#COVID19 Chanjo - Mrejesho: Wizara tambueni changamoto hizi

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mrejesho - day 1 (2nd Aug):

Nitapata chanjo yangu inshallah pamoja na washirika wangu makwetu. Hili si zoezi la kukosa mimi na wote niwapendao. Hayawi hayawi hatimaye huenda yatakuwa.

Tumefika kujiandikisha 08:00: wenye magonjwa mengine na wazee 50+ kwa mujibu wa waraka wa wizara.

Karibu Tanzania. Huku ndiko Dunia iliko:

1. Pana watu kwenye makundi lengwa wangali hawana vitambulisho vya Nida wala namba za Nida.
2. Kwenye kundi #1 wapo pia wengine ambao hawana vitambulisho vingine vyovyote katika vilivyotajwa kwenye waraka.
3. Katika walengwa kuna vikongwe 100+ wa kubeba kuwasogeza hata kwa umbali wa mita 1.
4. Katika walengwa wapo wasiokuwa na simu achilia mbali smartphone ya kujisajili online.
5. Maelekezo ya kujisajili mitandaoni kwa hakika hayana cha kufanya na Tanzania hii.

Mwitikio wa watu kujiandikisha ni mkubwa sana. Uhamasishaji haukuwa mdogo. Ni muhimu wote hawa wakawezeshwa kupata chanjo hii bila kukosa.

Itakuwa si haki kwa watu hawa wanaoihitaji chanjo kufanywa binadamu daraja la 2.

Nilipata nafasi ya kusema mawili matatu na maafisa waliokuwa wanafanya usajili huo. Nikidhani kuwa hatarini walikuwa ni wazee na wenye magonjwa mengine peke yao.

Haya ndiyo yaliyokuwa majibu yao:

"Mnadhani wanaokufa na ugonjwa huu ni wazee peke yao? Mbona vijana wengi tu nao unawaondoa?"

Bado sijachwanjwa labda hadi kesho. Tumeambiwa tutapigiwa simu. Bado hatujapata confirmation. Bado tunasubiri. Bado hatuachanjwa hadi tutakapokuwa nimechanjwa.

"Kama wasafiri bado tungali tuko njiani" -- King Kikki.

"We are standing by."
 
na sisi tusio kwenye makundi maalum watupe utaratibu, ni lini tunapata chanjo?

Hii kitu ni kujidanganya kuwa hauko kwenye kundi maalumu. Hapa chanjo walete za kutosha wote wanaotaka wachanjwe:

IMG_20210720_114420_251.jpg

Hii ya kupigana hadithi kuwa haumo kwenye kundi maalumu wakati mpiga hadithi amekwisha chanjwa mbona wala hailipi?
 
Hivi wale waliokufa baada ya kuchanjwa wenyewe wanasemaje>

Kumbuka ukichanjwa leo inachukua siku kadhaa kwa kinga kuzalishwa. Chanjo ni kichocheo cha kuzalishwa kwa kinga mwilini. Chanjo si kinga yenyewe.

Waliokufa kwa Corona baada ya kuchanjwa, wenyewe wanasema hivi:

"1. Tupo tulioshambuliwa na Corona kabla ya kinga kuzalishwa mwilini
2. Tupo tulioshambuliwa na Corona kabla ya kinga ya kutosha kuzalishwa mwilini
3. Tupo tulioanguka kwenye wale wachache tulioangukia katika wale wa kwenye failure rate ya chanjo.

Mfano kama chanjo ni 96% efficient basi sisi ni katika 4 kutokea katika 100 ambao aghalabu labda wangekufa wote bila chanjo.
4. Tupo tuliokuwa kwenye hatari zaidi ambao tungekufa tu hata bila Corona, kwani tuko kwenye hatua zetu za mwisho na magonjwa mabaya kama ya moyo, cancer nk.
5. Nk."

Kujua kamili kila aliyekufa kwenye mazingira yake, hayo ni vizuri ukajinasibu kumwuliza mfu mwenyewe.
 
Ukipata madhara uje tukuchangie wale vimbelembele 10 wa mwanzo tutawachangia

Pamoja na kuwa sihitaji mchango wa mtu awaye yote, nitaleta mrejesho kamili sawia kama itakavyokuwa.

Ni mawazo finyu sana, tena ya Kimaskini hohehahe uliopitiliza haya:

"Ukipata madhara uje tukuchangie wale vimbelembele 10 wa mwanzo tutawachangia"

Kwamba mawazo ni kwenye madhara? Mawazo kwenye michango?

Hiiiiii bagosha!

Iko hivi, "ni heri nipate madhara hasi na chanjo, kuliko kuwa bila madhara huku nikiishi kwa mang'amung'amu na gonjwa hili lisilosikia dawa."

Habari ndiyo hiyo.
 
Nitapata chanjo yangu inshallah pamoja na washirika wangu makwetu. Hili si zoezi la kukosa mimi na wote niwapendao. Hayawi hayawi hatimaye huenda yatakuwa.

Tumefika kujiandikisha 08:00: wenye magonjwa mengine na wazee 50+ kwa mujibu wa waraka wa wizara.

Karibu Tanzania. Huku ndiko Dunia iliko:

1. Pana watu kwenye makundi lengwa wangali hawana vitambulisho vya Nida wala namba za Nida.
2. Kwenye kundi #1 wapo pia wengine ambao hawana vitambulisho vingine vyovyote katika vilivyotajwa kwenye waraka.
3. Katika walengwa kuna vikongwe 100+ wa kubeba kuwasogeza hata kwa umbali wa mita 1.

Mwitikio wa watu kujiandikisha ni mkubwa sana. Uhamasishaji haukuwa mdogo. Ni muhimu wote hawa wakawezeshwa kupata chanjo hii bila kukosa.

Itakuwa si haki kwa watu hawa wanaoihitaji chanjo kufanywa binadamu daraja la 2.

Nilipata nafasi ya kusema mawili matatu na maafisa waliokuwa wanafanya usajili huo. Nikidhani kuwa hatarini walikuwa ni wazee na wenye magonjwa mengine peke yao.

Haya ndiyo yaliyokuwa majibu yao:

"Mnadhani wanaokufa na ugonjwa huu ni wazee peke yao? Mbona vijana wengi tu nao unawaondoa?"

Bado sijachwanjwa labda hadi kesho. Tumeambiwa tutapigiwa simu. Bado hatujapata confirmation. Bado tunasubiri. Bado hatuachanjwa hadi tutakapokuwa nimechanjwa.

"Kama wasafiri bado tungali tuko njiani" -- King Kikki.

"We are standing by."
Agiza dawa hii ya kinga na tiba. Achana na haya madude. Wewe si pany a buku wa kufanyiwa majaribio

Namba za simu zinapita hapa chini.

Unajua baada ya madhara haya ya muda mfupi, miaka ijayo utakuwa bado binadamu? Utazaa watoto binadamu? Wa aian gani?
 
Sina bundle la kupoteza kusikiliza utopolo.

Samahani lakini.

Ningali bado sijapata simu yao ya miadi. I am standing by. Watokee au wasitokee kesho ninatia timu mzima mzima.

"Janssen" chanjo ya bure toka kwake beberu - kwa hisani ya watu wamarekani hivi sasa ndiyo habari ya mjini!

Habari yote iko hapa:

IMG_20210720_094159_438.jpg

Habari ya chanjo itakuwa kwangu historia baada tu, ya kuipokea chanjo.
 
Mkuu watasemaje kwa nani wakati WAMEKUFA? au unamaana kwamba watasemaje kwa MUNGU?

Hao ni chawa yule bwana wametugharimu maisha ya watu wengi. Walipendelea sote tufe ili labda siku moja tusije kuwa hoji.
 
Hadi sasa 20:30 si mimi wala wenzangu (timu ya zaidi mtu takribani 40) aliyepokea simu yoyote kuhusiana na miadi yetu ya chanjo kesho kinyume na ahadi tuliyokuwa tumepewa.

Hata hivyo nguvu moja kesho tunakwenda 08:00 bila kukosa kupata kusikia mbivu na mbichi zitakuwa zipi.

Pamoja na yote, mimi na smartphone yangu kama asemavyo beberu:

"I am standing by."
 
Agiza dawa hii ya kinga na tiba. Achana na haya madude. Wewe si pany a buku wa kufanyiwa majaribio

Namba za simu zinapita hapa chini.

Unajua baada ya madhara haya ya muda mfupi, miaka ijayo utakuwa bado binadamu? Utazaa watoto binadamu? Wa aian gani?

Hiyo dawa imefanyiwa majaribio wapi ? Madhara ya muda mrefu yapoje ?
Ndani inakitu gani na unaweza kuhakiki kilichowekwa ?
Tunaweza kuuliza maswali tunayouliza kuhusu chanjo kuhusu dawa hii pia !
 
Kumbuka ukichanjwa leo inachukua siku kadhaa kwa kinga kuzalishwa. Chanjo ni kichocheo cha kuzalishwa kwa kinga mwilini. Chanjo si kinga yenyewe.

Waliokufa kwa Corona baada ya kuchanjwa, wenyewe wanasema hivi:

"1. Tupo tulioshambuliwa na Corona kabla ya kinga kuzalishwa mwilini
2. Tupo tulioshambuliwa na Corona kabla ya kinga ya kutosha kuzalishwa mwilini
3. Tupo tulioanguka kwenye wale wachache tulioangukia katika wale wa kwenye failure rate ya chanjo.

Mfano kama chanjo ni 96% efficient basi sisi ni katika 4 kutokea katika 100 ambao aghalabu labda wangekufa wote bila chanjo.
4. Tupo tuliokuwa kwenye hatari zaidi ambao tungekufa tu hata bila Corona, kwani tuko kwenye hatua zetu za mwisho na magonjwa mabaya kama ya moyo, cancer nk.
5. Nk."

Kujua kamili kila aliyekufa kwenye mazingira yake, hayo ni vizuri ukajinasibu kumwuliza mfu mwenyewe.
Vipi unalipwa nini? Naona uko busy na chanjo za corona as if wewe ndiyo mzalishaji wa chanjo hizo.
 
Mkuu wa wilaya ya temeke yupo kundi lipi? Ana umri Gani ?

Umri si kigezo pekee mkuu kuhusiana na waraka wa wizara. Kumbuka magonjwa mengine nayo hayakuachwa nyuma.
 
Vipi unalipwa nini? Naona uko busy na chanjo za corona as if wewe ndiyo mzalishaji wa chanjo hizo.

Hauoni wewe changamoto ambazo wizara ya afya inatakiwa kuzishughulikia ili wote wanaotaka chanjo kwa hiari yao waweze kuipata na kwa raha zao?

Yale mambo ya nyungu, mikaratusi, malimao, michai chai na yale matango pori. Vipi mngali mnaendelea nayo?

IMG_20210614_192655_399.jpg

Hivi kwani mlikuwa mnalipwa pesa mlipokuwa mkipotosha watu?

Msisahau, kwa kila kifo tutawawajibisha hata kama mtakuwa makaburini kama yule bwana. Hii pia ni hata kama nasi tutakuwa makaburini.

Corona: Orodha ya wahanga, sampuli

Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom