Changamoto ya umeme nchini ilianza na Awamu ya Tatu, sasa ni mbaya zaidi. Kwanini maji ya Ziwa Victoria yasipelekwe hadi Mtera na JNHPP kupata suluhu?

Jpm hakuendelea na gesi? Katika kipindi chake matumizi ya gesi kuzalisha umeme yaliongezeka kuliko vyanzo vingine.

Alichofanya ni kuongeza sources tu za umeme Kama hilo bwawa. Kutegemea gesi tu bila kuwa na mbadala ni hatari sana. Gesi sio renewable. Maji ni renewable. Hivyo alifanya sawa.
Kwa nini basi yasiendelezwe haya mabwawa yaliyopo, mfano Kihansi, Mtera hata na Hale?

Capacity ya Kihansi ni 300 MW lakini sasa imewekewa mitambo ya 180, nimewahi kutembelea Hale na Mtera mitambo yake duh! ya mwaka 47! Imechoka hatari.
 
Harafu acha upotoshaji wa kipumbavu..

Awamu ya 3 ya Mkapa ulitaka kubinafsisha Tanesco so uamzi wa mwisho haukufikiwa ndani Baraza la Mawaziri baadae wakaja wakafuta huo mpango na kufanya modernisation ya management ya Tanesco ila kwa Miaka yote ile ya mchakato wa ubinafsishaji Hakuna uwekezaji mpya wa Serikali uliofanywa kwa sababu ya hiyo sintofahamu..

JK alirithi Nchi ikiwa Hakuna Tanesco yenye vyanzo vipya vya umeme na Uchumi unajua so tunrescue situation ndipo Sasa mitambo ya mafuta almaarufu majenereta ikakodiwa na kuketwa maana huwezi kaa bila umeme huku wakiendelea na uwekezaji wa umeme wa Gas..

So Hadi anaondoka Madarakani Umeme wa gas ndio ukawa na proportion kubwa kwenye energy mix ya 63%.

Mwendazake akaja akaishia kupuuza gas na kuanza mradi wa bwawa ambao haujulikani ungeisha lini,Miaka 5 ikapita bwawa liko 30%.

Amekuja Rais Samia akakutana na Hali Kama ya aliyoikuta JK, mvua zikapungua umeme wa maji ukapungua na gas ilipuuzwa , Sasa kaongeza Pesa Wizara ya Nishati ili kupata umeme wa gas wakati wanaendela na kukomaa na bwawa..

Naomba hapa muelewe awamu ya 4 haitaki.kuzima Moto inaenda na ufumbuzi wa kudumu,bwawa litakuwepo na gas na vyanzo vinginevyo vitaanzishwa ili kuanzia 2026 huko walau kazi ibaki ya mainatanance na sio generation.
Ama kweli CCM ni janga kubwa kwa taifa hili. Na mnakiri kabisa utopolo wenu 🙆🙆🙆
 
Huu Ni ukweli mchungu,Ni ujinga tuu wa yule jamaa yenu.
Tena ili kukwepa usafirishaji wa gesi kutumia bomba.
Tungejenga station ya kuzalisha umeme huko huko Mtwara, afu transmission line zilete umeme huku. Hii ingesababisha bei kuwa ndogo maana tungekwepa tumia bomba.
Au tungelipa mkopo wote wa bomba tulimiliki liwe letu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini basi yasiendelezwe haya mabwawa yaliyopo, mfano Kihansi, Mtera hata na Hale?

Capacity ya Kihansi ni 300 MW lakini sasa imewekewa mitambo ya 180, nimewahi kutembelea Hale na Mtera mitambo yake duh! ya mwaka 47! Imechoka hatari.
Hayo bado hayawezi kuzalisha megawatt nyingi. Kumbuka mahitaji yetu hadi kufikia 2030 yaatakua zaidi ya megawatt 2000. Hivyo hakuna namna bwawa jipya ilikua lazima
 
Kuendelezwa kwake maana yake waondoe tope lote kwa kufunga maji yasitiririke kwa muda fulani.

Waweke turbines mpya, generators mpya.
Hiyo ni gharama kuliko kununua generators za gas

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Tena ili kukwepa usafirishaji wa gesi kutumia bomba.
Tungejenga station ya kuzalisha umeme huko huko Mtwara, afu transmission line zilete umeme huku. Hii ingesababisha bei kuwa ndogo maana tungekwepa tumia bomba.
Au tungelipa mkopo wote wa bomba tulimiliki liwe letu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kulipia bomba liwe letu alafu gesi unaendelea kununua kwa mwekezaji bado ni kazi bure. Wengi hadi sasa hamuelewi vizuri, kutegemea chanzo Cha umeme Cha kununua kwa mwekezaji ni jambo la ajabu. Labda ungesema tutafute pesa zaidi alqfu hiyo gesi tuanze kuchimba wenyewe
 
Ili uchimbe inabidi ufanye utafiti utafiti ni bahati nasibu.

Bomba twalipia dollar kadhaa kwa kila cbm 1, na bado hatuitumii gesi hata kwa asilimia 20 ya uwezo wa bomba, hivyo hii husababisha muda wa kulipa kuwa mrefu ukijumlisha mfumko wa bei twajikuta twalipa hela nyingi sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hayo bado hayawezi kuzalisha megawatt nyingi. Kumbuka mahitaji yetu hadi kufikia 2030 yaatakua zaidi ya megawatt 2000. Hivyo hakuna namna bwawa jipya ilikua lazima
Mimi sikatai kwamba bwawa jipya ilikuwa lazima, lakini lilihitaji proper planning na hesabu hasa za matumizi ya maji, kwani mto rufiji unategemewa na viumbehai wengi sana kwa hivyo impacts za kuzuia maji kwenye bwawa zilitakiwa zifanyiwe kazi vizuri. Sisi kama wananchi tunataka kitu sustainable siyo bwawa limejengwa halafu hakuna maji ya kujaza.
 
Endapo hela zilizotumika Mwalimu Nyerere zingewekezwa kwenye gas turbines hakika tungepata umeme mwingi sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Gesi sio renewable, kuwekeza pekee huko ni hasara kubwa mno. Kwa nchi yetu hii ambayo tuna renewable sources nyingi ni ajabu sana kuziacha na kutumia nguvu kwenye gesi. Hata hivyo gesi bado tunainunua kwa gharama kubwa toka kwa mwekezaji
 
Mimi sikatai kwamba bwawa jipya ilikuwa lazima, lakini lilihitaji proper planning na hesabu hasa za matumizi ya maji, kwani mto rufiji unategemewa na viumbehai wengi sana kwa hivyo impacts za kuzuia maji kwenye bwawa zilitakiwa zifanyiwe kazi vizuri. Sisi kama wananchi tunataka kitu sustainable siyo bwawa limejengwa halafu hakuna maji ya kujaza.
Hizi story za bwawa hupotoshwa na wale ambao walikuwa hawataki ni Kama story za gesi pia wale walikua hawataki walipotosha.

Mradi ni 2% tu ya eneo lote. Sasa hao viumbe wanakosaje kutumia hayo maji?
 
Gharama za uzalishaji usifikiri gesi ni bure, inanunuliwa kutoka kwa mwekezaji
Ni kweli. Hiyo gesi si yetu tena. Tulishanyang'anywa kitambo na mabepari aka wawekezaji kupitia mikataba mibovu ya miaka mia kama walivyotaka
kufanya kwenye bandari yetu ya Bagamoyo. Wanaimiliki kwa asilimia 100% (by JPM), wao ndiyo wanatuuzia kwa bei wanayoitaka wao. Mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao unatosha siku 7 tu za kupikia maharage ya familia ya watu saba, unauzwa TSH 60,000. Unit moja ya umeme majumbani tunauziwa TSH 400 na wanania ya kuipandisha. Yaani maharage ya Sh 1,000 unayapika kwa Sh 2,000 (bei ya Kilowatt-hour 5). Jumla inakuwa Sh 3,000 ambayo ingalitosha mboga ya nusu kilo iliyopikwa kwa kutumia kuni ulizokata mti bure.
Huko kwa mabepari bei ya umeme ni sawa na bure yaani Kilowatt-hour moja bei yake haizidi TSH 30!
 
Awamu ya baba wa taifa na ile ya mzee ruhusa hakukuwa na changamoto la katika katika kwa umeme maeneo ambayo huduma hii ilikuwa imeyafikia. Ni kweli kwamba maeneo hayo yalikuwa hasa kwenye miji mikubwa ya nchi. Shughuli za kiuchumi wa viwanda hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa ambapo tumesambaza huduma hii ya umeme hadi kwenye karibu kila kijiji.

Jinsi uchumi wa viwanda ulivyozidi kukua na idadi ya watu kuongezeka, ndivyo changamoto ya umeme ilivyojitokeza na kukua kila kukicha. Zilianza hasa katika kipindi cha awamu ya tatu ya Mzee Mkapa ambaye suluhisho lake lilikuwa ni kuwapa kampuni ya makaburu wa South Africa kutuendeshea Tanesco yetu. Matokeo yake hatutayasahau. Tulipigwa tukapigika.

Ikaja awamu ya nne ya Mzee Kikwete. Wao wakaona suluhisho lake ni kukodi majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka makampuni ya nje ya nchi kama yale ya Richmond, Dowans, Symbion na IPTL. Tukapigwa na kupigika hadi Waziri mkuu akatimuliwa na bunge la Mzee Sitta.

Ikaja awamu ya tano ya Mzee Magufuli. Nayo ikahangaika kwa kubana mafisadi na kuanzisha mahakama ya mafisadi kama suluhisho la changamoto hili la umeme. Kwa kiasi fulani kukawa na ahueni ya kuonesha kuwa ile ndoto ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025 labda ingaliweza kutimia.

Sasa imekuja awamu ya sita ya Mama yetu Mzee Salmia inayopenda kushirikisha wananchi wote kupata suluhisho la changamoto mbali mbali ya wananchi kidemokrasia. Kwa kuwa umeme wa bei rahisi kuliko wote ni ule unaotokana na maji. Na kwa kuwa nchi yetu imejariwa mito mingi na kuzungukwa na maziwa makubwa makubwa mengi: kwa nini maji ya ziwa kama lile la Victoria yasipekwe kwa mabomba huko kwenye bwawa la Mtera na lile la Nyerere ili wakati wa ukame kwenye mabwawa hayo, yakafunguliwa kuyajaza? Ethiopia wanatumia maji ya ziwa Victoria kupitia mto Nile kuzalisha maelfu ya maelfu ya MW za umeme hadi kuwauzia Wakenya.

Kwanini sisi tusitumie Ziwa hili ambalo liko kwetu? Kwani ni shilingi ngapi kupeleka maji ya ziwa letu huko? Kama hatuna hizo hela, tutafute pa kukopa kwani manufaa ya mkopo huu ni mkubwa sana. Hili litakuwa ni suluhisho la once and for all ya changamoto hili la umeme.

Tutaweza hata kuuza umeme nje ya nchi na kuachana na kuuza mahindi na mchele nje ya nchi wakati tukiwa tuna njaa. Tutaweza kupunguza sana bei ya umeme ili wananchi wote waweze kuitumia kama nishati rahisi ya kupikia na hivyo kuachana na ukataji wa miti wakitafuta kuni na mkaa. Mwananchi ataweza kutumia shilingi zisizozidi elfu tano tu kwa mwezi kwa nishati ya kupikia ya umeme.

Tanesco nao wataweza kukusanya matrilioni ya pesa kwani kila mwananchi atakuwa mteja wao. Viwanda vingi vitajengwa na kuzalisha bidhaa nyingi kwa bei nafuu. Kwa muda mfupi nchi yetu itakuwa upper middle income country chini ya uangalizi wa mama!

NB: Umeme utokanao na gesi mara zote bei yake ni ya juu sana (unaffordable to many of our people) ukilinganishwa na ule unaotokanq na maji. Umeme wa gesi ni kwa wakati wa dharura tu au kwa kuuza nje.
Mie nawaza tu ikiwa sa hivi ni msimu wa mvua lakini maji ya kuzalisha umeme bwawani tunaambiwa hakuna je ikifika kiangazi itakuwaje?
Si ndo itakuwa mgao wa week kwa week
 
Sababu zao ni kigeugeu tu. Kiangazi utaambiwa kuna ukame, sijui ni kiangazi gani ambacho huwa hakina ukame, au definition ya kiangazi kwa tanesco siyo ile tunayoijua sisi. Wakati wa masika na mvua zikileta mafuriko maeneo mbali mbali ya nchi, tanesco watasema mabwawa yao hayana maji kwa sababu ya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vyake vya maji. Utadhani hizo shughuli za kibinadamu zimeanza leo. Kwa nini hizi shughuli za kibinadamu hazizuii haya mafuriko bali zinazuia tu maji kutoingia kwenye mabwawa ya tanesco. JPM alituambia kuwa mabwawa haya huwa yanafunguliwa kuchepusha maji yasijae.

Mara tunaambiwa miundo mbinu yote ya transmission inahitaji overhaul yote. Trilioni takriban 60 za pesa zitahitajika kwa zoezi hili ambalo litakamilika mwaka 2026. Yote haya yanaweza kuwa hujuma tu zenye malengo fulani fulani yakiwemo ya kisiasa. Yanahitaji ufumbuzi wa haraka. Hata kama maji ya Victoria yakipelekwa kule bado mabwawa hayo hayatajaa kama hujuma hizo bado zitakuwepo.
 
Awamu ya baba wa taifa na ile ya mzee ruhusa hakukuwa na changamoto la katika katika kwa umeme maeneo ambayo huduma hii ilikuwa imeyafikia. Ni kweli kwamba maeneo hayo yalikuwa hasa kwenye miji mikubwa ya nchi. Shughuli za kiuchumi wa viwanda hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa ambapo tumesambaza huduma hii ya umeme hadi kwenye karibu kila kijiji.

Jinsi uchumi wa viwanda ulivyozidi kukua na idadi ya watu kuongezeka, ndivyo changamoto ya umeme ilivyojitokeza na kukua kila kukicha. Zilianza hasa katika kipindi cha awamu ya tatu ya Mzee Mkapa ambaye suluhisho lake lilikuwa ni kuwapa kampuni ya makaburu wa South Africa kutuendeshea Tanesco yetu. Matokeo yake hatutayasahau. Tulipigwa tukapigika.

Ikaja awamu ya nne ya Mzee Kikwete. Wao wakaona suluhisho lake ni kukodi majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka makampuni ya nje ya nchi kama yale ya Richmond, Dowans, Symbion na IPTL. Tukapigwa na kupigika hadi Waziri mkuu akatimuliwa na bunge la Mzee Sitta.

Ikaja awamu ya tano ya Mzee Magufuli. Nayo ikahangaika kwa kubana mafisadi na kuanzisha mahakama ya mafisadi kama suluhisho la changamoto hili la umeme. Kwa kiasi fulani kukawa na ahueni ya kuonesha kuwa ile ndoto ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025 labda ingaliweza kutimia.

Sasa imekuja awamu ya sita ya Mama yetu Mzee Salmia inayopenda kushirikisha wananchi wote kupata suluhisho la changamoto mbali mbali ya wananchi kidemokrasia. Kwa kuwa umeme wa bei rahisi kuliko wote ni ule unaotokana na maji. Na kwa kuwa nchi yetu imejariwa mito mingi na kuzungukwa na maziwa makubwa makubwa mengi: kwa nini maji ya ziwa kama lile la Victoria yasipekwe kwa mabomba huko kwenye bwawa la Mtera na lile la Nyerere ili wakati wa ukame kwenye mabwawa hayo, yakafunguliwa kuyajaza? Ethiopia wanatumia maji ya ziwa Victoria kupitia mto Nile kuzalisha maelfu ya maelfu ya MW za umeme hadi kuwauzia Wakenya.

Kwanini sisi tusitumie Ziwa hili ambalo liko kwetu? Kwani ni shilingi ngapi kupeleka maji ya ziwa letu huko? Kama hatuna hizo hela, tutafute pa kukopa kwani manufaa ya mkopo huu ni mkubwa sana. Hili litakuwa ni suluhisho la once and for all ya changamoto hili la umeme.

Tutaweza hata kuuza umeme nje ya nchi na kuachana na kuuza mahindi na mchele nje ya nchi wakati tukiwa tuna njaa. Tutaweza kupunguza sana bei ya umeme ili wananchi wote waweze kuitumia kama nishati rahisi ya kupikia na hivyo kuachana na ukataji wa miti wakitafuta kuni na mkaa. Mwananchi ataweza kutumia shilingi zisizozidi elfu tano tu kwa mwezi kwa nishati ya kupikia ya umeme.

Tanesco nao wataweza kukusanya matrilioni ya pesa kwani kila mwananchi atakuwa mteja wao. Viwanda vingi vitajengwa na kuzalisha bidhaa nyingi kwa bei nafuu. Kwa muda mfupi nchi yetu itakuwa upper middle income country chini ya uangalizi wa mama!

NB: Umeme utokanao na gesi mara zote bei yake ni ya juu sana (unaffordable to many of our people) ukilinganishwa na ule unaotokanq na maji. Umeme wa gesi ni kwa wakati wa dharura tu au kwa kuuza nje.
Duh, sijaelewa
 
Akili hizi we ukipewa nchi, lazima tuingie kwenye vita na wamisri
 
Back
Top Bottom