna hizo hela, tutafute pa kukopa kwani manufaa ya mkopo huu ni mkubwa sana. Hili litakuwa ni suluhisho la once and for all ya changamoto hili la umeme.
Tutaweza hata kuuza umeme nje ya nchi na kuachana na kuuza mahindi na mchele nje ya nchi wakati tukiwa tuna njaa. Tutaweza kupunguza sana bei ya umeme ili wananchi wote waweze kuitumia kama nishati rahisi ya kupikia na hivyo kuachana na ukataji wa miti wakitafuta kuni na mkaa. Mwananchi ataweza kutumia shilingi zisizozidi elfu tano tu kwa mwezi kwa nishati ya kupikia ya umeme.
Tanesco nao wataweza kukusanya matrilioni ya pesa kwani kila mwananchi atakuwa mteja wao. Viwanda vingi vitajengwa na kuzalisha bidhaa nyingi kwa bei nafuu. Kwa muda mfupi nchi yetu itakuwa upper middle income country chini ya uangalizi wa mama!
NB: Umeme utokanao na gesi mara zote bei yake ni ya juu sana (unaffordable to many of our people) ukilinganishwa na ule unaotokanq na maji. Umeme wa gesi ni kwa wakati wa dharura tu au kwa kuuza nje.
Kwani zile ndege zetu hazipo?How? Maji ya Ziwa Victoria yapelekwe Kidatu na Mtera! .Hivi somo la Geography lilifutwa?
Sababu zao ni kigeugeu tu. Kiangazi utaambiwa kuna ukame, sijui ni kiangazi gani ambacho huwa hakina ukame, au definition ya kiangazi kwa tanesco siyo ile tunayoijua sisi. Wakati wa masika na mvua zikileta mafuriko maeneo mbali mbali ya nchi, tanesco watasema mabwawa yao hayana maji kwa sababu ya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vyake vya maji. Utadhani hizo shughuli za kibinadamu zimeanza leo. Kwa nini hizi shughuli za kibinadamu hazizuii haya mafuriko bali zinazuia tu maji kutoingia kwenye mabwawa ya tanesco. JPM alituambia kuwa mabwawa haya huwa yanafunguliwa kuchepusha maji yasijae.Mie nawaza tu ikiwa sa hivi ni msimu wa mvua lakini maji ya kuzalisha umeme bwawani tunaambiwa hakuna je ikifika kiangazi itakuwaje?
Si ndo itakuwa mgao wa week kwa week
Duh, sijaelewaAwamu ya baba wa taifa na ile ya mzee ruhusa hakukuwa na changamoto la katika katika kwa umeme maeneo ambayo huduma hii ilikuwa imeyafikia. Ni kweli kwamba maeneo hayo yalikuwa hasa kwenye miji mikubwa ya nchi. Shughuli za kiuchumi wa viwanda hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa ambapo tumesambaza huduma hii ya umeme hadi kwenye karibu kila kijiji.
Jinsi uchumi wa viwanda ulivyozidi kukua na idadi ya watu kuongezeka, ndivyo changamoto ya umeme ilivyojitokeza na kukua kila kukicha. Zilianza hasa katika kipindi cha awamu ya tatu ya Mzee Mkapa ambaye suluhisho lake lilikuwa ni kuwapa kampuni ya makaburu wa South Africa kutuendeshea Tanesco yetu. Matokeo yake hatutayasahau. Tulipigwa tukapigika.
Ikaja awamu ya nne ya Mzee Kikwete. Wao wakaona suluhisho lake ni kukodi majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka makampuni ya nje ya nchi kama yale ya Richmond, Dowans, Symbion na IPTL. Tukapigwa na kupigika hadi Waziri mkuu akatimuliwa na bunge la Mzee Sitta.
Ikaja awamu ya tano ya Mzee Magufuli. Nayo ikahangaika kwa kubana mafisadi na kuanzisha mahakama ya mafisadi kama suluhisho la changamoto hili la umeme. Kwa kiasi fulani kukawa na ahueni ya kuonesha kuwa ile ndoto ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025 labda ingaliweza kutimia.
Sasa imekuja awamu ya sita ya Mama yetu Mzee Salmia inayopenda kushirikisha wananchi wote kupata suluhisho la changamoto mbali mbali ya wananchi kidemokrasia. Kwa kuwa umeme wa bei rahisi kuliko wote ni ule unaotokana na maji. Na kwa kuwa nchi yetu imejariwa mito mingi na kuzungukwa na maziwa makubwa makubwa mengi: kwa nini maji ya ziwa kama lile la Victoria yasipekwe kwa mabomba huko kwenye bwawa la Mtera na lile la Nyerere ili wakati wa ukame kwenye mabwawa hayo, yakafunguliwa kuyajaza? Ethiopia wanatumia maji ya ziwa Victoria kupitia mto Nile kuzalisha maelfu ya maelfu ya MW za umeme hadi kuwauzia Wakenya.
Kwanini sisi tusitumie Ziwa hili ambalo liko kwetu? Kwani ni shilingi ngapi kupeleka maji ya ziwa letu huko? Kama hatuna hizo hela, tutafute pa kukopa kwani manufaa ya mkopo huu ni mkubwa sana. Hili litakuwa ni suluhisho la once and for all ya changamoto hili la umeme.
Tutaweza hata kuuza umeme nje ya nchi na kuachana na kuuza mahindi na mchele nje ya nchi wakati tukiwa tuna njaa. Tutaweza kupunguza sana bei ya umeme ili wananchi wote waweze kuitumia kama nishati rahisi ya kupikia na hivyo kuachana na ukataji wa miti wakitafuta kuni na mkaa. Mwananchi ataweza kutumia shilingi zisizozidi elfu tano tu kwa mwezi kwa nishati ya kupikia ya umeme.
Tanesco nao wataweza kukusanya matrilioni ya pesa kwani kila mwananchi atakuwa mteja wao. Viwanda vingi vitajengwa na kuzalisha bidhaa nyingi kwa bei nafuu. Kwa muda mfupi nchi yetu itakuwa upper middle income country chini ya uangalizi wa mama!
NB: Umeme utokanao na gesi mara zote bei yake ni ya juu sana (unaffordable to many of our people) ukilinganishwa na ule unaotokanq na maji. Umeme wa gesi ni kwa wakati wa dharura tu au kwa kuuza nje.
Akili hizi we ukipewa nchi, lazima tuingie kwenye vita na wamisriAwamu ya baba wa taifa na ile ya mzee ruhusa hakukuwa na changamoto la katika katika kwa umeme maeneo ambayo huduma hii ilikuwa imeyafikia. Ni kweli kwamba maeneo hayo yalikuwa hasa kwenye miji mikubwa ya nchi. Shughuli za kiuchumi wa viwanda hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa ambapo tumesambaza huduma hii ya umeme hadi kwenye karibu kila kijiji.