Chanika ni kama unaenda mkoa mwingine

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
St anno amekuwa na attitude mbaya na hizo wilaya. Hajawahi kuiona kijichi huyu
 

Attachments

  • 20240626_161502.jpg
    804.3 KB · Views: 3
hukupoteza nauli kweli mkuu?
 
Huwezi kufananisha na kibaha mzee, kuna haja watu washuke kuchimba dawa kama gari itatokea kariakoo utake usitake
Mkuu hii mada tukiiweka kwa muktadha kwamba tubishane mimi nitakuachia ushindi.

Lakini ukweli mtu anayetoka lets say Posta kupandisha Kibaha humfananishi na anayeenda Chanika,akikamata Mwendokasi mpaka Mbezi ni 40min Mbezi akikamata coaster mpaka Kibaha hazizidi 25 to 30 minutes anashuka Kibaha sasa muda huo anayeenda Chanika kama kasogea sana atakuwa yupo Kipawa,well kinachowabeba watu wa Morogoro road ni Mwendokasi but still Chanika hata huo Mwendokasi wa G/Mboto ukianza bado patakuwa mbali
 
Kipawa ndo nashindaga mm kila siku.. kutoka posta kwenda kipawa haifiki 30 min. Wewe kweli unataka tushindane.. na mm ndo kinachoniweka mjini hiko! Nakuagizia popcorn hapa
 
na foleni pale airport duh
 
na foleni pale airport duh
Chanika nina dada'angu mpaka leo hatuongei vizuri harusi yake ilifanyika huko na mimi niliteuliwa kama mtoa neno wa familia nikaondoka Kariakoo saa tisa kipindi hicho Chanika mgeni nikijua nitawahi.

Barabarani foleni changanya na umbali nilifika ukumbini nikakuta wanakula tena na chakula nikakosa,mimi mtu anaeishi Chanika namuheshimu wale wana uvumilivu wa kipekee.
 
Yeah Kijichi kule watu wanaishi lakini Chanika wengi ni wale tunaoishi tukingoja siku zetu tutwaliwe.

Nimewahi kufika mara moja 2020 Kijichi ina hadhi ya kuitwa makazi ya watu.
Inaonesha watu wa humu mnapemda sana low density areas. Maeneo mengi yanayouzwa bei rahisi yani 1m to 3m hayafai kuwa low density mana kipande kidogo cha eneo kina watu kibao. Miguu 15 mpaka 20. Hili jambo haliwez kuingiliwa hata na mipango miji mana wauzaji ni wazawa

Kwa muktadha huu, jiji linataka liw na watu wa kipato cha kati na juu pekee. Hii ni mitazamo ya kibepari, so toa neno "hadhi" weka neno lingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…