Mrejesho - day 1 (2nd Aug):
Nitapata chanjo yangu inshallah pamoja na washirika wangu makwetu. Hili si zoezi la kukosa mimi na wote niwapendao. Hayawi hayawi hatimaye huenda yatakuwa.
Tumefika kujiandikisha 08:00: wenye magonjwa mengine na wazee 50+ kwa mujibu wa waraka wa wizara.
Karibu Tanzania. Huku ndiko Dunia iliko:
1. Pana watu kwenye makundi lengwa wangali hawana vitambulisho vya Nida wala namba za Nida.
2. Kwenye kundi #1 wapo pia wengine ambao hawana vitambulisho vingine vyovyote katika vilivyotajwa kwenye waraka.
3. Katika walengwa kuna vikongwe 100+ wa kubeba kuwasogeza hata kwa umbali wa mita 1.
4. Katika walengwa wapo wasiokuwa na simu achilia mbali smartphone ya kujisajili online.
5. Maelekezo ya kujisajili mitandaoni kwa hakika hayana cha kufanya na Tanzania hii.
Mwitikio wa watu kujiandikisha ni mkubwa sana. Uhamasishaji haukuwa mdogo. Ni muhimu wote hawa wakawezeshwa kupata chanjo hii bila kukosa.
Itakuwa si haki kwa watu hawa wanaoihitaji chanjo kufanywa binadamu daraja la 2.
Nilipata nafasi ya kusema mawili matatu na maafisa waliokuwa wanafanya usajili huo. Nikidhani kuwa hatarini walikuwa ni wazee na wenye magonjwa mengine peke yao.
Haya ndiyo yaliyokuwa majibu yao:
"Mnadhani wanaokufa na ugonjwa huu ni wazee peke yao? Mbona vijana wengi tu nao unawaondoa?"
Bado sijachwanjwa labda hadi kesho. Tumeambiwa tutapigiwa simu. Bado hatujapata confirmation. Bado tunasubiri. Bado hatuachanjwa hadi tutakapokuwa nimechanjwa.
"Kama wasafiri bado tungali tuko njiani" -- King Kikki.
"We are standing by."