Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia


Kwanza kabla ya kutangatanga sana kwa wanawake tofauti kutafuta mtoto wa kiume unatakiwa uelewe kuwa baba ndiye anayepelekea mtoto kuzaliwa wa kike au wa kiume.

Kwa hiyo hapo kati yako wewe na mwanamke anayekuzaa watoto wa kike, anayesababisha watoto wazaliwe wa kike ni wewe si mwanamke.


"The father determines the sex of the baby. While the mother’s egg always provides an X chromosome, the father’s sperm carries either an X (resulting in a girl, XX) or a Y (resulting in a boy, XY) chromosome. Therefore, the specific sperm that fertilizes the egg determines the baby’s sex."
 
Samahani, hii ndio popo kanyea mbingu style?
 
Ipo hivi tajiri.
Mtoto wa kike sio wako. Ni wako tuu kumkuza, kumlea na kumpa maadili, kumlea kiroho na mwanzo wa maisha kumuandaa kuwa mke wa mtu mwingine, ambako atatawaliwa na kutumikishwa.

Kaa ukijua unawaandalia wajuba wake zao.

Akiolewa anaenda tengeneza mji mwingine, uwe umemsomesha au umempa mali. Anakwenda jenga mji wa wengine na watanufaika nae huko na yeye kuwa mwanaukoo wa huko.

Mtoto wa kike haendelezi ukoo/familia/jina la ukoo wako, hana jina, hilo jina lako la ukoo ulilompa mfano Shirima ni geresha tuu, akiolewa na Mushi, anabadiri kuanza kuitwa Mushi. 😁

Mtoto wa kike, atamjali mama yake hata akija kuwa na mji wake au kazi yake, mama yake ataangaliwa sana kuliko wewe, hasa nguvu zako zikiisha yaani uzeeni. Angalia familia nyingi mama akifa, watoto wa kiume ndio wanabaki na mshua wao.

Mtoto wa mtoto wa kike (Mjukuu) sio wako, huna haki nae atakapo kuwa mkubwa, huwezi kumrithisha wala kuwa na maamuzi nae, wala hatabsikiliza neno lako, utakuwa babu tuu wa yeye kuja kunufaika na mali zako na kutembea. Wala hawezi jenga mji wala kuendeleza uzao/jina lako. Mjukuu wa kiume mwenye akili atakuwa na uchungu na babu, maana ndie damu yake, patakuwa panamuuma.

Swai hawezi kuja kujenga kwa akina Laswai, ni watu tofauti hawa, hawa kwa mwanaume hawa kwa mwanamke. Huwezi kujenga ujombani jomba, uliona wapi hiyo bwashee, unajenga ubabani. Ubabani ndio kuna kuhusu bwashee. 😁

Utaishi maisha ya upweke sana uzeeni, hutakuwa na right-hand men wa kukusaidia, kuongea nao, kukulinda, kukushauri kiume, kuwapa siri zako na mbinu zako za kuishi ili kuendeleza mali na ukoo.

Hutakuwa na warithi kisheria. Mwisho wa siku mali hizo zitaenda kwa wengine kupitia "chupi" yaani mtoto wa kike anachukua mali kwao na kuwapa watoto wake ambao sio wanaukoo.

Hutakiwa na "succession plan" ya mali, kizazi na mipango yako. Ukifa watu wanagawana fito. Watoto wa kiume watakomaa kuendeleza legacy yako. Mali, kampuni, hisa n.k

Wajukuu wa mtoto wa kike, hawatakuheshimu na kukupa uzito uzeeni kama babu yao, achilia mbali kukutunza. Watamtunza babu hao mzaa baba ambae ni "maternal grandparents" wanaitwa jina lake na wanaweza kumrithi, kiafrika babu mzaa baba anarithisha mali kwa wajukuu zake wa kiume.

Hutaweza kuwapa jina watoto wa mtoto wa kike. Achilia mbali kupewa kitovu chake wala kumfisha akifa.

Mtoto wa kike akifa, wewe unaenda msibani kama jirani, atazikwa ukweni na jina lake litaandika la mumewe. Kam unakaa kijiji A, utalazimika kwenda kijiji B kuzika mwanao, ukifika hapo utapewa jina la baba wa mwanamke, mkwe, mkamwana. Na majina mengine ya kukutenga.

Nyumbani kwa mtoto wa kike, utaenda kama mgeni kusalimia na hutaruhusiwa kukaa hapo, hata mkweo akiwa mwema vipi. Hutajisikia amani na uhuru wewe kukaa hapo. Kwa mtoto wa kiume ni kwako, na unaweza kaa hapo kwa amani maana utakuwa upo kwa mwanao yaani kitovuni kwako.
 
Nafahamu hilo. Kwa namna yoyote ile atapatikana wa kiume. Nimepokea ushauri wako.
 
Kwetu hakuna ushoga so sitalea mtoto awe shoga UKOME kuniambia hivyo. Ninachotaka niwe na mrithi. Akiwa jambazi tapeli, jambazi au mwizi ni wangu nitaenda kumuwekea dhamana na kumtoa jela.
Mzee usiseme hivo, yaache tu, Kuna kijana huku, kamuua mama yake, kwa kumchoma, kisu, Kuna kijana Arusha alikua mtukutu, wazazi wanamtetea kaja kaanza kuwapiga wote na ni wazee
 
Picha imenifurahisha kwa kweli, mwanaume anaingia kwa mbwembwe matatizoni πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
- umeandika kwa mtazamo wa mwaka 1970
-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…