Changamoto za mfumo wa maombi ya ajira za Elimu na Afya 2022

Maswali ni mengi,majibu ya watu hata wa stationery hayatoshelezi,hivi kwa wale walioomba kipindi cha nyuma,wanatumia zilezile akaunti za zamani au wanafungua akaunti mpya?
Endapo ikiwa ni akaunti za zamani zinatumika,ni mabadiliko gani yanafanyika katika viambatanisho vilivyomo?
 
unatakiwa kufungua akaunti mpya utabonyeza JISAJILI kama picha inavyoonyesha hapo chini
baada ya hapo utaingiza email yako kisha hakikisha pasword unayoweka inamchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo alama za uandishi pamoja na namba.... mfano 123@MHAndo utaweka na namba yako ya simu
kisha itafuata sehemu ya kuthibitisha taarifa zako za NIDA hapo utaingiza namba yako ya nida yatafuata maswali...ili wawe na uhakika kama wewe ndio mwenye namba hiyo ya nida...ukivuka hapo utakuwa teyari umeshafungua akaunti....

baada ya kufanikiwa kufungua akaunti ukitaka kulog in utaingiza namba yako ya nida bila vile vialama vya toa... mfano 200021214120000824
 
Mtandao ulikubali Kama dakika hvi afu ukasepa
 

Asante sana ndugu yangu,kwasasa mtandao unasumbua,naomba nikisumbue tena,Je nikibonyeza jisajili,nitakutana na taarifa zangu zilezile za zamani au ntaanza upya mambo ya kuattch sijui vyeti na viambatanisho vingine,na je kuna mabadiliko yoyote ya kuongeza au kupunguza endapo kama nikiingia kwenye mfumo nikazikuta taarifa zilezile za awali?
 
Unaanza upyaaaaaaaaaaa
 
Ukiingiza hiyo username na password unaambiwa unauthorised user
 
hapana unaanza upya taarifa za zamani huto zikuta...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…