Changamoto za barabarani usiku mkubwa

Changamoto za barabarani usiku mkubwa

Mimi nishatembea usiku kila sehemu sijaona hata kivuli achilia mtu, halafu hii picha kuona bango la kijani nyuma ya huyo mzungu nikajua tu picha ya kawaida.
 
Hii picha inasambaa kwenye magroup ya madereva. Kuna dereva mmoja kakutana na hii kitu akiwa safarini.
Mimi kuna siku natoka Tunduma kuja Mbeya nipo kwenye costa siti ya mbele SAA sita mchana jua Kali ghafla kwenye pori kaibuka mtoto miaka 5-7 kakatisha barabara dereva akamkwepa tukayumba sana ila hatukupinduka. Swali la abiria yale maeneo hakuna nyumba hata ya nyasi mtoto anatokea wapi?

Kila mtu akaanza kuomba dua yake.

View attachment 1781704
Niliwahi piga mmoja pale kati kati ya segera na mombo usuku wa saa 7 unusu hivi namwahisha mkuu wangu kwenye mkutano arusha aicc sikushika break wala nini na nikapita fresh tuu ila nilienda mbele kabisa kusimama natoka nje nakagua gari sikuona chochote tukaendelea na safari yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu ilimkuta hii akielekea Mikumi kutokea Iringa,alitokea mtu mbele akiwa kwenye speed kama 150kph usiku mkubwa,akihama upande wake na yule mtu anahama upande alikoendea,akili ya haraka ilikuwa ni kumgonga,anasema alisikia mshindo na akapita juu kwenye kioo cha mbele,hakusimama mpaka alipofika Mikumi akachukua Lodge,asubuhi akakagua gari yake hakukuta alama ya kugongwa wala damu,alipofika Dar aliuza ile gari maana alijua hayuko salama tena...
Mkuu huu ni oungo mtupu ni eneo gani Iringa mikumi unaweza kutembea 150km/hr Hilo la kwanza.

Kwa mwendo huo huwezi chezesha gari Kushoto kulia maana you only have less than sekunde tano tu. Hivyo ni uongo
 
Take it or leave it...
 
Dar Bagamoyo saa 8 usiku unakutana na mwanamke kavaa baibui jeusi peke yake katikati ya barabara unamfanyaje huyo? kadri unavyokaribia anasogea kurudi nyuma, sisimami.
Ndg yangu alikutana na hiyo kadhia, alichofanya akazima taa na kuwasha huku akiwa speed 110 hakuna kitu, uliza madereva wanasafirisha magazeti wakupe hadithi zao, hasimami mtu iwe mbuzi au mtu, mwisho wake unakuta hujagonga chochote ni vibweka vya njiani
Hatari sana
 
Nimekuwa Dereva wa Magari ya Mizigo kwa muda mrefu kidogo,hizi Barabara haswa za Bongo zina mauzauza mengi nyakati za Usiku mkubwa

Mchana pia kuna Mauzauza ila ni kidogo ukilinganisha na Usiku
 
Watanzania wengi mnaamini Sana ushirikina. Ukiangalia comments hapa utajua tulivyo na upeo mdogo.

Tutambue Tanzania tunaruhusiwa kutembea muda wowote usiku na mchana, hivyo kumkuta mtu usiku njiani Wala sio kitu Cha ajabu kukufanya umgonge.

Pili Tanzania sera yetu ya kutunza wagonjwa wa akili ni mbovu Sana. Kuna kichaa anatembea eneo la hifadhi ya mikumi Sasa ukikutana nae utasema ni msukule, kumbe kichaa tu. Hivyo hivyo na vichaa sehemu zingine za nchi.

Tatu Kuna watu wanafukuzwa kwa Ndugu zao usiku wanaamua kufanya maamuzi magumu kwenda kwa Ndugu zao kwengineko tukiwakuta tunataka kuwagonga eti wanga.

Mwisho Kuna walevi ambao wkaiwa wanatembea usiku kwenye Giza linapotokea gari ule Mwanga unawasumbua na kuwafanya waweweseke, tunataka kuwagonga eti ni wanga.

By the way wanga huwezi waona, wakitaka kukumaliza watakuja Kama punda, fisi, Ngombe etc ukiwagonga shida, ukiwakwepa shida
Mambo mengine kama huhui bora uulize kwahiyo ww ndounaupeo kuliko hao waliocoment tofauti naww
 
Mkuu huu ni oungo mtupu ni eneo gani Iringa mikumi unaweza kutembea 150km/hr Hilo la kwanza.

Kwa mwendo huo huwezi chezesha gari Kushoto kulia maana you only have less than sekunde tano tu. Hivyo ni uongo
We mgeni nn wa hiyo njia? Kuna vipande vingi tu vya kutembea speed kutoka Iringa to mikumi ila kwa uzoefu wangu havizid km 3 lazima ukutane na tuta ama kona kali
 
Maigizo au kweli?
Kuna kipindi huyo Dereva aliguna sasa hapo hayo yanaitwa machale kuwa huko unakoelekea kuna kitu kibaya

Mkuu mimi nilikuwa napeleka Mafuta Uwanja wa KIA nilipofika Korogwe nilikuwa nimechoka niasema nikalale Msambiazi yaani ilikuwa kazi sikulala nikaenda hadi Mombo
 
Watanzania wengi mnaamini Sana ushirikina. Ukiangalia comments hapa utajua tulivyo na upeo mdogo.

Tutambue Tanzania tunaruhusiwa kutembea muda wowote usiku na mchana, hivyo kumkuta mtu usiku njiani Wala sio kitu Cha ajabu kukufanya umgonge.

Pili Tanzania sera yetu ya kutunza wagonjwa wa akili ni mbovu Sana. Kuna kichaa anatembea eneo la hifadhi ya mikumi Sasa ukikutana nae utasema ni msukule, kumbe kichaa tu. Hivyo hivyo na vichaa sehemu zingine za nchi.

Tatu Kuna watu wanafukuzwa kwa Ndugu zao usiku wanaamua kufanya maamuzi magumu kwenda kwa Ndugu zao kwengineko tukiwakuta tunataka kuwagonga eti wanga.

Mwisho Kuna walevi ambao wkaiwa wanatembea usiku kwenye Giza linapotokea gari ule Mwanga unawasumbua na kuwafanya waweweseke, tunataka kuwagonga eti ni wanga.

By the way wanga huwezi waona, wakitaka kukumaliza watakuja Kama punda, fisi, Ngombe etc ukiwagonga shida, ukiwakwepa shida
Hapana unajua issue iko hivi. Fact ni kwamba maajabu yapo na watu wote tunajua kuwa yapo ila huwa siyo rahisi sana kuyashuhudia, japo tungependa sana kuyashuhudia. Kwa hiyo huwa inatokea linapotokea tukio lenye mkanganyiko kidogo, tunalazimisha kuwa ni maajabu ili huko mbele ya maisha yetu tukajiridhishe kwa nafsi zetu kuwa na sisi angalau tulishawahi kuyashuhudia maajabu yale ambayo watu huwa wanashuhudia kuwa yapo ila hatukuwa tumewahi kuyashuhudia hapo awali
 
Huyu atakuwa kichaa au pombe zimekubali.mzuka na camera havishikani[emoji23][emoji23].

Sema naandika huku ninaogopa.
nakumbuka siku moja usiku tunaenda klabu na bro usiku wa saa sita njiani tukamuona dada amemshika mkono mtoto wa umri km miaka 4.
nikamwambia bro simama tumpe lift uyo dada yupo na mtoto itakuwa anasafiri.
kwa huruma yetu tukampakia siti ya nyuma na mwanae..ajabu hatukumuuliza anapoenda sababu tulijua anasafiri na klabu na stendi ni njia hiyo hiyo!
tukawa tunapiga stori zetu kushtuka tushafika klabu!!daahh bro tumempitishia dada wa watu!!
kugeuka tumuombe radhi hakuna mtu huko nyuma...
nikamwambia jombaa tulipakia jini hamu ya klabu ikaisha tukageuza kurudi hom na njia tukabadili..
ungetuona tulivyokuw tunahaha njia nzima hakika ungecheka uzimie..ilifika sehem namwambia tuache gari tukimbie
 
We mgeni nn wa hiyo njia? Kuna vipande vingi tu vya kutembea speed kutoka Iringa to mikumi ila kwa uzoefu wangu havizid km 3 lazima ukutane na tuta ama kona kali
Hiyo njia
Hapana unajua issue iko hivi. Fact ni kwamba maajabu yapo na watu wote tunajua kuwa yapo ila huwa siyo rahisi sana kuyashuhudia, japo tungependa sana kuyashuhudia. Kwa hiyo huwa inatokea linapotokea tukio lenye mkanganyiko kidogo, tunalazimisha kuwa ni maajabu ili huko mbele ya maisha yetu tukajiridhishe kwa nafsi zetu kuwa na sisi angalau tulishawahi kuyashuhudia maajabu yale ambayo watu huwa wanashuhudia kuwa yapo ila hatukuwa tumewahi kuyashuhudia hapo awali
Ukiendesha gari muda mrefu ukaona macho yanataka kufunga lazimisha next ten km. Kisha uniambie utakuwa umeona vibwengo vingapi.

Unapochoka ubongo unatabia ya kutaka kushutdown (ni Kama radiator umepata Moto Sana gari huzima). Katika process hiyo macho hushurutishwa kufunga na hapa ndipo utaanza kuona vitu vya ajabu ajabu kwa sababu ushirikiano n aubongo umekuwa ndogo hivyo tafsiri za ilichokiona inaweza isitafsiriwe sawia, hivyo Calvert utaona Kama ni mbwa etc tukilazimisha kidogo ajali tunaanza kusema Kuna mtu alikatiza

Nocturnal wengi wanajua ukiendesha every 2.5 - 3hrs simama stretch kidogovuta sigara, kojoa hutakaa uone hivyo vibwengo Ila tutakutana na vitu vya kweli.

Mfano: maeneo ya hedaru mpaka Mwanga kukutana na punda ni jambo la kawaida sio miujiza ni wanyama kweli.

Njia ya mkuranga Lindi Kuna wabeba mkaa na magogo wa hatari jiandae, Morogoro kongwa jiandae na matrekta vicheche na waswaga Ngombe usiku Dodoma babati Arusha Ngombe, wanyama pori. Tabora Urambo Kaliua Uvinza mifugo na vinyama vya porini. Kila njia inachangamoto zake za kweli sio vibwengo.

Ingawa sipangani na ukweli kwamba hao washirikina hawapo la hasha Ila tahadhari ni muhimu Sana uweze kutofautisha story za vijiweni na reality
 
Back
Top Bottom